Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,096
- 22,626
Habari
Kwanini taratibu za mikopo ya Halimashauri ambayo inatokana na 10% ya mapato ya halimashauri husika inalazimisha vijana watakaokopeshwa au kwenda kuomba ni lazima waende kivikundi na kuja na idea za vikundi?
Kwahiyo kwa mfano mimi nina kampuni yangu ya kuuza magari, au nina biashara ya studio ya photoshoot, au nina duka la nguo, au nina mgahawa wa kisasa siwezi kwenda kuboost mtaji wangu kwa kupata mikopo hii nafuu ili nikuze biashara yangu?
Sababu hasa huwa ni nini kinachofanya hawa jamaa wanalazimisha masharti ya kizee na ya kishamba namna hii?!
Kwani hizo hela wanatoa mifukoni mwao au ni za baba zao?!
Hela si ni zetu raia na zinahitajika kufanyia maendeleo yetu.
Hapa nilikuwa natazama kipindi hapo channel 5, DC anahojiwa kuhusu mikopo ya Halimashauri, anatetea hoja ya kuwepo kwa vikundi.
Katika kipindi wamekaribisha vijana wajasiriamali kuelezea maoni yao wengi wameonesha kukerwa na hii hoja ya vikundi na wamewaambia hao maofisa biashara waache kutumia mawazo ya kizee waje kitaa watazame biashara active ambazo zinahitajika mitaji ili kukua. Nyingi si za vikundi....
Vikundi vikundi kwani tunataka kucheza ngoma?
Kila mtu apambane kwa mbinu zake wanaotaka vikundi waende kwenye section ya vikundi, wanaotaka binafsi waende na business plan zao wakabidhi wapewe mpunga wafanye biashara.
Serikali imejazwa watu wenye mawazo ya kijima na ya kibwege sana . Ushamba ushamba tu. Wanajifanya wanazijua risk na hawajawahi kufanya biashara hata ya nyanya.
Sent using Jamii Forums mobile app