Kwanini Mwanamke wako atakuchukia usipomuongoza?

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
692
Kwenye uongozi kuna lawama.

Lawama za kwanini jahazi halisongi mbele/ limeenda mrama. Lawama zingine huwa hazina msingi. Mwanamke hutegemea mwanaume ndo abebe hizo lawama. Na ndio inakua rahisi kwake kujiachia kwako kwa kuwa umemkinga na lawama. Hiyo ni moja ya majukumu yetu wanaume kwa wanawake wetu, kumkinga na kumlinda.

Lakini pale unapoacha kumuongoza, anajiona yeye ndo anabeba lawama.

Wanawake hawajaumbwa kukabili lawama. Hivyo hajui kitu gani cha kufanya ili aongoze jahazi bila kujali lawama. Na atajiepusha na vitu vinavyosababisha lawama kwa nguvu zake zote.

Mfano, mnataka kutoka out. Usikae kusubiri maamuzi ya mwanamke muende wapi. Maana huko mnaweza kuta chakula kibaya, hakuna mazingira mazuri, usafiri ukaharibika njiani au mkanyeshewa na mvua. Hizo zote ni lawama ambazo unategemewa wewe mwanaume kuzibeba.

Ukimuachia lawama zote hizo mwanamke atakua hajiamini kwako tena. Mwisho wa siku ataanza kukuchukia. Hata kama mwanamke alikua anakupenda vipi ukiacha kumuongoza ataanza kukuona wa kawaida. Atakuacha. Kwanini ateseke na lawama kwako?

Uongozi ni kutambua vitu vya msingi. Uongozi ni kutambua nini kifanyike muda huu kwa manufaa ya baadae. Sio kutaka kumfurahisha mwanamke muda huu lakini baadae mambo yanaharibika.

Wanawake wanaongozwa sana na hisia. Hisia hazijali kitu gani cha msingi, zenyewe ni kwamba zikikupata saivi inabidi uzifanyie kazi ili ziondoke au zibakie. Ukifuata hivyo ni rahisi kupoteza mwelekeo.

Ukweli ni kuwa inabidi uyaongoze maisha yake. Haijalishi wengine wanasemaje. Haijalishi utandawazi unasemaje. Lakini hakikisha unamuongoza katika njia iliyo sahihi.

Ukimuongoza vibaya jamii ya kisasa itapata sababu kwanini usimuongoze mwanamke. Mfano, kwenye maamuzi madogo tu ya kumuongoza, labda mmekubaliana muende sehemu A, lakini mmefika kati kati ya safari anasema amekumbuka kitu fulani sehemu B (nyingine tofauti na mliyokubaliana). Anakusisitiza kwamba muanze kwenda sehemu B kuna umuhimu, japo huoni cha umuhimu huko sehemu B.

Ukimkubalia atakuonesha upendo kwa muda huo “nakupenda/ asante my umenielewa” lakini kesho yake atakuona huna uongozi kutambua vitu vya msingi, ataanza kukuchukia.

Ukimkatalia na kusisitiza muanze sehemu A, atakuponda/ kukununia kwa muda huo “yani we hata hunipendi, umenikatalia twende sehemu B”. Lakini kesho yake atakuona we ni mtu mwenye uongozi na haupelekeshwi na mawazo/ hisia zake hovyo, atakupenda zaidi. Fanya maamuzi mazuri kwa ajili yake. Kazi yake iwe ndogo tu, kujiachia na kufurahia kwako.

Uzuri ni kwamba kadri unavyozidi kuwa kiongozi wake mzuri, ndivyo naye anazidi kujiachia kwako. Ndivyo atazidi kukuamini, kukupenda na kukuheshimu. Mambo yanakua rahisi zaidi.

Kwa kuwa wanawake wengi wanatambua nafasi yao. Ipo kwenye damu tangu wanadamu tupo duniani, hivyo usiwe na wasiwasi juu ya utandawazi unavyowafanya wanawake. Wewe jitahidi tu uwe kiongozi bora wa maisha yako, na utaona urahisi kumuongoza mwanamke.

Share Na Wengine Wapate Kujifunza.
 
Najivunia sana kuwa muislam. Yote uliyo yaandika tushafundishwa tayar mtume S.W.S asema kila mmoja ni mchunga na kila mchunga ataulizwa juu ya alio wachunga. mwanamke ni mchunga juu ya mali za mumewe na mwanaume ni mchunga juu ya mkewe na family yake kiujumla
 
Mkuu umeandika jambo la msingi sana, Lakini nashindwa kuelewa kwann comment ni chache hv
 
Back
Top Bottom