Kwanini mwanamke avae nusu-uchi halafu aogope kukaa uchi?

Kwanini mwanamke avae nusu-uchi halafu aogope kukaa uchi?

we binti mbona unaniwakia kama gesi ya mtwara?! i do NOT support rape, naona ume-quote the wrong person. elekeza hizo hasira kwenye posti 11

Hapana mbona nakuunga mmkono! For whatever reason you can not justify rape. By the way, I am a male father! Pole kama umekwazika
 
Hivyo vivazi vinasababisha mfadhaiko wa akili, na "Upofu"
 
Don't+tell+me+how+to+dress+tell+them+not+to+rape.jpg


tcc.JPG


Nakumbuka mwaka 2004 huko nchini Afrika Kusini kulizuka mjadala mkali sana kuhusiana na nguo za nusu uchi, hasa kwa wasichana wa shule. Mjadala huo ambao ulihusisha maoni ya wananchi wakiwemo wale wanaohemkwa pindi waonapo tupu za wanawake, ulizuka baada ya walimu wakuu wa shule mbalimbali za huko kusema nguo fupi zinazovaliwa na baadhi ya wanafunzi wa kike hualika kubakwa.

Unajua ni kwa nini kauli hiyo ya waalimu wakuu wa sekondari nchini humo imezua mjadala? Ni kwa sababu Afrika Kusini inaongoza katika Afrika kwa kasi ya ubakwaji na hata mauaji ya wanawake kwa njia zenye kutia kinyaa.

Wakizungumza na gazeti la Saturday Star la nchi hiyo, waalimu hao, ambao kauli yao hiyo imevifanya vikundi vyenye kutetea haki za wanawake nchini humo kuja juu, walisema, wanaamini uvaaji nao unachangia katika kufanya wanawake wabakwe. Kauli kama hiyo, imekuwa ikipingwa sana na vikundi hivyo nchini humo.

Akizungumza kwa hasira Delphine Serumanga wa taasisi ya kupambana na ufujwaji wa wanawake Afrika Kusini, ya People Against Women Abuse (POWA), alisema, waalimu hao wasitake kuwafanya watu waamini kwamba, wanaume ni binadamu wanaoshindwa kuwa tofauti na mbuzi kwa kuendeshwa na mihemko tu ya miili yao. Amesema, kumbaka mwanamke hakuhusiani kabisa na uvaaji, bali ni zaidi ya hapo. ‘Hata wabakaji wa wanawake, ukiwauliza, watakwambia kwamba, wanabaka kama njia ya kutafuta au kuonesha nguvu, madaraka au uwezo dhidi ya mwanamke. Siyo suala la uvaaji .' Alisema Serumanga.

Lakini waalimu wengi wamesema kwamba, wanapopata kesi ya kubakwa msichana, mara nyingi kama siyo zote, msichana huyo ni lazima atakuwa ni mvaaji wa nguo za nusu-uchi. Wameongeza kusema kwamba, hawajawahi kupata kesi ambapo mbakwaji ni mvaaji wa nguo za heshima. Elizabeth Mnyuku, mkuu wa chuo cha Liberty Community katika mji wa Bramley, alisema, ‘sijawahi kukutana na kesi ya kubaka ambayo msichana alityebakwa ni mvaaji wa nguo za heshima, hapana.'

Aliendelea kusema, mwanafunzi akilalamika kwamba amebakwa au kafanyiwa jaribio la kubakwa, angalia tu namna alivyovaa. Siku zote utabaini kwamba, uvaaji wake ni wa kihasara. Anasema ni vigumu wakati mwingine hata kwa mwalimu wa kiume kufundisha kwa umakini anapokuwa mbele. Wanafunzi wa kike wenye viguo vifupi, huku wakiwa wamepanua mapaja, huwafanya waalimu hao kukosa amani kabisa.

Kuna wakati hata wanafunzi wenyewe wanakosa amani, ambapo inabidi wachukue mikoba ya madaftari na kufunika mapaja yao, wanapogundua kwamba, mwalimu anababaika baada ya kuona mapaja yao. Anasema, hali hiyo huwafanya wanafunzi hao kushindwa kuzingatia masomo kwa hofu ya kwamba watakaa uchi.

Kumekuwa na swali la, ni kwa nini mwanamke avae nguo fupi, halafu aogope tena kukaa uchi. jibu lake limekuwa gumu sana. Siyo kwa Afrika Kusini pekee, hata hapa kwetu huwa tunawaona wanawake wengi , ambao wamevaa nguo fupi sana, lakini wamekuwa wakijitahidi sana kujiziba au kujifunika wasije wakakaa uchi, iwe wakati wa kupanda gari, kuruka mahali au pengine popote ambapo atahitajika kupanua miguu. Utakuta mwanamke kavaa kimini na kitopu, lakini kila saa utamkuta anajitahidi kukishusha hicho kimini na kitopu wakati akitembea barabarani. Je ulivalishwa? Au unaweza kukuta msichana kavaa skin jinzi na blouse au T-Shirt, lakini muda wote mkono uko nyuma akijitahidi kushikilia hiyo blouse au T-Shirt yake isipande na kuonesha kiuno chake. Sasa shida yote hiyo ni ya nini?

CC: Thanda and Thando

BCC: lara 1, gfsonwin, Lisa, charminglady, Nyamayao, marejesho, Preta, Kaunga, BADILI TABIA, King'asti, Paloma, MadameX, Zion Daughter, amu, Angel Msoffe, cacico, Mrembo by Nature, MwanajamiiOne, Madame B, @nivea

nakumbuka enzi hizo tupo Univer. mapicha kama haya tulikuwa tunaita kitafunio! Tumetoka mbali!
 
yay 1st reply.
rape is NOT acceptable under ANY circumstances. nguo za wadada zinavutia lakini hazina uwezo wa ku-induce/justify rape. kama huwezi ku-handle then ma.l.a.y.a wamejaa kwa bei chee, watumie hao.Mi nakubaliana nakabsa kwamba nguo siyo justification ya kubaka but it can be reason ya mtu kubakwa.So important ni kuwaelimisha dada zetu jinsi ya kudress
 
Naamini ni njia mojawapo ya kuanza kukaa uchi kwani hata ukiwauliza 7bu za kuvaa nguo fupi hawatakuwa na la kukujibu
 
ushasema wa bei chee kuna wasio na hicho kiasi chee, kuna walokaa jela wametoka aftr years nyege lita 30 no doo afu unakutana na pisi alone inakatiza kichochoroni imevaa umini utamu wote nje nje mavibration ya kutosha, acha kabisa blaza u know huwa tunasema sana ila hayajatukuta tu, hiyo situation mbaya sana akheri angekuwa kavaa fresh majaribu yanakuwa less otherwise man them teachers are so damn right
 
Wakati ni ukuta kwani hayao nayo yatapita, hamkumnuki mwaka 1971 taiti na min sketi si zilizua kizaazaa, kwanza sasa hivi kuna kaheshima kidogo angalau, wale tuliosoma MZ miaka ya 70 si mnakumbuka mtaa wa Lumumba, si tulikuwa tunakwenda kulipa Sh5/- tena ilikuwa biashara halali kabisa. kubaka ni tabia tu wala haisababishwi na nguo fupi.
 
watu wanabaka bata na mbuzi sijui nao wamefunikwa nusu uchi....

Anyway siwezi kujibu sana hoja yako...
Mie naamini nguo huvaliwa kutokana na sehemu na sehemu kuna vazi la disco kuna cazi la cokteili kuna la dinner nk....

Pia naamini kuna age na age...kuna age ya kuvaa kata k kuna ya kuvaa vibana ------ na kuna ya kuvaa kawaida....kuna mavazi ya binti chini ya miaka 20...kuna ya 21-30 kuna ya 30's na kuendelea kinachotakiwa ni kujitambua na kujielewa...na mavazi yanaangalia umbo pia......

All in all kwangu mie nguo ikiwa juu ya goti its ok....but itakapofika nusu paja mmmmh inategemea na tukio though nikiwa kwangu ni mwendo wa vibukta.......

Najua sijajibu hoja yako......ntarudi ...lakini naamini nguo sio kigezo cha kubaka

Kuongezea kidogo, enzi za mababu na mabibi, walikuwa wanavaa vimajani tu kuficha sehemu za mbele na hatari wala habari za ubakaji hatukuwahi kuzisikia sana. Pamoja na kwamba, nakwera na baadhi ya wadada wanaovaa nguo fupi kupita kiasi, ila pia siungi mkono wanaobaka kwa visingizio vya nguo fupi, hao ni watu waliopotoka mioyo na hawana sababu yeyote ya kujitetea.
 
Kubaka kaka mtambuzi, ni Tabia ya mtu tu na si kwa kuvaa nusu uchi , maana hata wanaobaka watoto wanakuwa wamevaa nusu uchi? la hasha.
Ila kwa wanawake kutojistiri kuna kudhalilisha wewe mwenyewe na familia yako kwa ujumla, tena wengine huwa wanajiuliza huyu kwao ana wazazi, maana unakutana na vituko, sema ndiyo hivyo nchi yetu imruhusu watu kwenda uchi.Kuna dada mmoja wakati huo Posta na Simu, alikuwa pale Postal house,sijui kwa sasa yuko wapi , alikuwa receptionist, alikuwa anavaa nusu Uchi pale kazini, ukifika kumuulizia mazazi wako anakudengulia ile mbaya na alikuwa anajiona Bab kubwa, sasa akaja akaolewa, lakini historia bado ipo kiasi akiisikia yeye mwenyewe watu wanavyomsema vibaya anakasirika sana. Kwa hiyo hao wanaovaa hivyo wanasahau kuna kesho na wao watakuwa na familia zao na watoto wao na watataka kubehave vizuri mbele za watu, ndipo hapo kazi inaanza.
 
Waswahili wanasema biashara matangazo lakini kama ndiyo hivyo mbona mpaka wake za watu bado tu wanavaa nusu uchi barabarani??

Kiukweli siungi mkono ubakaji lakini dada zetu mnatukwaza sana na uvaaji wenu!!
 
Back
Top Bottom