Kwanini mimi mvivu kusoma?

Kwanini mimi mvivu kusoma?

Mgboss

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
497
Reaction score
279
Wana jf habarini, naamini humu kuna walimu, wataalamu, wanafunzi na wote waliopitia katika suala zima la elimu, uzoefu wenu kama walimu, au wataalamu naamini naweza kupata msaada wa jambo linalonisumbua.

Katika maisha yangu kielimu ni kwamba mimi ni mwanafunzi wa kidato cha tano CBG, na matokeo yangu nina III ya 23 nimesomea shule za kata, na matokeo hayo yamesababisha hata nisichaguliwe shule za serikali japokuwa nimebalance kombi 3(CBG,HKL,HGL) ila namshukuru mungu kwani nimepita japokuwa nina matatizo tajwa hapo juu.

Nimejitahidi kuandika ratiba yangu ya kusoma ila ninashindwa kuifata kwa sababu ya mazoea niliyokuwa nayo tangu awali bila ya kujua kwamba masomo ya advance yanahitaji userious tofauti na ya awali.

Usingizi, mitandao, mpira na hata bila sababu nimeshidwa hata kusoma angalau somo moha tu kwa siku, nasikitika sana kwani nashindwa, nikitaka kusoma nashikwa na usingizi na uvivu pamoja na mawazo mengine yanaingiliana, naomba msaada wenu kimawazo pia kitaalamu na mbinu ili niweze kuepukana na hali hiyo sababu nikiangalia mbele naona kama naelekea kupotea, kwa kuwa ndio mwanzo wa masomo kwa form 5 hivyo ni wakati muafaka wa kuomba ushauri na bado sijachelewa.

Tafadhalini naobeni ushauri.
 
Subiri kupigwa nyembe tu mwisho wa form six, we ushaona dalili unasubiri janga???
Nakushauri ungeomba chuo, kufaulu kwa GPA ni rahisi kuliko hio njia ulioichagua mdogo wangu! Achana na hio kamari ukapoteza miaka yako miwili buree ohooo!!!
 
Je, kwa nini uko form five (a-level). Lengo la kuendelea kusoma ni nini kwako?
Je unataka uwe nani/ ufanye shughuli gani baadae/ baada ya kumaliza masomo? Umeangalia vigezo vya kukuwezesha kuendelea na masomo ya chuo (kama una nia hiyo) vikoje.

Nina imani ukujua nini unataka kwa maisha yako na jinsi ya kufikia malengo ya ni nini unachotaka, vitakufanya uache uvivu. Jaribu kuangalia mazingira unayojisomea, kama iko peke yako, uvivu utakutawala, uwe na mwenzako au wenzako ambapo mtaulizana au kujadili mambo mbalimbali ya masomo. Mitandao achana nayo, labda kama ni chanzo cha kukuelimisha katika masomo yako.
 
Wana jf habarini, naamini humu kuna walimu, wataalamu, wanafunzi na wote waliopitia katika suala zima la elimu, uzoefu wenu kama walimu, au wataalamu naamini naweza kupata msaada wa jambo linalonisumbua. Katika maisha yangu kielimu ni kwamba mimi ni mwanafunzi wa kidato cha tano CBG, na matokeo yangu nina III ya 23 nimesomea shule za kata, na matokeo hayo yamesababisha hata nisichaguliwe shule za serikali japokuwa nimebalance kombi 3(CBG,HKL,HGL) ila namshukuru mungu kwani nimepita japokuwa nina matatizo tajwa hapo juu. Nimejitahidi kuandika ratiba yangu ya kusoma ila ninashindwa kuifata kwa sababu ya mazoea niliyokuwa nayo tangu awali bila ya kujua kwamba masomo ya advance yanahitaji userious tofauti na ya awali,l. Usingizi, mitandao, mpira na hata bila sababu nimeshidwa hata kusoma angalau somo moha tu kwa siku, nasikitika sana kwani nashindwa, nikitaka kusoma nashikwa na usingizi na uvivu pamoja na mawazo mengine yanaingiliana, naomba msaada wenu kimawazo pia kitaalamu na mbinu ili niweze kuepukana na hali hiyo sababu nikiangalia mbele naona kama naelekea kupotea, kwa kuwa ndio mwanzo wa masomo kwa form 5 hivyo ni wakati muafaka wa kuomba ushauri na bado sijachelewa. Tafadhalini naobeni ushauri.
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
wenzako tulikesha class.
labda mizimu ya kwenu aitaki usome.
 
Jaribu kujiuliza kwa nini ukisoma huelewi. Tatizo sio uvivu wa kusoma, I can assure you wengi wetu ni wavivu, sana tu (Procrastination). Soma kwa malengo, jiwekee mpango wa kumaliza kiasi kidogo cha topic utakayopanga. Achana na kukesha, wanaokesha mara nyingi wanakariri. Komalia somo moja kati ya hayo matatu, maana Credit pass moja (mfano C) ina weight kuliko kupata EEE. Usiogope, wengi wametoka na ni wavivu kuliko wewe
 
Tumia muda mwingi kudiscuss na wenzio na muda mchache ukiwa peke yako itakusaidia sana hiyo njia kwan hata mimi yamenitokea hayo lakini discussion ziliniokoa sana
 
Back
Top Bottom