Kwanini mwanaume ukikosa kazi mwanamke anakusimanga sana?

wenzetu huwa na wasiwasi sana ktk wakati mgumu,mwanamke hupaniki haraka sana,(hasa akiwaza kuhusu mustakabali wa familia)kumbuka wanawake wengi wana amini kuwa wewe mwanaume ndo kila kitu katika familia hata kama yeye anafanya kazi anajiona yeye hana ubavu wa kuiendesha familia,hupelekea kuwaza vitu vingi sana,anakuja kuharibu zaidi anapokwenda kutafuta ushauri kwa marafiki zake..!!ni jukumu lako mwanaume kumuelewa na kufanya jambo litakalompa tena matumaini!!
si kweli,unataka kusema hawajielewi hawana akili? ukweli ni kwamba wao wana akili kama sisi na pengine kutuzidi ndo maana unaona wapo wanawake maprofesa,marais,huwajui vizuri wanawake acha kutetea usichokijua.
 
Wanaume muombe sana mpate wake wema,.msiseme tuu tuna roho mbaya au wabinafsi,kila mtu ni mbinasi na hii ni hulka kwa jinsia zote...mke mwema humstiri mumewe wakati wa changamoto za kimaisha hawezi kumuacha aaibike hata mara moja tena kwa wakati kama huo huongeza juhudi katika kazi ili kuziba mapungufu yaliyojitokeza,.
Safi sana. Umenifanya ni tabasamu.
 
Hata Mimi waifu kipindi sipati tender alishaanza kuniambia inabidi nitafute Kazi vinginevyo hatutofika......ila wakati nilivokua nakwarua mitenda ya maana alikua ananisifia kwa uamuzi wangu Wa kujiajiri teh......
 
Nina jamaa yangu amefukuzwa kazi baada ya kubainika alikuwa na cheti ambacho si chake, kwakweli jamaa yupo kwenye wakati mgumu maana ni miezi mitatu tu imepita lakini anaona kama miaka 10 ya mateso katika familia yake.

Shemeji yani mkewe ni mtumishi lakini amekuwa akimsema na kumsimanga sana kwa maneno na kuwa na mgogoro kila siku ndani ya nyumba hakuna amani.

Imefikia hatua jamaa anasema mkewe anamwambia mwanaume gani wewe ukizingatia jamaa wakati alipokuwa kazini alimjali sana mkewe kwa matumizi yote ya msingi na familia kwa ujumla.

Nimejiuliza huu ubinafsi wa kiwango hiki kwa wanawake kweli jamani mbona ni roho mbaya sana hii. Sidhani kama mkewe ndio angefutwa kazi jamaa angemnyanyasa kiasi hiki.

Hili ni funzo kwa sisi wanaume tuliooa na ambao mnatarajia Kuoa. Tuishi na hawa viumbe lakini kwa tahadhari kubwa sana ukikosa kazi kinachofuata ni masimango na kashfa za kila aina.

NB: Kwa wale wanawake wachache ambao ni wavumilivu kwa wenzi wao nawapongeza na nawaomba waendelee na moyo huohuo. Na kwa wale wenye tabia kama hii niliyoelezea hapo juu jirekebisheni.
Du! Pole sana mkuu
 
Na kuna wanaume wanawanyanyasa wanawake pia wakati wakiwa na hela, nina rafiki yangu alikua na kazi nzuri anahudumia familia vizuri hadi mama wa mwanaume anahudumiwa siku alipoacha kazi sababu mimba ilikua inamsumbua mno alinyanyaswa na mwanaume mpaka sasa hivi na ndoa imevunjika. So hii kitu inatokea pande zote mbi.
 
Hujawahi kukumbwa na masahibu. Unaongea ukiwa na afya njema na kazi unayo. Ila ipo siku
Ndo utafute ukiwa mzima. Huku ukijua ipo siku yatakukumba majanga. Hapo utakuwa unaishi kwa vitega uchumi vyako. Au bro we Marioooo design ya kina IYOBO!
 
Ndo utafute ukiwa mzima. Huku ukijua ipo siku yatakukumba majanga. Hapo utakuwa unaishi kwa vitega uchumi vyako. Au bro we Marioooo design ya kina IYOBO!
Vyovyote utakavyoandika lkn haujajua nini maana ya maisha. Walikuwepo watu wenye hela na viburi zaidi yako ww lkn leo ninavyoandika hata chakula nyumbani ni shida.
Hongera. "aliyekupa ww kiti ndiyo aliyenipa mimi kuti''
Haujajua nini maana ya maisha. Kwenye maisha hata vitega uchumi huisha. Haya maisha ww yaache km yalivyo. Ukipata ww mshukuru Mungu na si kubeza wengine.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Vyovyote utakavyoandika lkn haujajua nini maana ya maisha. Walikuwepo watu wenye hela na viburi kama ww lkn leo ninavyoandika hata chakula nyumbani ni shida.
Hongera. "aliyekupa ww kiti ndiyo aliyenipa mimi kuti''
Twende taratibu boss. Kwa nn unakwepa jukumu la kutafuta unakimbilia matatizo/kuishiwa?
 
Twende taratibu boss. Kwa nn unakwepa jukumu la kutafuta unakimbilia matatizo/kuishiwa?

Haujajua nini maana ya maisha. Mshukuru sana Mungu upo kwenye connection na haujatoka. Rudi kwenye uzi wa mtoa uzi usome upya ndiyo utaelewa ninachomaanisha.
Kutafuta siyo tatizo lipo hapa. Je, unachotafuta na kukipata sasa kinalingana na ulichokuwa unakipapata zamani? Km nyumbani ulikuwa unaacha 20,000 leo unaacha 5,000 je mkeo anachukuliaje?
Ndiyo maana nikasema km ww umefanikiwa mshukuru sana Mungu kuna watu walikuwa na hela lkn leo hii hawana hata connection. Haya maisha yaache km yalivyo
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Vlad umekaza sana aisee, well ni haki yako kupendwa na kuheshimiwa ila sasa mbaya zaidi kwa sisi vidume ukiwa huna pesa wala security ya pesa kama kazi your life will be a living hell aisee.

Yani kama una mke atakukosesha raha always na kukuua kwa stress maana comparison hazitakuacha salama. Utaonekana not a man enough! Yote mazuri uliomfanyia atayasahau na kugongewa itakuwa kama kazi.

Hiki ndio kipindi ambacho hata kurudi nyumbani kwako itakuwa mtihani mkubwa. Aisee wasio na kazi wanateseka kaka acha tu. Usiombe uanzishe uhusiano na mtu ukiwa huna hela. Kuna mda utafika utalia na kujuta.
Uanzishe uhusiano ukiwa huna hela?hutaweza kianzisha Mkuu
Sema ukianzisha ukiwa na kipato au kikakata sasa
 
si kweli,unataka kusema hawajielewi hawana akili? ukweli ni kwamba wao wana akili kama sisi na pengine kutuzidi ndo maana unaona wapo wanawake maprofesa,marais,huwajui vizuri wanawake acha kutetea usichokijua.
binadamu tumetofautiana mitazamo na jinsi tunavyoyachukulia mambo..!!wewe unaweza kupatwa na jambo jinsi utakavyolipokea ni tofauti na nitakavyolipokea mimi na jinsi ya kulitatua..!!nimechangia kutokana na experience yangu mimi mwenyewe hili jambo lishawahi nitokea hapo awali nikaenda hadi kwa mzee wangu (kwa sasa ni marehemu) ushauri alonipa ndo huo ambao umenusuru familia yangu hadi leo hii...
hata hivyo naheshimu mawazo yako boss..
 
Back
Top Bottom