Hiyo haizekani kuwa hivyo. Mzee Nyerere ni mwalimu, Mzee Mwinyi ni mwalimu, Rais Magufuli ni mwalimu, Mh. Majaliwa ni mwalimu,.... kwavyovyote vile mwl sio shetani, una kitu unakitafuta utakipata.
Tunachosema sisi ni kwanini mwalimu wa leo anafananishwa na mwizi asiyepaswa kushika hela ya mchango wowote? bila shaka kuna ushahidi kuwa hela zinazochangwa na kupokelewa na mwalimu hazifanyi kazi iliyokusudiwa. Kwa nini maadili ya mwalimu yameporomoka kwa kiasi hiki? Zamani mwalimu ndiye aliyekuwa anaaminiwa kwenye jamii kuliko mtu yeyote, leo vipi mwalimu jamii haimuamini tena.
Kwanini mwalimu wa leo anatoza wanafunzi na wazazi michango mingi?
a) ni mwizi anataka kuiba michango ya wazazi na kuitumia kinyume na madhumini ya michango?
b) anataka watoto wapate elimu bora?
c) Ana huruma zaidi kwa watoto kuliko serikali yenyewe?
d) Anaifichia aibu serikali?
e) Kipato kidogo anataka kujalizia kilichopungua?
Tatizo ni moja tuu mkuu,
Siku moja funga chumba chako hafu weka funguo mfuko halafu usahau uone utakavohangaika.
Matatizo mengi mno sasa hivi yanageuzwa changamoto hapo ndipo shinda inpoanzia.
Na utatuzi wa changamoto hizo unahitaji mikakati ya kitaalamu unafanywa na wanasiasa hapo ndipo tatizo linapoanzia.
Mfano: watoto wanamwomba mwalimu wawe wanakula shule mida ile ya kutawanyika kwani wengine wakifika nyumbani hawawezi kusoma tena hasa vidato vy mituhani
Mwalimu kwa busara yake anaitisha kikao cha wazazi kuyasikia maoni ya watoto wao, kweli kikao kinaendeshwa na kukubalina kwamba kila mmoja atachangia kwa ajiri ya mwanae
Kimbembe kinakuja pale mmoj au wengine wanapopata changamoto ya kuikosa michango
Hapo hukimbia kwa diwani ili wote wakose badala ya kukubaliana n wazazi wenzake
Kiukweli sasa hivi wazazi ndio wanaotamani kuwaona walimu wakifukuzwa na pengine kufungwa.
Hiki ni kizazi cha tukose wote,
Mwanangu akikosa mchango wa makubaliano wote wakose badal ya kutumia busara.
Embu fuatilieni michango wanayolalamikia utakuta ni ile waliyokubaliana kuchangia na wakti mwingine anaechangisha hata sio mwalimu ni mtoto mwenyewe.
Hay nimeyaona kwenye shule ambayo mimi ni nimo kwenye kamati ya bodi ya shule hiyo