Kwanini mwanamke akibeba mimba anadeka sana?

manSniper

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
814
679
Nakumbuka miaka ile ya 93 mama alikua mjamzito ila alikua anapiga kazi balaa kule Marangu utamkuta kwenye majani, kufagia mbolea, kwenda sokoni nk,
yaani mpaka anajifungua yupo bize.

Sasa hichi kizazi cha leo wakibeba mimba mwanaume utakoma mara chips kuku, mara baga daah.Mimi mke wangu ni mjamzito sasa nilimfungulia duka sasa nipo zangu kikazi Mbeya kule imekua kero kila saa simu nikipiga simu kafunga duka, leo nimerudi yaani ni anadeka balaa hivi kwanini kizazi hichi wanadeka hivi?
 
nakumbuka miaka Ile ya 93 maza alikua mjamzito ila alikua anapiga kazi balaa kule marangu utamkuta kwenye majani, kufagia mbolea, kwenda sokoni nk yaani mpaka anajifungua yupo bize.. sasa hichi kizazi cha leo wakibeba mimba mwanaume utakoma mara chips kuku, mara baga daa.. mm wife ni mjamzito sasa nilimfungulia duka sasa nipo zangu kikazi mbeya kule imekua kero kila saa simu nikipiga cm kafunga duka leo nimerudi yaani ni anadeka balaa hivi kwa nn kizazi hichi wanadeka hivi?
Pole mkuu, vumilia ni shida za mda tu.
 
kudeka sio wote!
mimi mdogo wangu mtoto wa mjomba anafanya kazi hatari.. mimba miezi8
lakini sisi wenye asili ya kuwa watoto wa mwisho katika familia tunadekaga sana..

kama mwanaume huna moyo utajuta
ni vitabia tu vya mtu ikiwemo mimi...
pia wakati mwingine mimba zinachosha sana maana ni mzigo ule na unaleta mabadiliko mengi mwilini ..
pia jinsi mtoto utakavyo mlea ndivyo atakavyokua..
inaonekana ulihitaji mtt sana ,sasa anadeka anaona kashatimiza agano lake...
 
Wanawake wengi wa leo huona ujauzito kama ugonjwa. Akikutana na mtu wa kumdekeza ndio anadeka balaa na ndiyo maana wengi wanajifungua kwa kupasuliwa (operation). Ni vema wajawazito watambue kuwa kutobweteka na kufanya shughuli ndogondogo ni kwa faida yao wakati wa kujifungua.
 
Mkuu badilisha hiyo avatar?
Kudeka kwa mwanamke ni jambo la kawaida sana na wala sio dhambi sana sana hutokea kipind cha ujauzito km unaroho nyepes unadhan anajifanyisha kumbe kawaida sana.
Inategemea jins mnavyoish km ulikuwa unamdekeza atadeka lkn kam ulikuwa kauzu hawez kudeka sbb anaweza kuchezea kichapo. Mwanamke ni km mtoto vile ukimdekeza atadeka usipomddkeza hawez kufanya hivyo
 
1465827011886.jpg
 
Back
Top Bottom