Kwanini mke wangu hataki kunisamehe?

Kwanini mke wangu hataki kunisamehe?

Wakuu habari ya ujenzi wa taifa,

Kwa kweli hadi leo sijui nini kilinipata hadi nikatembea na shemeji yangu mdogo wa mke wangu wa ukoo.Kama si yule binti kunirubuni nisingefikia hatua ya kufanya kitendo hicho.

Historia ya tatizo:
Mwanzoni mwa mwaka jana wife aliniomba nimuombee kazi au nimpe kazi mdogo wake mtoto wa babake mkubwa ambae amemaliza chuo mwaka juzi. Hapo ninapofanya kazi mimi ni Administrative Officer ni kiwanda cha wahindi, hivyo haikua shida nikapigana kiume akaanza kazi ingawa sio ya mshahara mkubwa maana wahindi mnawajua walivyo. Miezi 4 mbele akaniambia ana zawadi yangu niifute alipopanga maana hawezi kuibeba kuja nayo kazini, ni shukrani kwa kazi niliyompa,ikawa kila nikifika kazini asubuhi huja ofisini kwangu kuniuliza kwa nn Jana yake sikweenda kwake

Siku moja nikamwambia basi leo tuongozane nina nafasi tulipofika pale akanipa shati jipya nikamshukuru akaniuliza haujaribishi nikufanyie na massage ya mgongo?Kwa kweli sijui nilikua nawaza nn nikajibu sawa akaaenda duka La dawa akanunua olive oil akaja nayo chumba ni kimoja tu hivyo akaanza kunifanyia masage huku tunapiga story mbalimbali Ilifika pahala nikawa sina nguvu hata ya kuongea tena hasa alipoanza kifuani kushuka chini, nilihisi ni shoti ya Umeme imenipiga.

Zoezi zima likawa limekamilika na ukawa ni mchezo wetu kila mara, na hatukuwahi kwenda guest tulikua tukifanyia hapo hadi siku moja ambayo tulisikia hodi ikigongwa na binti kwenda kufungua na kukutana uso kwa uso na dada yake yaani mke wangu mimi.Mimi nilikua ndani ya shuka kitandani kama nilivyozaliwa.Mke wangu akaingia akaanza kulia mbele yangu, walikuepo na kaka zake wawili na ndugu wengine watatu wanawake kumbe walitufuatilia kutoka kazini hadi hapo baada kutuchunguza kwa muda mrefu

Matokeo:
Wife alibeba vitu vyake vyote akaondoka na watoto akarudi kwao baadae akaenda kupanga sehemu ambapo anaishi hadi sasa. Nimemuomba msamaha katika ngazi zote za familia na hata ngazi ya kanisa na hadi kwa paroko bado amekataa kunisamehe.Nimetuma marafiki zake na watu Wa heshima na hata bosi wake kazini anisaidie kuzungumza nae ndio kwanza akanitukana kwa nn nimeenda ofisini kwake.Hataki hata niende kuwaona watoto wangu pale anapoishi.

Wakuu nimefanya kosa gani kubwa la kustahili haya yote? Umeshakatika mwaka tangu aondoke home kwa tatizo hili sioni dalili njema siku za usoni na mimi nampenda mke wangu nahitaji turudiane cha kushangaza nyumbani kwao wanaona kama mimi ndio niliemrubuni yule shemeji yangu kwa aijili ya kumpa kazi wakati yeye ndio alinirubuni mimi.

Kwanini anakua na roho mbaya kiasi cha kushindwa kumsamehe mtu? Akina dada ukikosewa kiasi hiki unaweza kutaka kufanyiwa nini ili usamehe? Kwa ujumla napaswa kufanya kitu gani hasa kuweza kumu win tena wife? Maana kuna wanaomshawishi akadai talaka mahakamani sinajua a awaza nn kwa sasa.Nimekuja kwenu kwa Mara ya kwanza as a last resort to this problem.

Wana JF nifanye lipi liliobaki ili mke wangu arudi?

Your regards
Hujitambui wewe.
 
kwanza sababu ya kutosamehewa nimeijua , una kauli chafu sana , unaleta ubabe japo umekosea,? unasema kabisa " kwa nini anakuwa na roho mbaya kiasi hiki" huoni wewe ndo una roho mbaya??? kwa hiyo unaona usaliti sio kosa la adhabu hio? unajua bibilia na quran vimebainiaha kosa lakuvunja ndoa ni udhinifu???

kwa style hyo maneno uliyoandika nakujiweka kama unaonewa yawezekana ukienda una maneno ya shombo sasa ngoja wenzio wapigepige akichoka vya mtaani hasira itaisha mtarudiana
 
Labda hujaonesha kweli ya dhati kwamba unauhitaji huo msamaha
 
kwanza sababu ya kutosamehewa nimeijua , una kauli chafu sana , unaleta ubabe japo umekosea,? unasema kabisa " kwa nini anakuwa na roho mbaya kiasi hiki" huoni wewe ndo una roho mbaya??? kwa hiyo unaona usaliti sio kosa la adhabu hio? unajua bibilia na quran vimebainiaha kosa lakuvunja ndoa ni udhinifu???

kwa style hyo maneno uliyoandika nakujiweka kama unaonewa yawezekana ukienda una maneno ya shombo sasa ngoja wenzio wapigepige akichoka vya mtaani hasira itaisha mtarudiana

Mtaani wakisha piga piga na hasira zikaisha akarudi kwa jamaa, atakuta jamaa keshavuta demu mwingine yy anageuka jamvi la wageni, bora akubali msamaha wa mshikaji
 
Ameshakusamehe. Angekuwa hajakusamehe angeshakuua....ulikuwa mdogo wake naye amepata mdogo wako anamla!
 
Hahahahahahahaha.....pole na bado hiyo dhambi itakutafuna mpaka uwe chiziiii..hapana chezea laana ya mke......
 
hizo harakati za kuomba msamaha ungezitumia kujiepusha na zinaa na shemeji yako wala yasingetokea hayo
 
Jamani kuna watu wengine wanaokuja hapa washakiri katika nafsi zao kama wamekosea, kama mtu unashindwa kumshauri ni vyema kuwa kimya kuliko kuzidi kumsakama, Mungu anasamehe iweje sie binadamu...Kaka kuhusu mkeo ana haki ya kukasirika nadhani endelea kumpa muda, chakufanya tubu dhambi yako halaf hili swala liweke kwenye maombi Umrudishe kupitia Maombi kwa muumba wako, ila sisi wanawake ni dhaifu mno, kila siku hakikisha unamtumia msg za kumuuliza hali yake na watoto, usiombe msamaha katika hizo msg bali ulizia hali, na pia umwambie kama utakuwa na tatizo lolote la kifedha nambie n.k..kifupi onyesha kumjali kwa kutumia mawasiliano ya simu, kama yupo kwenye whassap weka picha yenu ya harusi ikae hapo milele.....muongee muda ila usikate mawasiliano ya msg kila leo na hata simu piga kama anapokea kama hapokei endeleza msg ili asikusahau kwa haraka....fanya kama wamtongoza sasa.
 
Hustahili kusamehewa kabisa. Geuza hiyo story hlf wewe ndio uwe umemfumania mkeo ingekuwaje?...ungempa kipigo cha nguvu na kumfukuza ungemfukuza. Tena wanaume huwa hamsamehi kitu km hicho...iweje unamuona mkeo mkatili? Wewe ndio mkatili haswa..hukuona wanawake wengine mpk utembee na ndugu yake.

Halafu unatoa sababu za kijinga eti alikurubuni! Wanaume bana! Ukitaka kuchepuka nenda mzima mzima na akili zako timamu. Sio baadae useme umerubuniwa.

Pole...
Naomba namba ya mkeo nimpongeze.
Kuchepuka tunachepuka...tukikamatwa inakuwa Bahati mbaya...hatusemi tumerubuniwa...ukichepuka unakuwa na akili zako timamu na unajua nn unafanya. No regrets baadae
 
Mama mbona umekua mkali sana, mwanaume kuchepuka ni jambo la kawaida
 
Mama mbona umekua mkali sana, mwanaume kuchepuka ni jambo la kawaida

Ni kweli ni jambo la kawaida lkn hizo sababu anazotoa ndio zinaudhi..amesema amerubuniwa! Kha!
Na why amuite mkewe mkatili, kwa lipi?
Halafu why atembee na ndugu wa mke wake? Naamini angekuwa ni mwanamke mwingine ambaye si ndugu wa mke wake angeweza kusamehewa.
 
Kasafishe nyota hahahaaaa.
Kuna kaka mmoja aliniambia akimfanyia mkewe kosa akiona atamind anapitia kwa mganga akirudi nyumban hali shwarii.
Tahadhari... chukuaa hatua
 
Jamani kuna watu wengine wanaokuja hapa washakiri katika nafsi zao kama wamekosea, kama mtu unashindwa kumshauri ni vyema kuwa kimya kuliko kuzidi kumsakama, Mungu anasamehe iweje sie binadamu...Kaka kuhusu mkeo ana haki ya kukasirika nadhani endelea kumpa muda, chakufanya tubu dhambi yako halaf hili swala liweke kwenye maombi Umrudishe kupitia Maombi kwa muumba wako, ila sisi wanawake ni dhaifu mno, kila siku hakikisha unamtumia msg za kumuuliza hali yake na watoto, usiombe msamaha katika hizo msg bali ulizia hali, na pia umwambie kama utakuwa na tatizo lolote la kifedha nambie n.k..kifupi onyesha kumjali kwa kutumia mawasiliano ya simu, kama yupo kwenye whassap weka picha yenu ya harusi ikae hapo milele.....muongee muda ila usikate mawasiliano ya msg kila leo na hata simu piga kama anapokea kama hapokei endeleza msg ili asikusahau kwa haraka....fanya kama wamtongoza sasa.

Follow this advice. Very wise. Thank you for this advice ..Thanks..
 
Hawa Act bora tu wangekubali kujiunga ukawa coz wote ni vyama vya upinzani kwa ccm .Sera za vyama tu ndio vinawatofautisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom