Kwanini mnawaamini wanasiasa?

Mtu mzito

JF-Expert Member
May 13, 2016
1,779
3,183
Habari ndugu
Kuna watu wanaamini wanasiasa kiasi cha kutukanana na wale walio upande wa pili, wasomi wetu na ma profesa wamekuwa ni bure kabisa! Hawasimamii elimu yao zaidi ya kufuata mkumbo wa wanasiasa.
Vijana wetu ndio huwaelezi kitu kabisa, yaani mtu atapambana maneno hata kama chama lake limevurunda!
Wapo wanasiasa walituaminisha kuwa Lowassa ni fisadi papa na kusema ushahidi wanao.....tukawaamini kabisa kabisa lakini ghafla akagombea urais huku huku kwa malaika!!! Bado niendelee kuamini watu hao?

Yupo aliyejitamba kuwa atapambana na mafisadi na tukamsikiliza tukijua atapambana na Richmond, Escrow, na majizi yaliyokuwa magogoni awali, mwisho wake anawafukuza wale waliopewa amri na mabwana wakubwa tu.....bado niwaamini wanasiasa??

Msiwatusi viongozi wenu ila tumieni akili zenu kupambanua
 
Uko sahihi, ila kuna wale ambao wako kama hivi"" ngoja niwatukane chama cha pili lbda na mi ntaonekana kwa mweshimiwa kwenye uteuzi flani"" au ntapata suport nitakapokuwa nagombea;; kama hivo
 
Nchi inamshinda mapemaa hata mwaka ajamaliza nchi haiendeshwi na mtu mmoja kupenda sifa kunakera watu kibao fukuza mtu mfunge si mwizi? Kwanini mnatuchezea kiini macho nchi imejawa na ukabila atuwezi kufika jamaa kajisahau sana tena mapema kabana mzunguko wa pesa watu wanakimbia nje ya nch mambo ayaendi
 
Tz bhana!kugumu sana,JPM nae imembamba,amebak na majipu yasiyo na uelekeo wa kumwinua mwananchi kiuchumi,sion uelekeo wa nchi.
 
Ni ujinga ujinga tu kuwapigania watu kama unalala nao kitanda kimoja wakati wenzako wanajaza account zao na kunufaika na familia zao, wananchi ni kama soko na wanasiasa wanatangaza biashara zao na kuzisifu hata kama ni uongo.

Hakuna cha upinzani wala watawala wote ni wale wale tu ila kinachofanyika ni huyu kuwaaminisha kuwa anafanya (ili mumchague tena) na huyu kuwaaminisha yule hafanyi (hata kama anafanya) ili mumchague yeye.

Hata Magu atende mambo kwa kutumia katiba ya Ukawa, haitatokea Ukawa wakamkubali na kusema wanamuunga mkono sababu anawakomboa wananchi.

Na hata Ukawa wakileta maendeleo kiasi gani katika majimbo na halmashauri walizopata, bado Ccm haitawasifu itatafuta madhaifu au kuwawekea uzito katika miradi mbali mbali.

Umegundua nini?

Hawana nia ya dhati kutukomboa wananchi bali wanatufanya soko la kutuuzia maneno ili wajaze matumbo yao.

SASA WEWE TOKA MISHIPA YA SHINGO UTETEE UVYAMA KAMA UNAMTETEA MAMAAKO MZAZI WAKATI HATA UKIFA HAWAKUJUI.
JITAMBUE
 
Waache mihemko wakati wenzao wanapiga noti

Ndugu umepiga nondo zilizosimama hata mimi nakupa bigup. Sasa hebu tuambie nini kifanyike maana hakuna chochote utakakachofanya nchi hii bila ruhusa ya mwanasiasa. Hakuna uwezekano wa wewe kufanya mradi mkubwa bila mwanasiasa kutia baraka zake. Kila kitengo cha maamuzi katika nchi hii kinapata uamuzi wa mwanasiasa penda usipende. Unapoona wengi wanaamini wanasiasa, sio kweli kwamba wanawaamini bali wengi wanatarajia mwanasiasa fulani akipata madaraka na yeye atatoka kimaisha. Wananchi wengine wao hawana wajualo zaidi ya kuuziwa matangazo ya maisha bora, ni kabila langu, ni dini yangu nk na wanasiasa hapo wanageuza siasa kuwa mechi ya simba na yanga. Hebu tuambie tufuate mfumo gani maana hata kodi zetu zikikusanywa wanasiasa ndio wanapanga vipaombele.
 
Ni kweli wanasimamia kila kitu ila tusiuze utu wetu, fikra zetu, na wanapokosea tusione haya kuwakosoa kisa tuko upande wao.
Na pia tusijigawe kisa wao, tusipigane, kuuwana na hata kutukanana kisa tuna itikadi tofauti za vyama.
Tunaowapigania hawana nia ya kutupigania kwa dhati zaidi ya kutufanya mtaji wa kufanikiwa wao.
 
Ndugu yangu naona kama unakosea, kwanza kumbuka kila mtu ana uwezo wake wa kufikiri. Hilo la kuuna sioni kama kwenye nchi yetu linatokea japo huko mbeleni inawezekana. Kuwakosoa tunawakosoa sana, labda wanaoogopa kukosoana ni wale wenye itikadi moja. Kutukanana hili litakuwa gumu sana kwani tayari ushabiki umekuwa kama wa timu za mpira, kwani huko kwenye timu za mpira watu wanavyotukanana na kupigana vijembe unadhani wachezaji wanawagaia washabiki wao hela? Hilo la wanasiasa la kuwafanya wananchi ndio mtaji wao haliepukiki maana ndio nature ilivyo, ili mwanasiasa apate nafasi lazima apate wanaomuunga mkono. Ila kwamba watatukomboa ama la hilo wanye ushabiki hawana muda wa kuliangalia kwani kipendacho roho....
 
Umekwenda vizuri, hao wenye itikadi moja ndio ninao waongelea.....mpira hawakusanyi kodi zetu wala kugawana ruzuku.
Kuhusu kuuwana kwa sababu za kisiasa kupo sana haswa kwa madiwani na hata wafuasi
 
Back
Top Bottom