VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Uhakiki wa vyeti vya kitaaluma ulipaswa kuwa wa haki. Uhakiki ulipaswa kuwahusu wote wanaopokea mishahara ya kiserikali. Kuwaacha pembeni Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Wakuu wa mikoa, Wakuu wa Wilaya na kadhalika si sahihi na ni kuwaangusha watanzania. Watanzania watashtushwa sana na hili.
Hoja hapa si kujua kusoma na kuandika. Hoja ni kughushi cheti cha kitaaluma. Hoja ni kudai kuwa una cheti/sifa fulani wakati huna. Hoja hapa ni jinai inayoendena na kughushi cheti. Kusema una shahada, stashahada au astashahada ndiko kunakoambatana na uteuzi wako katika nafasi fulani. Ni kosa kubwa kuwaacha wateule wa Rais pembeni katika uhakiki wa vyeti vya kitaaluma.
Kwanini tuache Rais wetu azungukwe na kuwaamini matapeli wa kitaaluma? Kwanini tumuache Rais wetu alaghaiwe na wasaidizi wake kuwa wana taaluma fulani wakati hawana? Rais na Waziri Kairuki, mtaikumbuka siku ya leo kama siku mliyowaangusha watanzania na kuwaonesha ubaguzi wa wazi wa kiserikali. Mmefanya kosa kubwa.
Ndiyo maana Waziri Kairuki ulikuwa 'unajishtukia'. Haukujiamini. Nilikukazia sana macho pale Ukumbini. Nilitikisa na kichwa changu. Matapeli wakubwa ni walioachwa kwenye uhakiki wa vyeti kwakuwa wao ndiyo wanaopokea mishahara minene na minono. Wao ndiyo wakitapeli wana athari kwa taifa kwa ujumla. Hamkuwatendea haki watumishi wengine na watanzania kwa ujumla.
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)