Kwanini Mh Ahmed Shabiby wa Gairo asipewe sifa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Mh Ahmed Shabiby wa Gairo asipewe sifa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LIGUNIKA, May 21, 2011.

 1. L

  LIGUNIKA New Member

  #1
  May 21, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni muda mrefu tangu mbunge wa jimbo la gairo alipolikwapua jimbo hilo likiwa na hali mbaya sanaa. asipewe sifa kwa nini? tunasema apewe sifa kwanza amelitoa jimbo sehemu mbaya na amejaribu sana kusaidia watu wengi kwa namna moja au nyengine kuanzia elimu,maisha,nakadhalika hivyo ukweli anahitaji sifa sana na ninamuombea kwa mungu kamwe asiliachie jimbo la gairo pamoja na wale wote wanaojaribu kumchafua jina lake kisiasa washindwe kwani sisi ndo wakazi wa pale na tunamjua kuliko mtu mwengine yeyote .
   
 2. z

  zamlock JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  sisi atuwezi kumpa sifa kama mtashindwa kuorodhesha aliyo yafanya hapa na ushahidi
   
 3. L

  LIGUNIKA New Member

  #3
  May 21, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunampenda sana mbunge wetu
   
 4. Mlimazunzu

  Mlimazunzu JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 420
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Mpe sifa au lawama mbunge wa jimbo lako. Mie niko Matongoro Shaby saluti 5 nampa
   
 5. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  Aisee ningekuwa mod ningekupa ban miaka mitatu
   
 6. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,083
  Likes Received: 1,729
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe kazi kuu za Mbunge unazijua?
  Ziko tatu:
  1. __________________
  2. _________________
  3. _________________
  Zitaje halafu utwambie ni zipi kati ya hizo (au zote) amezifanya/kamilisha na hatimaye kuleta mabadiliko chanya katika jimbo lenu la Gairo.

  Usisahau kuwa jimbo la uchaguzi siyo mamlaka ya utawala, hivyo halina kikao cha maamuzi, kwa maana maamuzi yote ya kiutawala katika jimbo husika hufanyika ngazi za vijiji na/au halmashauri ya wilaya/mji/manispaa au jiji. Jibu lako sharti lizingatie mifano halisi katika vijiji na/au halmashauri ya wilaya/mji/manispaa au jiji.
  Sifa za kweli iwe ni baada ya kufanya kazi za kweili.
  No cheap politics!
   
 7. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mods kwa nini wasifute thread za kipuuzi kama hizi?
   
 8. C

  Chamkoroma Senior Member

  #8
  May 21, 2011
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumpa sifa au la ni jukumu la waliopo Gairo lkn sioni kuna nn cha ajabu alichofanya, kama kuwasaidia maskini ni sawa, lkn je anavuna kiasi gani kupitia kura zenu? je amewawezesha wangapi kufikia level ya mafanikio? nimefika gairo feb 22 mwaka huu tangu 1991 nikimaanisha miaka 20 nikakuta hakuna lami ktk mitaa ya gairo, pale mbele yaani madukani kama nilivyoona miaka hiyo, sasa kunakitugani cha ajabu ambacho unaona anastahili sifa? jamani elimu kwanza, chapili jamii ya vijana iwezeshwe, kwani gairo madukani haina tofauti sn na kibaigwa iliyoanza hivi karibuni, sasa asifiwe kwa lipi?
  Mimi ni mkazi wa maeneo hayo, nasema kulingana niliyvoona mwezi Feb 2011.
   
 9. z

  zamlock JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  ndo maana hata mimi nimemweleza ataje alichofanya atushabiki magamba hapa na ukizingatia hyo rangi nyeupe aifanyi kazi kwa hasara hata kidogo
   
 10. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  So ****ing what?
   
 11. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  acha ujinga basi
   
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Nilianzisha topic ya kuomba sisi wengine tuwe wachangiaji tu badala ya kuwa waanzisha thread zisizo na kichwa wala miguu!
   
 13. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kuna aina mbili za sifa:
  1. Sifa mzuri
  2. Sifa mbaya
  Mi naona labda anastaili sifa mbaya kutokana na kutopenda wengine waongoze kwenye jimbo la Gairo tangu miaka ya 2000 hivyo ni mpenda madaraka, mtoa rushwa na hana demokrasia
   
 14. Binti Magufuli

  Binti Magufuli JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 7,455
  Likes Received: 756
  Trophy Points: 280
  Dogo, ulichopaswa kufanya ni kujenga hoja ya nini kimewafanya mumpende huyo shabiby wenu, sio kusema tu hoyeeeee na kudai unampenda, ama sivyo sisi tutakuona mzandiki tu na usiye na hoja aka umefulia na hivyo hoja yako kukosa maana.
   
 15. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  acha upuuzi!
   
 16. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Huyu anaua tu dada zetu na watotio wetu kwa UKIMWI,
  yes i said it UKIMWI
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,308
  Likes Received: 19,458
  Trophy Points: 280
  kafanya nini? weka data hapa na uthibitisho,,,,tuambie ni vitu gani kavileta baada ya uchaguzi na vitu gani kaviboresha
   
 18. Binti Magufuli

  Binti Magufuli JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 7,455
  Likes Received: 756
  Trophy Points: 280
  Katumwa huyu mimi nimemshitukia. Nasikia kuna watu humu JF wamepewa moral and material support ili kuwasafisha wanamagamba( Source JF). Nimeona thread nyingine imeandikwa tu "shabiby hoyeeeeeee" na mtoa thread akaandika kuwa wanampenda shabiby bila maelezo yoyote ya ziada. Huwezi tu kusema anafaa bila kutueleza kwanini umeona anafaa na anastahili pongezi.
   
 19. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako LIGUNIKA,

  Mkuu kwanza naomba unijuze kazi za mbunge majibu yako yazingatie katiba ya JMT.
  Baada ya kuipitia katiba ya JMT nitaomba unitajie mambo aliyofanya ili na mimi nijumuike kumwaga sifa kwa Mheshimiwa Shabiby vinginevyo utakuwa unajidanganya wewe na wanavijiji wa Gairo.

  Nitajaribu kukusaidia kazi kuu ya mbunge ni kutunga sheria na kuisimamia serekali,ukitaka kumpongeza mbunge yoyote wa JMT lazima kwanza uyatazame maeneo hayo mawili makuu.

  Nianze na kipengele cha utungaji wa sheria.
  Wabunge wa upinzani wakiongozwa na kiongozi wa upinzani bunge Mheshimiwa Hamad na msaidizi wake Dr W Slaa [bunge la mwaka 2005 - 2010] walijitaidi kadri ya uwezo wao wote kupinga sheria mbovu na kandamizi zilizoletwa bungeni na serekali mara kadhaa walishindwa kwasababu ya uchache wa kambi ya upinzani bungeni.Wabunge wa CCM Mheshimiwa Shabiby akiwemo walikubali kupitisha sheria mbovu na kandamizi amabazo zimeligharimu taifa letu mabilioni ya fedha.Sifa unazojaribu kumpa Mheshimiwa Shabiby kwenye kipengele cha utungaji wa sheria hana kabisa labda kama unataka kuchangamsha jamvi.

  Kusimamia serekali.kwenye kipengele hiki Shabiby hayumo kabisa sina haja ya kutoa maelezo marefu kabisa.Wahusika wa kipengele hiki kwa uchache kabisa ni Dr W Slaa na Zitto Z Kabwe.

  Nakusihii mshauri Shabiby hajachelewa sana ana muda wa miaka minne ya kufanyakazi hana haja ya kutafuta njia ya mkato afanye kazi itaonekana tutampatia heshima yake.
   
 20. B

  Brown-Suga New Member

  #20
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nyie wengine tusikilizeni sisi tunao ijua gairo vizuri, mh ahmed shabiby anastahili sifa na tunampenda sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa amefanya mengi sana tu kwa wananchi wa gairo. kwanza kama mlikuwa hamjui Gairo sasa hivi ni wilaya! big step already! kiafya na kielimu gairo ipo juu sasa, kama mnabisha nendeni mtaniambia wenyewe...mbali na hayo mh ahmed shabiby amesawasaidia wananchi wengi sanaaa individually!!! na ameanza kufanya hivi even kabla hajawa mbunge! tunampenda sana na tutaendelea kumpenda hata akiacha ubunge kwasababu sisi wote tunamjua vizuri, tumetoka nae mbali na tunajua passion aliyonayo kwa ajili ya gairo! kwa kifupi AHMED SHABIBY IS THE BEST nyie wote mnaojaribu kumchafulia jina elimikeni bwana, mmejaribu kufanya hivyo mara ngapi lakini ndo kwanza anazidi kusonga mbeleeeee and so is Gairo!!!!!!! :love:
   
Loading...