Kwanini Mwami Zitto Zuberi Kabwe hashuki kisiasa?

Zitto ni jabari hasa,tungekua na kina zitto wengi , ingekua poa sana,wanasiasa wa upinzani both wa zamani na wanao emerge ingependeza mngenchagua zitto kuwa mentor wenu
 
Chadema BAVICHA kamwe hawatamkubali Zito Kabwe kwasababu siyo ndugu yao wa damu kikanda/kimkoa. Zitto aliona kabisa kwamba Freeman Mbowe hatoshi kuungoza upinzani kuing'oa ccm. Na hata mbowe mwenyewe analijua hilo na ndiyo maana yupo tayari kuwa kiongozi mkuu wa chama lakini hayuko tayari kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama chake. Sasa Zito alipoonyosha leadership ambition ya kukiongoza chadema, ndiyo bavicha kwasababu ya loyalty kwa mbowe, wakamfanya Zito ni adui, mamluki, ccm B, na upuuzi wote waliousema.

Ukweli utabaki kwamba, Zito is the most astute political operator in the land. Kuanzia ccm mpaka upinzani, hakuna kama Zito.
 
Zitto ni mamluki ndio maana nakwambia hakamatwi, kushirikiana ni mikakati tu lakini sio kwamba kwa kuwa yeye mammluki na wao wawe mamluki

Zitto kamwe hawezi kuwa Mamluki eti kwa sababu hakamatwi?!!, wanaogopa kumkamata kipindi hiki kwa sababu suala la T. lissu limewakalia pabaya, sasa hawawezi tena kuongeza "balaa" jingine litakalowatesa zaidi na litakalo amsha hisia za ndani na nje ya nchi.
 
Hahaha zitto hakamatwi tangu zamani hata kabla ya T.Lissu kuanza kuongea nje ya nchi. Zitto wao wanataka tumuamini lakini mimi simuamini hata wamjenge vipi.
 
Kipindi cha Jakaya hakukuwa na udikteta kama uliopo leo na baada ya kutokea mtafaruku kule Chadema ndipo watu wakasema Zitto ni CCM B, ndiyo hadi leo hiyo notion inaendelea.

Je umeona hio sheria mpya ya vyama vya siasa iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni, kuna kipengele juu ya uraia wa wazazi wa atakaye teuliwa kugombea Urais-- bila shaka hicho kipengele kimelenga kumdhibiti mtu mmoja, ni nani huyo??
 
Kuna bavicha mmoja alifikia mpaka kutembea na sumu kwa lengo la kumuua Zito, wakati Zito alipokuwa naibu katibu mkuu wa chadema. Siamini kama bavicha anaweza kufanya jaribio la kumuua naibu katibu mkuu bila ya maelekezo kutoka kwa mwenyekiti. Bavicha yule sijui siku hizi yuko wapi, maana kapotea muda tuu sasa.
 
Kipindi cha Jakaya hakukuwa na udikteta kama uliopo leo na baada ya kutokea mtafaruku kule Chadema ndipo watu wakasema Zitto ni CCM B, ndiyo hadi leo hiyo notion inaendelea.

Je umeona hio sheria mpya ya vyama vya siasa iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni, kuna kipengele juu ya uraia wa wazazi wa atakaye teuliwa kugombea Urais-- bila shaka hicho kipengele kimelenga kumdhibiti mtu mmoja, ni nani huyo??
Hahaha Zito ni mamluki, kuzaliwa kigoma hakumfanyi asigombee urais akitaka, hizo ni sharia za ccm sio katiba ya nchi. Hata wahindi wengi humu wazazi wao sio raia lakini ni watanzania wao unawaweka kundi gani ikiwa wangependa kugombea urais?
 
Kwa mujibu wa hiyo sheria mpya kamwe hao wahindi hawataweza kugombea Uraisi.
 
Sheria za ccm hizo wakikuhitaji wanasahau kila kitu. Unadhani Rostam akigombea hizo sharia zitafanya kazi?
 
Watapeleka hati ya dharula bungeni kubadilisha hicho kipengele cha sheria ili Mtu wao apite.😁😁
 
mkuu MAHORO in kiasi cha muda tu ndio utajua kupanda na kushuka kwa zitto
 
Back
Top Bottom