Kwanini Mungu hakurekebisha kilichosababisha shetani akaasi kabla ya kumuumba binadamu?

Haya mambo ni hatareee sana mwanzo life coded nilikua nambishia sana kuhusu haya mambo ya kiiman za kimungu.

kunasiku nilimuuliza mchungaj juu ya ile kauli ya "MIMI MUNGU MWENYE WIVU" jibu alilonipa sita kaaa niende kanisan tena.
 
Lakini Adamu alipowekwa kwenye ile bustani alitahadharishwa juu ya ule mti. Kuhusu kuwarubuni binadamu ni kwa wale walio acha dini na kufata matamanio ya nafsi zao,na hili Allah alimwambia Shetani ya kuwa ataweza kuwarubuni wale wafatao matamanio ya nafsi zao na kuacha maamrisho ya Mola wao.

Nipo ....
Kwa hiyo umekubali kwamba shetani ana uwezo mkubwa kuliko mwanadamu?
 
Shetani wapo wa Aina 2, shetani wa kijini na shetani wa kibinaadam, hawa wote ni maagent wa iblisi, mtoa post na waunga mkono post jiulizeni je, mpo ktk kundi gani kati ya hayo mawili? By the way , Islam has an answer of all the posed questions.
Give us the answer from islam please.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini Adamu alipowekwa kwenye ile bustani alitahadharishwa juu ya ule mti. Kuhusu kuwarubuni binadamu ni kwa wale walio acha dini na kufata matamanio ya nafsi zao,na hili Allah alimwambia Shetani ya kuwa ataweza kuwarubuni wale wafatao matamanio ya nafsi zao na kuacha maamrisho ya Mola wao.

Nipo ....
Lakini tunaambiwa kila mtu ana malaika wake mlinzi! Sasa kazi ya huyo malaika ni nini kama anashindwa kutuwekea ulinzi mpaka shetani anaturubuni!! Je na yeye ataenda motoni kwa kuniacha nirubuniwe na shetani!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo umekubali kwamba shetani ana uwezo mkubwa kuliko mwanadamu?

Sijakubali,bali ni kwa wale walio muasi Mola ndio anaweza kuwarubuni ila wale wenye kumtii Mola hawezi kuwarubuni. Hapa unatakiwa uelewe maneno.
 
haya mambo ni hatareee sana mwanzo life coded nilikua nambishia sana kuhusu haya mambo ya kiiman za kimungu

kunasiku nilimuuliza mchungaj juu ya ile kauli ya "MIMI MUNGU MWENYE WIVU" jibu alilonipa sita kaaa niende kanisan tena
Saizi usharudi kwenye mstari?

Nakumbuka tulishawahi kubishana sana juu ya haya mambo sikumbuki ni uzi gani

Sent using unknown device
 
Baada ya kurubuniwa na Shetani (kama ni kweli) binadamu tumekuwa tukipata mateso sana katika dunia hii mfano kupata magonjwa, njaa, vifo n.k. wakati tukiendelea kusubiri hiyo siku ya kiama (kama ipo) ambapo kwa waliotenda maovu napo watapata adhabu nyingine kubwa zaidi. Swali langu ni je kwa upande wa Shetani yeye amekuwa akipata shida au mateso gani hapa kati kati wakati na yeye akisubiri hiyo siku ya kuangamizwa yeye na wafuasi wake?
Ikiwa kila matatizo yanayotukumba sisi binadamu chanzo chake ni shetani

Sasa je shetani akiwa nae anapata matatizo je yatakua yanasababishwa na nini au kuna shetani mwingine?

Sent using unknown device
 
Lakini tunaambiwa kila mtu ana malaika wake mlinzi! Sasa kazi ya huyo malaika ni nini kama anashindwa kutuwekea ulinzi mpaka shetani anaturubuni!! Je na yeye ataenda motoni kwa kuniacha nirubuniwe na shetani!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nafsi ya mwisho inayoamua either kurubuniwa au kutorubuniwa ni wewe mwenyewe.

Mungu ameweka power ya free will ndani yako. So ni wewe ndiye unayeamua kurubuniwa au kukataa kurubuniwa.

Maana unao uwezo wa kukataa kurubuniwa.
 
Kutenda dhambi ama kutotenda huwa maamuzi ya binadamu mwenyewe hivyo hata kwenda peponi ama motoni inategemea namna ulivyotumia uhuru wako kufanya maamuzi wakati ukiishi hapa duniani, Shetani huwa hamlazimishi mtu kutenda mabaya bali anakushawishi tu, maamuzi ya kutenda ama kutotenda ni juu yako.

Mungu ametoa uhuru wa maamuzi kwa binadamu, hata shetani alitumia uhuru huo kuasi na ndio maana yupo mpaka leo. Mungu si dikteta..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapo fanya maamuzi bila kua na maarifa katika kileunacho amua sikuzote hatima yake ni kuangamia.. na shetani huwatumia wasio na maarifa maana hao hawata kielewa wanacho kiongea mbele za watu..
Nakushauri tafuta kwanza maarifa ya Mungu uyaelewe ndio ufanye maamuzi.. na nahakika baada ya kuyaelewa huwezi fanya haya..

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini unishauri nitafute maarifa ya mungu ambayo tayali yamejikita kuelezea chuki dhidi ya shetani je kuna kitu gani kipya nitakachojifunza hapo ambapo?

Mimi nilifikiri utanipa ushauri wa kusoma vitabu vyenye maelezo ambayo yametolewa na shetani ili niweze kupima mizani ya haki kubaini nani anastahili kulaumiwa kati ya mungu na shetani, lakini wewe unanisisitizia kusoma tena habari za mungu ambazo zimetoa maelezo yenye kumuonesha shetani ni mbaya

Sent using unknown device
 
Sijakubali,bali ni kwa wale walio muasi Mola ndio anaweza kuwarubuni ila wale wenye kumtii Mola hawezi kuwarubuni. Hapa unatakiwa uelewe maneno.

mkuuu kulingana na iman hizi za kidin mtu asiye mjua mungu wala kumfuata huyo ndio wa shetani leo hiii unatumia na kuamini science and technology wakati ujui vinapotokea au miongon mwa wale wajuzi au wagunduzi wa hivyo vitu bado walipinga uepo wa mungu na nguvu zake

washika din wote niwatumwa wa science and technology pia haya mapinduzi ya kiteknolojia kuna nguvu zaid ya kibinadam inayorun kwa nyuma ya pazia
 
Adhabu ya milele ni ile kuishi motoni (jahanam) na hiyo ni baada ya kufa, hivyo shetani baada ya kuasi aliondolewa katika wale viumbe wema, kwa kuwa aliomba aishi kwa muda mrefu ndiyo maana Mungu alimkubaliya ombi lake rejea kwenye aya za Kurani 15:26-50 hapo chini:-

26. Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura. 26

27. Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto. 27

28. Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura. 28

29. Basi nitakapo mkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi mumwangukie kumsujudia. 29

30. Basi Malaika wote pamoja walimsujudia, 30

31. Isipo kuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na walio sujudu. 31

32. (Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata hukuwa pamoja na walio sujudu? 32

33. Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliye muumba kwa udongo unaotoa sauti, unao tokana na matope yenye sura. 33

34. (Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe ni maluuni! 34

35. Na hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo. 35

36. Akasema (Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watapofufuliwa. 36

37. (Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika walio pewa muhula 37

38. Mpaka siku ya wakati maalumu. 38

39. Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote, 39

40. Ila waja wako walio safika. 40

41. Akasema: Hii Njia ya kujia kwangu Iliyo Nyooka. 41

42. Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipo kuwa wale wapotofu walio kufuata. 42

43. Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipo ahidiwa wote. 43

44. Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewa. 44

45. Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem. 45

46. (Wataambiwa:) Ingieni kwa salama na amani. 46

47. Na tutaondoa chuki iliyo kuwamo vifuani mwao, wawe ndugu juu ya viti vya enzi wameelekeana. 47

48. Humo hayatawagusa machofu, wala hawatatolewa humo. 48

49. Waambie waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 49

50. Na kwamba adhabu yangu ndio adhabu iliyo chungu! 50
Udongo unaotoa sauti uko vipi? Naomba ufafanuzi hapa

Sent using unknown device
 
Back
Top Bottom