Kwanini msimu wa zambarau, maembe...

KakaJambazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2009
Posts
18,828
Reaction score
12,321
Ukiotesha miembe 12, katika miezi 12, yani kila mwezi unaotesha mwembe mmoja, wakati wa mavuno huwa ni mmoja, vivyo hivyo kwa mizambarau.
Leo hii miembe ya zamani yenye miaka 50 plus, ina msimu mmoja na hii ya kisasa ya mwaka mmoja. Je ni kwanini?
Mi nilizani labda ni kutokana na uchevushaji, yani kipindi flani nyuki wanakua wengi huko misutuni, lakini mbona kuna kuna njia nyingi tu za uchevushaji?
 
Ili mmea uweze kuzalisha matunda inabidi kwanza utengeneze maua, Hii ni njia ya kuendeleza kizazi "species". Kifupi ni kwamba UA ndio chimbuko la TUNDA.
Kama ilivyo kwa wanyama ambao kuna majira fulani ya mwaka huwa katika JOTO, vivyo hivyo hata mimea huwa na majira ya kutengeneza MATUNDA ambayo kwayo kuna MBEGU ambayo(zo) ndio chanzo cha uhai wa MMEA.


Sasa kwa asili ili mmea mathalani MWEMBE uweze kutoa MAUA ambayo yatapelekea kutengenezwa kwa MATUNDA, huwa unahitaji mazingira maridhawa ambayo hayatakuwa kikwazo cha ukuaji wa MAUA.
Ninaposema mazingira maridhawa, moja kwa moja ninamaanisha ya hali ya hewa. Ikumbukwe kwamba zao la MWEMBE hukua kwenye hali ya hewa ya Kitropiki.
Ili MWEMBE uweze kutoa maua, unahitaji kiwango fulani cha jotoridi, hali ya hewa ya unyevu au umande (high humidity and dew), mvua.
Aina hii ya Hali ya Hewa hupatikana wakati huo ambao huwa unaona Miembe inatoa MAUA na hatimaye MATUNDA.
 

Mkuu asante.
Ila ukichukulia ishu ya hali ya hewa, inakuache msimu wa maembe au machungwa unakua mmoja nchi nzima?
 
Mkuu asante.
Ila ukichukulia ishu ya hali ya hewa, inakuache msimu wa maembe au machungwa unakua mmoja nchi nzima?

Mmmh kwa ufahamu wangu nadhani MAEMBE na MACHUNGWA huwa majira tofauti ya Mwaka

Kama utakuwa na muda, jaribu kupitia hii Article mkuu MAEMBE
 
Bado naendelea kutafuta majibu, kwa nini huu msimu mfano wilaya nzima Kuna maembe wakati kila mtu alipanda mmea kwa wakati wake!?
 
Bado naendelea kutafuta majibu, kwa nini huu msimu mfano wilaya nzima Kuna maembe wakati kila mtu alipanda mmea kwa wakati wake!?
Mkuu mbona huyo mtaalamu comment #2 kakujibu kisomi sana kwanini haujamuelewa?

Kakujibu kuwa hayo maembe unayoongelea wewe, mfumo wake wa kutoa maua (kuzaa) huendana na mfumo wa hali ya hewa kutokana na eneo husika.

Halafu kusema kwamba msimu wa kuzaa maembe ni mmoja nchi nzima si kweli, nenda Kariakoo kila siku utapata embe.

Hivyo misimu na hali ya hewa imetofautiana eneo na eneo.

Kuhusu machungwa kama yanapata maji ya kutosha hayana musimu, huzaa muda wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…