Kwanini mwanaume anapiga goti anapomvisha pete ya uchumba binti?

Anayeenda kuomba uchumba ni mwanaume so kupiga goti ni kama ishara ya kuomba

Hata hivyo inategemea makubaliano yenu ni nani apige,unaweza kupiga ama akapiga yeye ama mkasimama wote
Hili nalo linahitaji makubaliano?
Nafikiri ni utashi tu.
Liko wazi hili,,
 
To propose.... kupiga magoti sio utaratibu wa kiafrika, na kupropose kwa kumvalisha pete ya uchumba sio utamaduni original wa kiafrika. Kwa makabila mengi utaratibu ilikuwa unawatuma wazee/washenga, then binti anaitwa na kuulizwa kama anakufahamu na anakukubali, akisema ndiyo basi inapangwa siku ya MAHARI, na mkishalipa mahari tu basi binti anakuwa officially mkeo. Ndo maana kwa makabila mengi, after send off upande wa mwanaume huomba familia ya mwanamke iwatunzie mke wao mpaka siku ya harusi ya kidini.

Kwa nini mwanaume kupiga magoti? Kwa mujibu wa utaratibu wa wenzetu, kupiga magoti kunamaanisha mambo mawili.

1. Kuonyesha kwamba wewe ni gentleman
2. Na ambalo ndo zito zaidi, unaonyesha kwamba kwa dakika hizo mbili tatu utakazokuwa umepiga magoti, mdada anakuwa na mamlaka kushinda wewe, maana jibu lake ndo litakalobeba mustakabali wa maisha yako.

Kwa sisi Wahehe ni mwiko kumpigia magoti mwanamke, so hata mimi sikupiga magoti.

Lakini, maadam tumeshaingiza sana Mungu kwenye tamaduni zetu, soma mazingira yako then act accordingly. Wanasema, WHEN IN ROME, DO AS THE ROMANS DO.
Mambo ya queen Elizabeth .Colonization
 
Upuuzi mkubwa sana,mimi alikuwa anajua mapema sitafanya hivyo maana alikuwa ananiona ninavyowakandia wanaopiga goti.

Nikamuambia sasa kesho utaamua usimame ,ukae,ulale,au upige magoti wewe maana mm nitakuwa nimesimama.
Akajiongeza akapiga yeye magoti
dah
 
Kwa Mungu ñdio goti linapigwa only


Nyie Ladies ñdo mpige wakati wa kuvishwa ukigoma nahairisha shughuli
 
Mwanamke Kama humuelewi unamwelekeza kabisa akachukue pete mwenyewe kwa sonara avae kabisa huko huko akija ni kuendelea na Mambo mengine ya msingi maswala ya kusuprise kisa Pete tuwachie Western people's
 
Back
Top Bottom