Kwanini Mhe. Kagasheki kamwaga unga

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Wakati Mheshimiwa Kagasheki anatangaza kung?€™atuka ni dhahiri kuna sababu nyingi ambazo hata yeye hayupo tayari kuzisema ambazo zimechangia kumshawishi kuwa hana sifa za kuwa waziri wa maliasili na utalii.

Ni rahisi kusahau ya kuwa Mheshimiwa Kagasheki alipoteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii alitamba kuwa kabla ya yeye kufukuzwa kazi atakuwa amewashughulikia waliochini yake kikamilifu na kuwa hayupo tayari kumwaga unga kwa mapungufu ya waliochini yake. Hii kauli ndiyo imemsulubu Mheshimiwa na haya ndiyo maoni yangu:-


a) Aidha mara tu baada ya kuteuliwa kuwa waziri wa maliasili na utalii, Mheshimiwa Kagasheki alikumbana na kashfa ya TANAPA ya kuuawa na majangili kwa faru wa JK na uongozi wa TANAPA uliendelea kufumbia macho mauaji hayo kwa takribani miezi miwili hivi na ikumbukwe faru hao waliligharimu taifa zaidi ya bilioni saba. Kama Kagasheki angelikuwa anajali kauli yake ya kuwa hawezi kuwajibishwa kwa mapungufu ya waliochini yake angeliivunja bodi ya TANAPA na kutengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo kwa uzembe lakini yeye akasimamisha kazi maaskari na baadhi ya watendaji wizarani ambao kiutendaji wala hawawajibiki kwake! Kifupi tu ni kuwa Mheshimiwa Kagasheki alisahau kauli yake na sasa imekuja kumsulubu kiaina hivi. Aliwaogopa kambale akashughulikia dagaa!

b) Aidha wafanyakazi wa TANAPA na baadhi ya idara ya wanyamapori ambao walikuwa amewasimamisha kazi baadaye katika mazingira ya kutatanisha aliwarudisha kazini na hivyo kuua kabisa dhana ya uwajibikaji sasa mambo yakiharibika nani awajibishwe kama siye yeye anayelinda uozo ndani ya Wizara aliyokuwa anaisimamia?

c) Aidha Mheshimiwa Kagasheki amekuwa akiyalazimisha mashirika ya umma yaliyoko chini yake kuwaajiri bila ya kufuata taratibu za mashirika hayo swahiba wake na hivyo kuleta minong?€™ono ya kuwa mbona bosi hafuati sheria ambazo yeye amekuwa anazihimiza na maswahiba wake wamekuwa chanzo cha mivutano na wale ambao wamewakuta.

d) Aidha uhusiano wake na Kamati ya uhifadhi ambayo sasa imemng?€™oa inayoongozwa na Mheshimiwa Lembeli amekuwa na mivutano ya muda sasa kuhusiana na ujenzi wa Hoteli ya Kibo kwenye kingo za Kireta ya Hifadhi ya Ngorongoro. Kamati ya Lembeli ilipinga ujenzi huo kwa sababu za kimazingira wa hiyo Hoteli ambayo inasemekana inamilikiwa na Basil Pesambili Mramba na huku Mheshimiwa Kagasheki akihimiza ijengwe. Mivutano hiyo iliifanya Kamati ya Lembeli kumchukia kuwa anaidharau kwa kutotekeleza maazimio ya kamati hiyo.

e) Aidha kutokana na jeuri na dharau za waziwazi za kuidharau kamati ya uhifadhi tajwa, mahusiano yake na Kamati husika yaliporomoka na ndiyo maana ilipokuja kashfa ya operesheni ya ujangili alijikuta hana pa kuegemea na kamati hiyo ilimwona ni mzigo na hivyo kupendekeza afukuzwe kazi kwa kushindwa kusimamia kikamilifu operesheni tajwa na hivyo kusababisha ukiukwaji wa kutisha wa haki za binadamu.

f) Aidha shehena kubwa ya pembe za ndovu zinazozungumziwa siyo kuwa tembo wanauawa bali ni wizi mkubwa unaendelea katika maghala ya serikali chini ya Wizara yake. Uchunguzi wa kina umeonyesha ya kuwa umri wa hizo pembe ni zaidi ya miaka 10-20 hivyo kuthibitisha ya kuwa maghala yetu yaliyochini ya wizara ya maliasili ndiyo yanaporwa na Mheshimiwa Kagasheki hana jawabu pale.

g) Aidha jitihada zake za kukamata watuhumiwa wa biashara haramu ya pembe za ndovu kama wale wachina inaonekana kuwa ni changa la macho kwani pembe hizo huwa zimeibiwa kutoka maghala anayoyasimamia yeye mwenyewe!

h) Mivutano yake na Meya wa Bukoba mjini tayari ilimdhoofisha kisiasa na hivyo kuanguka kwake lilikuwa ni swala la ni lini badala ya hivi inawezekana? Katika mgogoro tajwa, Kagasheki alionekana hajali masilahi ya chama chake hata kuhatarisha kupoteza viti saba vya madiwani katika mazingira yaliyoonyesha alikuwa anatetea masilahi yake ya mbio za ubunge za mwaka 2015 tu!


i) Aidha akielewa madhambi yake ni lukuki, Mheshimiwa Kagasheki alishiba na kuamua kheri nusu ya shari kulikoni shari kamili?€??€??€?..ndipo alipochukua uamuzi mzito wa kujisalimisha bungeni kuwa kazi imemshinda kabisa na kujiuzulu.

FUNDISHO.
Tuwe waangalifu na kauli zetu kwani siku moja zinaweza kutuumbua mchana kweupe kama hizi za Mheshimiwa Kagasheki.
 
Nilisahau kumpa pole Mheshimiwa kagasheki kwa dhoruba zilizomkuta......POLE MLANGILA!
 
Tatizo ni mfumo katika nchi,tunatakiwa tuwe na Operesheni Ondoa Ufisadi katika nchi,au kamati maalumu ya kuchunguza Ufisadi na kuutokomeza
 
Tatizo ni mfumo katika nchi,tunatakiwa tuwe na Operesheni Ondoa Ufisadi katika nchi,au kamati maalumu ya kuchunguza Ufisadi na kuutokomeza
Hizi operesheni mbona zipo ila tunazichakachua wenyewe? Operesheni rekebisha mfumo si ndiyo hiyo ya katiba mpya sasa angalia sura na mwelekeo iliyochukua ni kichekesho kikubwa kabisa.
 
Back
Top Bottom