Kwanini Mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi ya HIV Tanzania?

Mbao zinauzwa na wabena na Wakinga. Njombe ni mkoa ambapo wangeni wachache sana au Hakuna kwenye biashara, kama Malori Dar, Dodoma na Moro ni Mengi kuliko huku.
Kula like mkuu.
Binafsi naunga mkono hoja ya biashara ya mbao na viazi. Hizo biashara zinafanyika kwa mapana sana na ndipo hapo wafanyabiashara hupata nafasi ya kurubuni wanawake vijijini kwa fedha nyingi na kuwalala.
Unategemea nini kama si kuambukizwa ukimwi?
Kingine ambacho umesahau ni njia panda. Ile ni njia panda ya kuelekea Mbeya na Ruvuma. Hivyo magari mengi hupumzika hapo baada ya kupima kwenye mzani. Sasa kama mjuavyo madereva wetu wakilala sehemu tena yenye baridi kama ile lazima walale na wanawake.
Mengineyo yote naunga mkono hoja zako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achana na hizo % Dar ndo inawathirika wengi kuliko mkoa wowote hapa TZ, idadi ya watu mkoa wa njombe ni tarafa moja tu ya Dar
Mkuu unafahamu "uwiano" au ratio? Hiki ndicho kinachozungumziwa.
 
Mkuu unafahamu "uwiano" au ratio? Hiki ndicho kinachozungumziwa.
Sio uwiano tu hadi calculus najua, check kwa mfano:-
-watu 30/100=30% mkoa wa Njombe
-120/1000=12% mkoa wa Dar
Hope utakuwa umeelewa point yangu.
-
 
Sio uwiano tu hadi calculus najua, check kwa mfano:-
-watu 30/100=30% mkoa wa Njombe
-120/1000=12% mkoa wa Dar
Hope utakuwa umeelewa point yangu.
-
Mkuu bado kuna kitu unaki-miss.
Uwiano ninaouzungumzia ni kama vile ukiweka vijiko vitano vya sukari kwenye kikombe cha chai cha robo lita, effect yake haitakuwa sawa na kuweka vijiko vitano vya chai kwenye pipa la chai la Lita 200. Kwa hiyo hata kama idadi ya waathirika wa mkoa wa Njombe ni sawa na idadi ya waathirika wa jiji la Dar, uwiano wa idadi ya waathirika kwa ile idadi ya watu wote kwa mkoa mzima itaonesha kuwa Njombe iko juu kuliko Dar kwa kuwa Njombe ina idadi ndogo ya watu kuliko Dar. Kama sijaeleweka Niko tayari kujaribu kuelezea hili.
Hayo mambo ya calculus ya kina Sir Isaac Newton tuyaache.
CC: Papa Mobimba
 
Back
Top Bottom