Kwanini nayapinga makafara?

Kwanini nayapinga makafara?

Mbuzi anayechinjwa lazima atimize Miezi 6, Kondoo mwaka 1, Ng?ombe miaka 3, Ngamia miaka 5

Mkusanyaji S. Hussein

NENO UDHIYYAH la Kiarabu linatokana na mzizi wa herufi tatu daad-haa-alif, ambazo huwakilishwa kama d*h.*aa yenye maana ya katikati ya Asubuhi.

Maana ya kilugha ya al-udhiyyah ni mnyama anayechinjwa siku ya Id-ul-Adha. Kisheria, udhiyyah maana yake ni mhanga unaofanywa kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu katika siku mahususi na kwa kutimiza masharti fulani.

Mnyama yoyote achinjwaye siku nyingine kwa ajili ya Mwenyezi Mungu si udhiyyah. Hata mnyama anayechinjwa siku ya Idd Kubwa lakini bila kuelekeza nia kwa Mwenyezi Mungu kama vile mnyama anayechinjwa kwa ajili ya kuuzwa buchani, huyo si udhiyya.

Kuchinjwa huko kwa udhiyya katika masiku ya kuchinja (ayyam al-nahr, tarehe 10, 11, 12 na 13 ya Dhul-Hijja) ni jambo lililoamrishwa katika Uislamu kuwa ni sehemu ya ibada ya Hijja.

Qur?an, Sunna na Ijmaa vyote vinathibitisha jambo hilo. Kwa upande wa Qur?an, Mwenyezi Mungu, katika sura ya 108-Al-Kawthar, aya ya pili, anasema, ?Basi swali kwa ajili ya Mola wako, na uchinje (kwa ajili ya Mola wako)?.

Hiyo ni amri iliyotolewa kwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, ambayo inasimama kama amri kwa waumini wote. Kwa upande wa Sunna ya Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, ilikuwa ni mila yake na mila ya Maswahaba wake na wafuasi wao waandamizi kuchinja mnyama (mara nyingi kondoo) katika Siku ya Idd Al-Adha.

Zipo riwaya nyingi mno za Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, zinazothibitisha kuwa Mtume na Maswahaba wake walichinja Siku ya Idd na kuwaamrisha wengine kufanya hivyo.

Hekima ya Al-Udhiyyah haiwezi kufahamika kwa wanadamu kwa ukamilifu. Hata hivyo, sehemu fulani ya hekima hiyo yaweza kufahamika. Mosi, ni ishara ya shukurani kwa Mwenyezi Mungu kwa kuumba.

Pili, ni uhuishaji wa mila ya Ibrahim (as), Baba wa Manabii. Hivyo, Muumini anapochinja, anakumbushwa namna Ibrahiim (as) na Ismail (as) walivyotii kwa subira kubwa amri ya Mwenyezi Mungu.

Utii wa Ibrahim kukubali kumchinja mwanawe kipenzi, na utii wa Ismail kukubali kuchinjwa ni masomo kwa Waumini kwamba wawe tayari kuvitoa vipenzi vyao na kuyatoa muhanga maisha yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Tatu, Al-Udhiyyah ni tendo linalopingana waziwazi na wale wanaosema kuwa ni haramu kwa wanadamu kuchinja wanyama na kula nyama kwani kitendo cha kuwachinja kinawaumiza wanyama na kinahujumu utukufu wa maisha yao.

Nne, Al-Udhiyya inabainisha kuwa njia ya huruma zaidi ya kumuua mnyama ni kumchinja. Na tano, Al-Udhiyya inazidisha shukurani ya Muumini kwa Mwenyezi Mungu kikiwa ni kiashiria cha namna Mwenyezi Mungu alivyoutiisha ulimwengu kwa wanadamu na kuuhalalisha uhai wa wanyama kwao ili wapate manufaa mbalimbali.

Kwa undani wake, udhiyyah ni ibada iliyokokotezwa katika Sunna ya Mtume, swallallahu alayhi wa sallam. Ni Sunna Mu?akkadah, hivyo ndivyo idadi kubwa ya Maulamaa wanavyosema.

Masharti yake ni pamoja na mtu anayechinja lazima awe Muislamu, awe mkaazi, na asiwe msafiri, awe mtu mwenye uwezo kifedha, awe mtu mzima na mwenye akili timamu.

Masharti ya kuswihi kwa Udhiyyah ni pamoja na mnyama anayechinjwa awe yule anayefugwa; ng?ombe, kondoo, mbuzi, nyati maji na kadhalika, mnyama anayechinjwa lazima awe ametimiza miezi 6 ikiwa ni mbuzi, mwaka mmoja ikiwa ni kondoo, miaka 3 ikiwa ni ng?ombe, na miaka 5 ikiwa ni ngamia, mnyama asiwe na hitilafu hasa zile zinazoweza kuathiri nyama yake.

Muda wa kuchinja huanzia Alfajiri, hata hivyo, uchinjaji uanze baada ya Swala ya Idd. Sunna ya kuchinja ni kuiacha damu ya mnyama imwagike. Ugawaji wa nyama ni kwamba; theluthi moja ni sadaka ya masikini, theluthi moja ni zawadi kwa majirani, ndugu na jamaa, na theluthi moja kwa ajili ya nyumbani kwa mtu mwenyewe.

Mgawanyo uwe sawasawa lakini kama mahitaji ya nyumbani ya mchinjaji mwenyewe ni makubwa, basi mchinjaji achukue sehemu kubwa. Au kama ana ndugu fukara wa nasaba, basi sehemu kubwa wawape ndugu. Kama yeye mwenyewe si muhitaji wa nyama hiyo, basi sehemu kubwa atoe Swadaka.
Aamin.
 
Mi naona waendelee tu... Maana ndo wanaotusaidia kwenye huduma za kijamii
 
Kafara ni nini?
Agano ni nini?
Mkataba ni nini?

Kafara ni sadaka ya damu kwa mizimu/ mashetani au Roho chafu zilizo kinyume na Mungu.

Agano ni makubaliano yanayoingiwa Kati ya mtoa kafara na mtolewa kafara, ili mtoa kafara aweze kufaidika kwa mambo kadha wa kadha iwe utajiri, mafanikio nk.

Mkataba ni hati fungani inayobeba masharti na adhabu atakazopata mtoa kafara iwapo ataenda kinyume na agano.
Adhabu za kuvunja maagano huathiri mvunja Agano na vizazi vyake vyote.
Mateso Mengi ya watu wa Leo yamwtokana na adhabu ya kuvunjwa kwa maagano Kati ya mababu na mizimu yao.
Umeichambua vizuri mno Nazjaz
 
Kwani bila hzo kafara huwezi kufanikiwa?ipi njia sahih yakumiliki utajiri bila hzo kafara?je matajiri wote wanatoa hzo kafara?msaada pls?
Inawezekana kufanikiwa lakini mchakato ni mrefu sana na kujitoa sana hivyo wengi hupendelea short cut
 
Kwani MUNGU hajawahi kutolewa kafara?
Kafara ni nini?
Agano ni nini?
Mkataba ni nini?

Kafara ni sadaka ya damu kwa mizimu/ mashetani au Roho chafu zilizo kinyume na Mungu.

Agano ni makubaliano yanayoingiwa Kati ya mtoa kafara na mtolewa kafara, ili mtoa kafara aweze kufaidika kwa mambo kadha wa kadha iwe utajiri, mafanikio nk.

Mkataba ni hati fungani inayobeba masharti na adhabu atakazopata mtoa kafara iwapo ataenda kinyume na agano.
Adhabu za kuvunja maagano huathiri mvunja Agano na vizazi vyake vyote.
Mateso Mengi ya watu wa Leo yamwtokana na adhabu ya kuvunjwa kwa maagano Kati ya mababu na mizimu yao.
 
Ivi kitimoto anafaa kutolewa kafara wanajamvi????maana simikiii watu wakimtaja zaidi ya mbuzi .ngamia na ng'ombe!!!
 
Mshana naomba uje na mada ya inayohusu nini hasa waganga wanafanya kumkinga mtu dhidi ya wachawi,Kinga mbalimbali na nguvu zake.

Halafu malizia kwanini mtu asitumie Kinga za waganga, thanks
 
Mshana naomba uje na mada ya inayohusu nini hasa waganga wanafanya kumkinga mtu dhidi ya wachawi,Kinga mbalimbali na nguvu zake.

Halafu malizia kwanini mtu asitumie Kinga za waganga, thanks
Nipe muda
 
.
tapatalk_1560790915387.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom