Kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia takwimu mbali mbali kupitia vyombo mbali mbali kuwa mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi na waathirika wa UKIMWI.
Swali langu ni la kidadisi(curiosity). Napenda kusikia toka kwa wataalamu na watafiti(kama tafiti zipo), kwanini isiwe majiji na mikoa mikubwa kama Dar, Mwanza, Mbeya n.k? Kama awali ilikuwa mkoa wa Kagera ndiyo ulioripotiwa mgonjwa wa kwanza na baadaye kuwa na waathirika wengi, ilikuwaje HIV iliruka mikoa ya hapo kati(Shinyanga, Tabora, Dodoma, Singida...) na kuufanya mkoa wa Njombe kuongoza?
Kama ni tohara kwa wanaume je, ni mikoa mingapi Tanzania hii walichelea kufanya tohara? Kwanini mikoa hiyo haijaathirika kiasi hicho? Japo kwa zamani(ninavyokumbuka) wilaya ya Makete(Njombe) ndiyo iliyokuwa ikiongoza na kwa sasa sina taarifa rasmi, bado ni jambo ambalo sina majibu yake, ilikuwaje mkoa wa Njombe uongoze kwa maambukizi?
Naomba wenye kufahamu majibu ya swali langu la msingi wanisaidie.
Kwanini Njombe?
Takwimu zinaonyesha maambukizi njombe ni 14.8% na ndo mkoa unaoongoza. Sababu za maambukizi ya VVU kuwa juu ni:-
Moja, Biashara ya viazi mviringo. Biashara hii huwaleta wafanyabiashara na madereva, matingo wa malory, na makuli ambao hulala vijijini wakikusanya na kupakia viazi. Watu hawa kwa kuwa na fedha hufanya sana ngono zembe na wanawake wa vijijini.
Mbili, Tohara kwa wanaume haikwepo kwa Kabila la wabena, pangwa nk.
Tatu, idadi ya wanawake mabinti ni ndogo kulinganisha na wanaume. Mkoa huu nazani ndio unaoongoza kwa kutoa house girls wengi Tanzania. Hivyo unakuta mwanamke mmoja anagombaniwa na wanaume kumi na zaidi no way out.
Nne, Ulevi hasa kwa wanawake hasa njombe vijijini, na ludewa na makete pia.
Tano, house girls hurudi kwao na VVU na kwa uchache wa wanawake basi kila mwanaume kijijini ata mlala kwa uzuri wake.
Sita, uhaba wa kondomu vijijini. Maduka mengi vijijini hayauzi kondomu. Unaweza tafuta kondomu ludende siku nzima usiipate.
Saba, biashara ya mbao nk