Kwanini? Mmeteleza

Kwanini? Mmeteleza

Yaani hadi twende mahakamani ili itusaidie kutafsiri nani ni mtumishi wa umma na nani lah?, JPM hata wateule wako wengine wamedesa hadi vyeti, fagio lifagie kote.
 
Na amesema majizi na hayo majambazi yafungwe miaka saba. Sijui ni kina nani hao
 
Labda wateuzi wa Rais hufanyiwa uchunguzi wa kina na idara mbali mbali nyeti za serikali, mpaka uteuliwe na Rais unakuwa umechunguzwa kweli kweli, labda ndio maana hawakuona haja ya kuhakiki vyeti vyao.Ili kuondoa malalamiko ya double standards ilibidi tu wafanye huo mchakato mdogo wa kuhakiki cheti tu maana wateuzi wa Rais huhakikiwa mambo mengi🙄
 
Hakika hizi dhambi ipo siku zitawatafuna tu, haiwezekani wote walipwe mishahara na serikali ila linapokuja swala la uhakiki wa kitaaluma wanyonge wakaguliwe na wengine walindwe. Hili swala halikubaliki na Magufuli tayari umefel katika kila jambo isipokuwa katika kuwalinda akina bashite and co
Najiuliza maswali mengi bila majibu. Kubwa nikwamba utekelezaji wa zoezi hili litakuaje ikiwa msimamizi na mfuatiliaji wa vyeti feki ni miongoni mwa wale waliowekwa pembeni wasiguswe ktk zoezi hili naye akijua wazi kuwa vyeti vyake sio halali, atawezaje kuwa na ujasiri wakumuajibisha mtu? Nafikiri kuna baadhi ya maafisa elimu watakuwa wamekumbwa ktk zoezi hili, ni wakati wao sasa kuwanyooshea vidole wale wote ambao waliwahi kuwa wanafunzi wao na wanawafahamu vema majina wanayoyatumia kwa sasa kwamba sio yao lkn kwakuwa wamewekwa pembeni ktk zoezi hili basi hakuna namna nyingine zaidi yakupasa sauti zao kuonyesha kutokubaliana na ubaguzi huu wa hali yajuu kutokea toka tulipopata uhuru.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom