Kwanini mtu anajiua kwa ajili ya mapenzi?

Sasa ukijiuwa si ndio unawaachia waungwana wajisevie kwa raha zao!! huyo lazima atakuwa mnyarukolo.
Acha hizo Mr Valentine.
Hata mimi usipotokea siku ya Valentine najinyonga na uzi wa kushonea nguo.
 
Waswahili wanamsemo usemao usilolijua ni kama usiku wa giza, samahani kama nitakuwa nimeukosea huo msemo. Ila kwa suala zima la watu kujiua kwa ajili ya mapenzi haitakuwa sahihi tukisema ni ujinga, ni kweli kujiua sio suluhisho ila mkumbuke mpaka mtu anachukua uamuzi huo tayari anakuwa kwenye hali ambayo amekata tamaa, kuchanganyikiwa,anajihisi hopeless, ana kuwa na msongo wa mawazo na mambo mengine mengi ambayo kwa wakati ule yanamfanya kutokuwa normal na kushindwa kuona upande wa pili.
Mtakumbuka ule wimbo wa Msondo ngoma ulioimbwa na Marehemu TX Moshi ambapo ndani yake kuna maneno haya namnukuu......"Mapenzi yakikuchanganyia ni faraja moyoni ila yakikuchachia yaweza kuwa sumu inayoweza kuua kwa dakika chache......akaendelea kwa kusema .....wakati hawa wanafunga ndoa pale mtaa wa pili kuna kijana amejinyonga kwa sababu ya mapenzi... ni wimbo mzuri kama una nafasi utafute uusikilize.

Sio kwamba natetea watu kujiua kwa sababu ya mapenzi ila hoja yangu ni kupingana na watu wanaosema hao wanao jinyonga ni wajinga hapana, Mwombe Mungu yasikukute, kuna watu wamepitia mambo magumu sana ukikaa nao wakakueleza utawasikitikia na ilifika mahala wakawa na mawazo ya kujiua ila kwa rehema za Mungu walisalimika ukipata wasaa wa kuzungumza nao unaweza ukanielewa nina maanisha nini kusema sio wote wanaojiua ni wajinga, na sio kwamba wanapenda kujiua hapana.

Anyway.
 
Hahaha. . . Jibaba.
Alafu wewe jana siulikua unalalamika eti Valentine imekaribia na Lizzy humuoni. . ina maana hukumpenda jimama hata kidogo?
Ndio mahaba yenyewe hayo segito. Si unajuwa hata wahindi lazima umuimbie song muchuchu ili kumuweka sawa!!
 
Wanaojiua wanakuwa wamechoka kuishi tu, labda tuwaulize wanaoua wapenzi wao, wao ni nini kinawasukuma kuua? Manake kama ni kusalitiwa si mnaachana tu halafu maisha yanaendelea, kwani lazima uue ndio ujiskie amani?
 
Wengi huchukua maamuzi sababu ya hasira.... Wengine they cant stand the thought of being betrayed after putting a total trust on a person... Wengine ndio hivyo mapenzi yaliyopitiliza anaona maisha hayana thamani tena...
 
Huo ni ushamba wa kimapenzi, mtu hakukujali halafu ujiue kwa ajili yake ni ujinga mkubwa, ukiachwa piga myo konde na songa mbele hujui matatizo aliyokuepushia, mbona kabla hamjakutana uliishi vizuri tu, so just imagine mahusiano yako na yake ilikuwa ni kama ndoto ambayo itaisha muda si mrefu.

  • :rant:
 
Labda hao wanakuwa hawana kitu kingine kizuri kwenye maisha yao zaidi ya hayo mapenzi.
 
Hata sijui niseme ni nini. kwanza ni ubinafsi wa hali ya juu kuacha wanaokupenda kama ndugu/wazazi wako kisa mpenzi aliyekusaliti na umekutana nae tu katika maisha haya.
Kuna cousin sister wangu alijiua kisa mpenzi hivyo hivyo, jamani sijawahi kuelewa alifikiria nini. Dada mzuri kawaacha wazazi wake na kaka yake kisa mpenzi. Huyo mpenzi wake aliendelea na maisha yake na kuoa zake.
Hata kama ni kupenda, kujiua kisa binadamu mwenzio ni ujinga wa wali ya juu.
 
Mambo ya hovyo ni ya hovyo,haijalishi unaufaham nayo ama la!
 
ndg yangu acha haya mambo yakupite isitokee kwako,binafsi nilitaka kuingia hiyo dhambi mda mrefu sana,maana nilisalitiwa na pia nikafilisiwa kila kitu.haikuwahi kutokea ktk maisha mwanamke kunifanya hivyo, niliingia uchizi na maamuzi niliyochukua ni kujiondoa. Badae nikaghairi kuondoka mwenyewe nikaona nikamfanyie kwanza huyo demu kisha nijimalize.mungu yupo bwana siku hiyo nimejiandaa na silaha zangu kamili gado nikaenda pahali kupata stimu si nikaibiwa hizo silaha zenyewe!
Isingekua hivyo walah saizi ningekua naongelea segerea
angalia sasa baada ya hapo nikajisahaulisha nikaendeleza life nikaja oa mbali hukooo
na kuwa na good time tu,yule mama aliyetaka niingie matatizoni yupo ila ndo hivyo life imempiga mbaya kawa changu mwerevu siku hizi
 
the major reason is a failure of ones control of his/her emotions and dis is a great weakness i always consider.
 
Back
Top Bottom