Kwanini Mungu hakurekebisha kilichosababisha shetani akaasi kabla ya kumuumba binadamu?

Kwa nn nia ya kujiona shetani kuwa yeye ni bora kuliko binadam ilikuwemo ndani yake ilihali mungu alikuwa na uwezo wa kuiondoa kabla ya ubishi kutokea?
Yani mkuu inashangaza sana kuona mtu mzima anawezaje kuamini stori kama hizi...
 
Huo si ubaguzi sababu hakuna kuingiliana katika maumbile hayo,kama vile walivyoumbwa kuku na viumbe wengine,waumbwa na kuwekewewa mfuno wa maisha kivyake.

Ule ni ujinga wake mwenyewe kujiona bora kuliko Adamu,mbona malaika wameumbwa kwa nuru lakini hawajajiona bora kuliko wengine ?

Kwahiyo utakuta ni kiburi,ujinga na matamanio ya nafsi ya Shetani.

Wewe huoni leo hii sisi kwa sisi binadamu tunajiona bora wengine kuliko wengine na tabia mbaya nyingine ?
Lakini mwanadamu si kaumbwa katika umbile bora kuliko viumbe wengine au?
 
Habari ya jumapili.

Dini inasema shetani aliasi huko juu mbunguni mahala palipotukuka na palipoinuka juu anapoishi mungu. Baada ya shetani kuasi mungu akamtimua na kumshusha huku Duniani.

Dini inasema baadae mungu akamuumba mwanadamu na kumuweka Duniani, maana yake mwanadamu alipowekwa duniani tayari shetani alikua duniani muda mrefu tu anakula zake maisha.

Hadithi ya shetani kuasi iko one sided, yaani inaelezwa kutoka upande wa mungu, hakuna aliewahi kusikia upande wa shetani(tayari binadam wanamshutumu shetani kwa habari ya kuambiwa, one sided story, hivyo shetani anahukumiwa kua ni mbaya bila kusikilizwa).

Dini haisemi kwa nini shetani aliasi na ilikuaje akaasi. Dini inasema mungu anajua kila kitu, all knowing lakini haisemi mungu alishindwaje kujua kua shetani atakuja kuasi ili asimuumbe. Na kama alijua shetani atakuja kuasi kwa nini alimuacha aasi. Mbaya zaidi huo mgogoro wao umetuingiza na sisi binadam ambao hatujui chanzo cha mgogoro. Yaani mungu anarecruit binadam washirikiane nae mwenye mgogoro wake na shetani huku binadam hawajui chanzo cha mgogoro wao. Na mungu anatishia kua yoyote ambae hatashirikiana nae kwenye mgogoro huo atampanish vikali. Unajiuliza hakuaje involved kwenye mgogoro nisioujua chanzo chake na natishiwa adhabu kali kama sitashiriki huo mgogoro ambao in fact haupo kwa sababu mungu hajaonyesha kuwepo, hivyo watu waoga na wajinga wanalazimika kushiriki mgogoro blindly ili kuogopa adhabu.

Kama mungu anawapenda wanadamu kama dini inavyosema alipaswa kurekebisha kasoro zilizojitokeza kabla ya kumuumba mwanadam, lakini pia alipaswa kujua in the first hand kua shetani atakuja kuasi kabla hajamuumba, vinginevyo hajui kila kitu kinyume na inavyosemekana kua anajua kila kitu.

Tukubali tukatae, maovu yote duniani kama mauaji, wivu, kifo, husda, wizi, matetemeko ya ardhi, tsunami, vimbunga, ukame, magonjwa yote chanzo chake ni mungu. Mungu ameshindwa kabisa kutuonyesha kua kweli anatupenda kama anavyosemwa, ameshindwa kuonyesha kweli kua anajali Mbaya zaidi ameyatengeneza alafu ameshindwa kuyaondoa.

Hii mada inaendelea.

Ntongeza ya mjumbe.
Tumezaliwa tukaukuta ugomvi kati ya Mungu na shetani. Ila kwa asilimia 98 Mungu ndio anaonekana kushinda dhidi ya miungu wengine pamoja na shetani. Mungu alianza na Adam akaja kwa Ibrahim akashukia kwa Isaka akaenda kwa Yakobo (Israel). Katika Israel zikaja zile kabila 12 na ndani yake akaja Sauli, Daudi kisha Suleiman na wengine. Kote huko Mungu anapata upinzani toka kwa watu anaowapenda na aliowachangua. Sio kwamba hana uwezo wa kuwamaliza, but what for?

Sasa toka uzao wa Daudi akatumwa Yesu. Bado kuna binadamu hawakumwelewa na wakamfanyia mbaya kwa kumuua. Lakini kabla hawajamuua akaongea na Baba yake kwa kusema (soma Yohana 17 yote) mengi dhidi ya uovu na ulimwengu. Naye alipofufuka alihakikisha anatuachia Roho mtakatifu ili kwa njia yako Baba pia apate kutukuzwa. Naye Roho Mt. akatupa matunda ya kuishi nayo. Kama huna hata moja yakupasa uwe umeshakufa. Kadhalika huwezi kuwa na yote. Nayo ni haya: soma Wagalatia 5: 22-23.

Sasa kwa muhtasari huo nakushauri usilalamike sana maana Mungu hajakubana kiasi hicho. Amekupa uhuru wa kuchagua kati ya jema na baya. Kati ya uzima na mauti. Anasema yeye hunyeshea mvua yake wema na wabaya. Hivyo basi kwa kuwa unataka kusikia upande wa pili, haujazuiwa. Mtafute shetani. Wala si wa kutafuta maana yupo tu, na utampata pale Roho wa Mungu asipokiwapo ndani yako. Ruhusu mwili kuishinda roho tu na utakutana na matendo ya mwili na rafiki wa ibilisi katika Wagalatia tena 5: 18-20.

Uzuri Mungu ni mwema. Atakuruhusu kurudi tena kwake kwa kuambatana na matendo ya Roho. Ila angalia usichelewe. Pia ni bora zaidi kuamini haya kuliko kuwa Tomaso.
 
Habari ya jumapili.

Dini inasema shetani aliasi huko juu mbunguni mahala palipotukuka na palipoinuka juu anapoishi mungu. Baada ya shetani kuasi mungu akamtimua na kumshusha huku Duniani.

Dini inasema baadae mungu akamuumba mwanadamu na kumuweka Duniani, maana yake mwanadamu alipowekwa duniani tayari shetani alikua duniani muda mrefu tu anakula zake maisha.

Hadithi ya shetani kuasi iko one sided, yaani inaelezwa kutoka upande wa mungu, hakuna aliewahi kusikia upande wa shetani(tayari binadam wanamshutumu shetani kwa habari ya kuambiwa, one sided story, hivyo shetani anahukumiwa kua ni mbaya bila kusikilizwa).

Dini haisemi kwa nini shetani aliasi na ilikuaje akaasi. Dini inasema mungu anajua kila kitu, all knowing lakini haisemi mungu alishindwaje kujua kua shetani atakuja kuasi ili asimuumbe. Na kama alijua shetani atakuja kuasi kwa nini alimuacha aasi. Mbaya zaidi huo mgogoro wao umetuingiza na sisi binadam ambao hatujui chanzo cha mgogoro. Yaani mungu anarecruit binadam washirikiane nae mwenye mgogoro wake na shetani huku binadam hawajui chanzo cha mgogoro wao. Na mungu anatishia kua yoyote ambae hatashirikiana nae kwenye mgogoro huo atampanish vikali. Unajiuliza hakuaje involved kwenye mgogoro nisioujua chanzo chake na natishiwa adhabu kali kama sitashiriki huo mgogoro ambao in fact haupo kwa sababu mungu hajaonyesha kuwepo, hivyo watu waoga na wajinga wanalazimika kushiriki mgogoro blindly ili kuogopa adhabu.

Kama mungu anawapenda wanadamu kama dini inavyosema alipaswa kurekebisha kasoro zilizojitokeza kabla ya kumuumba mwanadam, lakini pia alipaswa kujua in the first hand kua shetani atakuja kuasi kabla hajamuumba, vinginevyo hajui kila kitu kinyume na inavyosemekana kua anajua kila kitu.

Tukubali tukatae, maovu yote duniani kama mauaji, wivu, kifo, husda, wizi, matetemeko ya ardhi, tsunami, vimbunga, ukame, magonjwa yote chanzo chake ni mungu. Mungu ameshindwa kabisa kutuonyesha kua kweli anatupenda kama anavyosemwa, ameshindwa kuonyesha kweli kua anajali Mbaya zaidi ameyatengeneza alafu ameshindwa kuyaondoa.

Hii mada inaendelea.

Ntongeza ya mjumbe.
mkuu Hakimu Mfawidhi nadhani wewe ni hakimu kama jina lako linavyoonesha

Tuseme leo wewe kama hakimu unatuhumiwa na watu kadha wa kadha kwamba wewe huwa hutendi haki katika maamuzi unayoyafanya,na tena kuna kesi inaendelea ambayo wanaokutuhumu wameshafikia mkataa kuwa hakimu huyu huwa hatendi haki na kama hamuamini subirini hii kesi iishe muone atakavyoamua,na tayari maneno hayo mabaya kukuhusu yanasambazwa kwa watu wengi kadri iwezekanavyo,wewe kama hakimu utachukua hatua gani?

ni kipi kinachotupa ukweli kumhususu Mungu na shetani? una uhakika gani kuwa hakuna majibu kuhusu hila ambayo shetani alifanya mpaka akawa mbaya?ni dini ipi inayosema hayo uliyoyasema wewe hapo juu?

methali isemayo mchuma janga hula na wa kwao unailewaje mkuu? umewahi kujipata katika hali ambayo unaingia kwenye kosa hata kama si wewe uliyekosa?shuleni?kazini?popote pale?

Ni Mungu yupi unayemwongelea wewe?

ukisema Mungu huyu aliyetuumba sisi,hatupendi wanadamu,pumzi inayokuwezesha wewe kuandika hii mada yako leo umeinunulia wapi?kiasi gani?unakula chakula cha nani? ubongo wa kufikiria maswali yote hayo uliyonayo,nani kakupa?

ukisema chanzo cha maovu yote leo duniani ni Mungu,tuseme basi watu leo wanapigana na Mungu?Mfano tuseme serikali inapigana na Mungu kupunguza uhalifu kwa kuweka polisi ,mahakama na taasisis zozote za kupambana na uhalifu? hospitali je,vilimo vya umwagiliaji?tuseme vyote hivyo ni katika kupambana na Mungu,na maovu aliyoyaleta?

Na bado havijaisha tuseme Mungu katuzidi nguvu katika mapambano yetu na anaendelea kutushambulia vilivyo na maovu yake?Na ikiwa tumeshindwa mapambano dhidi ya Mungu,nini mwisho wa haya yanayoendelea sasa?ni nani atakayetuokoa kutoka kwenye mkono wa Mungu huyo mwovu unayemsema wewe?

Ni kupitia nini Mungu anafundisha watu uovu kama wizi n.k?
 
Angalia : 1 : Mungu ni Mkuu na ni mweza wa yote, 2 : Mungu ni mwema mwenye huruma : semi hizi mbili zinakinzana, " Kama ni Mkuu sio mwema, na kama ni mwema sio Mkuu. A lot of contradictions, even in the Bible
 
Nimeuliza maswali ya contradictions kumhusu huyu Mungu kwa miaka kadhaa hapa.

Sijapewa jibu la kueleweka.
 
Angalia : 1 : Mungu ni Mkuu na ni mweza wa yote, 2 : Mungu ni mwema mwenye huruma : semi hizi mbili zinakinzana, " Kama ni Mkuu sio mwema, na kama ni mwema sio Mkuu. A lot of contradictions, even in the Bible
Mkuu, awezaye kuwa mkuu aweza pia kuwa mwema,na mara nyingi, wenye ukuu na uwezo huwa na wema zaidi kuliko dhaifu,japo si wote.Nachukulia kwa mfano wa binadamu tu,walio kinyume na ukuu (samahani,nakosa kiswahili kizuri hapa) mara nyingi zaidi ndio wachache sana wa tabia za wema.Mfano,hawa ndio hata wagumu kusamehe.

Sioni Mungu awezaje kuwa Mungu bila kuwa mweza yote.Na pia sioni Mungu atakuwaje Mungu kama sio mwema...kimsingi awe na upendo!
 
Lakini mwanadamu si kaumbwa katika umbile bora kuliko viumbe wengine au?

Nadhani hapa ipo wazi.Hata kama shetani angeumbwa kwa almasi,huyo aliyemuumba,yaani Mungu, ndiye anajua ubora upi ndio wa juu zaidi kati yake na binadamu.Anapotoa maelekezo halafu akatoa upinzani,ni kosa la wazi kabisa.

Lakini, tuseme hata kama kweli shetani alijiona bora zaidi, lakini aliyewaumba anapotoa maelekezo na akayapinga, hapo ndio shida.Infact, hata kama angeambiwa asujudie bwawa la tope, vema angetii tu.Ni suala la utii tu.

Noti ya pesa haipati thamani kwa tarakimu zake zilizopo,imepewa thamani na waliotaka iwe na thamani hiyo ndio sababu siku za ubadilishwaji noti ili zije mpya,huishia kuchomwa tu moto kama takataka.Vile vile shetani thamani yake aliipata kutoka kwa aliyempa hiyo thamani na ndio sababu aliponyang'anywa hiyo thamani yake, akabaki kuwa shetani tu, kiumbe duni zaidi asiyepaswa kufuatwa hata kidogo na ambaye hatima yake imeshakuwa 'sealed'-motoni!
 
Habari ya jumapili.

Dini inasema shetani aliasi huko juu mbunguni mahala palipotukuka na palipoinuka juu anapoishi mungu. Baada ya shetani kuasi mungu akamtimua na kumshusha huku Duniani.

Dini inasema baadae mungu akamuumba mwanadamu na kumuweka Duniani, maana yake mwanadamu alipowekwa duniani tayari shetani alikua duniani muda mrefu tu anakula zake maisha.

Hadithi ya shetani kuasi iko one sided, yaani inaelezwa kutoka upande wa mungu, hakuna aliewahi kusikia upande wa shetani(tayari binadam wanamshutumu shetani kwa habari ya kuambiwa, one sided story, hivyo shetani anahukumiwa kua ni mbaya bila kusikilizwa).

Dini haisemi kwa nini shetani aliasi na ilikuaje akaasi. Dini inasema mungu anajua kila kitu, all knowing lakini haisemi mungu alishindwaje kujua kua shetani atakuja kuasi ili asimuumbe. Na kama alijua shetani atakuja kuasi kwa nini alimuacha aasi. Mbaya zaidi huo mgogoro wao umetuingiza na sisi binadam ambao hatujui chanzo cha mgogoro. Yaani mungu anarecruit binadam washirikiane nae mwenye mgogoro wake na shetani huku binadam hawajui chanzo cha mgogoro wao. Na mungu anatishia kua yoyote ambae hatashirikiana nae kwenye mgogoro huo atampanish vikali. Unajiuliza hakuaje involved kwenye mgogoro nisioujua chanzo chake na natishiwa adhabu kali kama sitashiriki huo mgogoro ambao in fact haupo kwa sababu mungu hajaonyesha kuwepo, hivyo watu waoga na wajinga wanalazimika kushiriki mgogoro blindly ili kuogopa adhabu.

Kama mungu anawapenda wanadamu kama dini inavyosema alipaswa kurekebisha kasoro zilizojitokeza kabla ya kumuumba mwanadam, lakini pia alipaswa kujua in the first hand kua shetani atakuja kuasi kabla hajamuumba, vinginevyo hajui kila kitu kinyume na inavyosemekana kua anajua kila kitu.

Tukubali tukatae, maovu yote duniani kama mauaji, wivu, kifo, husda, wizi, matetemeko ya ardhi, tsunami, vimbunga, ukame, magonjwa yote chanzo chake ni mungu. Mungu ameshindwa kabisa kutuonyesha kua kweli anatupenda kama anavyosemwa, ameshindwa kuonyesha kweli kua anajali Mbaya zaidi ameyatengeneza alafu ameshindwa kuyaondoa.

Hii mada inaendelea.

Ntongeza ya mjumbe.

Kama wewe mwenyewe unayeleta mada unayosema ni 'one-sided' unadhani utakubaliana na mchango wowote? Kwangu mimi mjadala huu umefeli kuanzia unapoanza kujenga hoja isiyojengeka (self-defeating argument).
 
Dah haya mambo ni Magumu

Weka huo mchango tuuone, sasa kama wewe mwenyewe huna uhakika kama nitakubaliana na nchango wako au la maana yake ni kua huna hoja ya maana.

Ahsante kwa kutambua kua I do not take bogus arguments.
 
Mkuu maswali kama hayo ukijiuliza na tuseme kwa akili ndogo tu ya ufahamu kama binaadam anaetumia akili yake vizuri,dini kama dini haina majibu yanayo ridhisha sema tutaenda kwenye majengo kwa kusema tunaenda kuabudu lkn hasa tunaenda kuchangamana na jamii tu na yanayoletwa nayo kama kufiwa,kuzikwa,ndoa na mambo kama hayo

Kwa ufupi ni suala la kujumuika kijamii tu huko misikitini na kanisani zaidi kuliko hata kumjua huyo Mungu na hatima yetu tukifa
 
Aliacha iwe hivo na alimuongezea nguvu shetani nguvu ili siku ya mwisho amuonyeshe Shetani kuwa Yeye/Mungu ndiye mfalme na mkuu wa kila kitu.
 
Mkuu maswali kama hayo ukijiuliza na tuseme kwa akili ndogo tu ya ufahamu kama binaadam anaetumia akili yake vizuri,dini kama dini haina majibu yanayo ridhisha sema tutaenda kwenye majengo kwa kusema tunaenda kuabudu lkn hasa tunaenda kuchangamana na jamii tu na yanayoletwa nayo kama kufiwa,kuzikwa,ndoa na mambo kama hayo

Kwa ufupi ni suala la kujumuika kijamii tu huko misikitini na kanisani zaidi kuliko hata kumjua huyo Mungu na hatima yetu tukifa
Kwa kiasi kikubwa unasema ukweli.Na hivi asilimia fulani ya kutosha ya hao wasimamia dini madhabahuni wapo zaidi kuganga njaa zao kupitia sadaka n.k. Hata kuelimisha vema kumhusu Mungu haipewi uzito zaidi ya utisho wa moto wa jehanamu,umuhimu mkubwa wa kutoa sadaka na mambo kama hayo ambayo yanaacha pengo kubwa kumhusu huyo anayeabudiwa.
 
Yaani nadhani kuna muda Mungu mwenyewe anasoma comment jinsi watu wanavyomtetea hadi anatikisa kichwa aisee.
 
Back
Top Bottom