CHUAKACHARA
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 12,388
- 6,482
we binti mbona unaniwakia kama gesi ya mtwara?! i do NOT support rape, naona ume-quote the wrong person. elekeza hizo hasira kwenye posti 11
apology accepted. sry for the gender mix-upHapana mbona nakuunga mmkono! For whatever reason you can not justify rape. By the way, I am a male father! Pole kama umekwazika
Mimi sivai nusuuchi!!!
Mimi sivai nusuuchi!!!
Nakumbuka mwaka 2004 huko nchini Afrika Kusini kulizuka mjadala mkali sana kuhusiana na nguo za nusu uchi, hasa kwa wasichana wa shule. Mjadala huo ambao ulihusisha maoni ya wananchi wakiwemo wale wanaohemkwa pindi waonapo tupu za wanawake, ulizuka baada ya walimu wakuu wa shule mbalimbali za huko kusema nguo fupi zinazovaliwa na baadhi ya wanafunzi wa kike hualika kubakwa.
Unajua ni kwa nini kauli hiyo ya waalimu wakuu wa sekondari nchini humo imezua mjadala? Ni kwa sababu Afrika Kusini inaongoza katika Afrika kwa kasi ya ubakwaji na hata mauaji ya wanawake kwa njia zenye kutia kinyaa.
Wakizungumza na gazeti la Saturday Star la nchi hiyo, waalimu hao, ambao kauli yao hiyo imevifanya vikundi vyenye kutetea haki za wanawake nchini humo kuja juu, walisema, wanaamini uvaaji nao unachangia katika kufanya wanawake wabakwe. Kauli kama hiyo, imekuwa ikipingwa sana na vikundi hivyo nchini humo.
Akizungumza kwa hasira Delphine Serumanga wa taasisi ya kupambana na ufujwaji wa wanawake Afrika Kusini, ya People Against Women Abuse (POWA), alisema, waalimu hao wasitake kuwafanya watu waamini kwamba, wanaume ni binadamu wanaoshindwa kuwa tofauti na mbuzi kwa kuendeshwa na mihemko tu ya miili yao. Amesema, kumbaka mwanamke hakuhusiani kabisa na uvaaji, bali ni zaidi ya hapo. ‘Hata wabakaji wa wanawake, ukiwauliza, watakwambia kwamba, wanabaka kama njia ya kutafuta au kuonesha nguvu, madaraka au uwezo dhidi ya mwanamke. Siyo suala la uvaaji .' Alisema Serumanga.
Lakini waalimu wengi wamesema kwamba, wanapopata kesi ya kubakwa msichana, mara nyingi kama siyo zote, msichana huyo ni lazima atakuwa ni mvaaji wa nguo za nusu-uchi. Wameongeza kusema kwamba, hawajawahi kupata kesi ambapo mbakwaji ni mvaaji wa nguo za heshima. Elizabeth Mnyuku, mkuu wa chuo cha Liberty Community katika mji wa Bramley, alisema, ‘sijawahi kukutana na kesi ya kubaka ambayo msichana alityebakwa ni mvaaji wa nguo za heshima, hapana.'
Aliendelea kusema, mwanafunzi akilalamika kwamba amebakwa au kafanyiwa jaribio la kubakwa, angalia tu namna alivyovaa. Siku zote utabaini kwamba, uvaaji wake ni wa kihasara. Anasema ni vigumu wakati mwingine hata kwa mwalimu wa kiume kufundisha kwa umakini anapokuwa mbele. Wanafunzi wa kike wenye viguo vifupi, huku wakiwa wamepanua mapaja, huwafanya waalimu hao kukosa amani kabisa.
Kuna wakati hata wanafunzi wenyewe wanakosa amani, ambapo inabidi wachukue mikoba ya madaftari na kufunika mapaja yao, wanapogundua kwamba, mwalimu anababaika baada ya kuona mapaja yao. Anasema, hali hiyo huwafanya wanafunzi hao kushindwa kuzingatia masomo kwa hofu ya kwamba watakaa uchi.
Kumekuwa na swali la, ni kwa nini mwanamke avae nguo fupi, halafu aogope tena kukaa uchi. jibu lake limekuwa gumu sana. Siyo kwa Afrika Kusini pekee, hata hapa kwetu huwa tunawaona wanawake wengi , ambao wamevaa nguo fupi sana, lakini wamekuwa wakijitahidi sana kujiziba au kujifunika wasije wakakaa uchi, iwe wakati wa kupanda gari, kuruka mahali au pengine popote ambapo atahitajika kupanua miguu. Utakuta mwanamke kavaa kimini na kitopu, lakini kila saa utamkuta anajitahidi kukishusha hicho kimini na kitopu wakati akitembea barabarani. Je ulivalishwa? Au unaweza kukuta msichana kavaa skin jinzi na blouse au T-Shirt, lakini muda wote mkono uko nyuma akijitahidi kushikilia hiyo blouse au T-Shirt yake isipande na kuonesha kiuno chake. Sasa shida yote hiyo ni ya nini?
CC: Thanda and Thando
BCC: lara 1, gfsonwin, Lisa, charminglady, Nyamayao, marejesho, Preta, Kaunga, BADILI TABIA, King'asti, Paloma, MadameX, Zion Daughter, amu, Angel Msoffe, cacico, Mrembo by Nature, MwanajamiiOne, Madame B, @nivea
Nguo fupi ila huoni kitu aiseee hao wadada ni wataalamu kweli!
yay 1st reply.
rape is NOT acceptable under ANY circumstances. nguo za wadada zinavutia lakini hazina uwezo wa ku-induce/justify rape. kama huwezi ku-handle then ma.l.a.y.a wamejaa kwa bei chee, watumie hao.Mi nakubaliana nakabsa kwamba nguo siyo justification ya kubaka but it can be reason ya mtu kubakwa.So important ni kuwaelimisha dada zetu jinsi ya kudress
watu wanabaka bata na mbuzi sijui nao wamefunikwa nusu uchi....
Anyway siwezi kujibu sana hoja yako...
Mie naamini nguo huvaliwa kutokana na sehemu na sehemu kuna vazi la disco kuna cazi la cokteili kuna la dinner nk....
Pia naamini kuna age na age...kuna age ya kuvaa kata k kuna ya kuvaa vibana ------ na kuna ya kuvaa kawaida....kuna mavazi ya binti chini ya miaka 20...kuna ya 21-30 kuna ya 30's na kuendelea kinachotakiwa ni kujitambua na kujielewa...na mavazi yanaangalia umbo pia......
All in all kwangu mie nguo ikiwa juu ya goti its ok....but itakapofika nusu paja mmmmh inategemea na tukio though nikiwa kwangu ni mwendo wa vibukta.......
Najua sijajibu hoja yako......ntarudi ...lakini naamini nguo sio kigezo cha kubaka