Wakuu mimi sio gamba na sitakuwa gamba. Swali hili ni muhimu kujibiwa kwa umakini. Zitto mwenyewe alishawahi kunukuliwa akilalamika udini unamtengenezea maadui ndani ya chama. Na hili la Mnyika kukaimu sio mara ya kwanza. Hii sababu ya ugonjwa sioni kama ina mantiki kwa sababu kwenye ukatibu hakuna kazi ya kubeba zege, ni busara na maamuzi tu. Kama Zitto aliweza kuongea na media alipotoka India na bado akaenda kufungua kongamano la vijana wa kiafrika lililoandaliwa kwa ushirikiano na Bavicha sioni kama ana ugonjwa unaomfanya asiweze kukaimu ukatibu mkuu. Hata kama Dokta Slaa alienda kuuguza familia kipindi ambacho Zitto alikuwa India bado Zitto baada ya kurudi alipaswa kukaimu hiyo nafasi.
Kuna jambo cdm hawataki kuliweka wazi kuhusu Zitto. Ni kama vile haaminiki!