Kwanini Mungu hakurekebisha kilichosababisha shetani akaasi kabla ya kumuumba binadamu?

Ikiwa kila matatizo yanayotukumba sisi binadamu chanzo chake ni shetani

Sasa je shetani akiwa nae anapata matatizo je yatakua yanasababishwa na nini au kuna shetani mwingine?

Sent using unknown device
Labda yeye atakuwa anatupa lawama zake kwa mwenyezi Mungu aliyemuumba na kumwekea "uwezo wa kuasi" ndani ya roho au akili zake. Sasa hapo tusemeje wajameni?
 
Kwanza sio kweli ya kuwa Shetani ndio chanzo cha kila baya.

Pili,baada ya Shetani kukaidi ile amri,alimuomba Mola wake asimfishe mpaka itakapo karibi kiama,na aka ahidi kuwapoteza wanadamu na Mola akasema ya kuwa atawapoteza wale ambao watamtii yeye Shetani lakini wale waja wa Allah wenye kumtii,katu Shetani hatawapoteza.

Na miongoni mwa viumbe wa mwisho kufa ni Shetani laana ya Allah iwe juu yake.

Nipo .....

Kama shetani sio chanzo cha kila baya je nini chanzo cha kila baya?

Kwanini mungu hakufanya hivyo kwa binadamu kua wote tuwe viumbe wa mwisho kufa pamoja na shetani?

Sent using unknown device
 
Kwanini unishauri nitafute maarifa ya mungu ambayo tayali yamejikita kuelezea chuki dhidi ya shetani je kuna kitu gani kipya nitakachojifunza hapo ambapo?

Mimi nilifikiri utanipa ushauri wa kusoma vitabu vyenye maelezo ambayo yametolewa na shetani ili niweze kupima mizani ya haki kubaini nani anastahili kulaumiwa kati ya mungu na shetani, lakini wewe unanisisitizia kusoma tena habari za mungu ambazo zimetoa maelezo yenye kumuonesha shetani ni mbaya

Sent using unknown device
Nipe reference kutoka kwenye kitabu chechote, sehem inayoonyesha Mungu anamchukia shetani..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda yeye atakuwa anatupa lawama zake kwa mwenyezi Mungu aliyemuumba na kumwekea "uwezo wa kuasi" ndani ya roho au akili zake. Sasa hapo tusemeje wajameni?
Ikiwa kila baya linawezekana kufanyika pasipo kusababishwa na shetani je tutakua na uhakika gani wa furaha ya milele iliyoko peponi wakati tunaweza kutenda dhambi tukiwa huko huko peponi pasipo kushinikizwa na shetani?

Kama shetani sio msababishi wa dhambi basi hata kuangamizwa kwa shetani sio suluhisho la kutokomeza dhambi

Sent using unknown device
 
Hivi ni kwa nini baada ya Eva kutenda kosa hakuhisi tofauti yoyote na pia hakupata adhabu hapo hapo hadi pale Adam na yeye alipokula lile tunda alilopewa na Eva ndipo wote kwa pamoja wakaona hali tofauti na kisha kupewa adhabu ya pamoja?
Nyaka...

Swali fikirishi....

Na kweli angekwidwa hawa peke yake lakini ni kama alisubiriwa na adam ...aje waliviruge kabisa ili walaanike wote maana angetoka hawa tu sijui ingekuwaje...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja nzuri inayohitaji falsafa ya hali ya juu . Hivi nimelogwa mpaka nikaamini eti shetani alitupwa duniani kutoka mbinguni?

Ni uwongo ambao hauhitaji kufikiria , walioleta hizo dini wametuweza ! Eti akamtuma mwanae kutukomboa , hivyo alimtoa msukule mwanae ili apambane na shetani , bianadamu huenda hana kosa kumtoa mtu kafara ili afanikiwe kwa kuwa Mungu alishaanza huo mchezo ! Nafuu nisome katiba yangu ya nchi kuliko uwongo wa biblia .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kutupa ushahidi wa haya maneno ?

Je unajua ilikuwaje Ibilisi akatolewa katika rehma za Mola muumba ?

Nakukumbusha tu,kilichomfanya Ibilisi(Shetani) kufukuzwa ni yeye kukataa kumsujudia (Kumpa heshima) Adamu. Hii ina maana ya kuwa Adamu amemumbwa kipindi Shetani bado yupo mbinguni. Rejea Qur'aan sura ya pili (al Baqara) inaelezea kisa hicho.

Nipo ....
kwa aliyeyagulia kushuka duniani ni nani?

shetani au binadamu?
swali ni hilo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutenda dhambi ama kutotenda huwa maamuzi ya binadamu mwenyewe hivyo hata kwenda peponi ama motoni inategemea namna ulivyotumia uhuru wako kufanya maamuzi wakati ukiishi hapa duniani, Shetani huwa hamlazimishi mtu kutenda mabaya bali anakushawishi tu, maamuzi ya kutenda ama kutotenda ni juu yako.. Mungu ametoa uhuru wa maamuzi kwa binadamu... hata shetani alitumia uhuru huo kuasi na ndio maana yupo mpaka leo.. Mungu si dikteta..

Sent using Jamii Forums mobile app
Naogopa kumwita Mungu dikteta ila kwenye biblia kitabu cha Kutoka 20:5 hadi 20:6 pameandikwa "....Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu".

Labda tuseme Mungu wetu ni mzazi asiyependa mchezo mchezo.
 
Hoja nzuri inayohitaji falsafa ya hali ya juu . Hivi nimelogwa mpaka nikaamini eti shetani alitupwa duniani kutoka mbinguni ?? Ni uwongo ambao hauhitaji kufikiria , walioleta hizo dini wametuweza ! Eti akamtuma mwanae kutukomboa , hivyo alimtoa msukule mwanae ili apambane na shetani , bianadamu huenda hana kosa kumtoa mtu kafara ili afanikiwe kwa kuwa Mungu alishaanza huo mchezo ! Nafuu nisome katiba yangu ya nchi kuliko uwongo wa biblia .

Sent using Jamii Forums mobile app
Eti yesu alikufa kwa ajili yetu

How is it possible for a white man' to die for black man??



Sent using unknown device
 
Back
Top Bottom