Malisa Godlisten
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 201
- 1,534
Nimemsikia SACP Lazaro Mambosasa, (Kamanda wa kanda maalumu Dar) akieleza tukio la kuvamiwa Meja Jenerali Mstaafu Vincent Karyongo kwa risasi nyumbani kwake Tegeta, wakati akitoka bank (NBC Tangibovu).
Kamanda Mambosasa ameeleza kuwa wamenasa mawasiliano kati ya mfanyakazi mmoja wa NBC na mmoja wa waliofanya uhalifu huo. Kwamba kuna mfanyakazi wa NBC "aliuza ramani" kwa majambazi hao kwamba Meja Karyogo amedraw kiasi cha TZS 5M. Mfanyakazi huyo anashikiliwa na Polisi kwa sasa kwa ajili ya upelelezi.
Kwanza nalipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua ilizochukua hadi sasa kuhusu suala hilo.
Pili kwa kadri ya uelewa wangu kwenye banks ni marufuku matumizi ya simu. Si kwa Mteja akiwa ndani wala mfanyakazi. Sasa huyu mfanyakazi wa NBC aliyekamatwa aliwezaje kuwasiliana na hao wahalifu? Alificha simu kwa siri, au branch ya Tangibovu inaruhusu matumizi ya simu kwa wafanyakazi wakiwa kazini? Hapa napata shida kidogo kumuelewa Mambosasa.
Lakini ikiwa taarifa ya Mambosasa ni ya kweli kwamba walitrack mawasiliano ya huyo banker na kugundua anawasiliana na wahalifu, basi nadhani kuna haja ya mabank kujiridhisha na wasifu wa watu wanaowaajiri. Ni aibu kwa mfanyakazi wa bank kubwa kama NBC kushirikiana na majambazi kupanga uhalifu. Usalama wa pesa zetu uko wapi? Usalama wetu uko wapi?
Tatu; ikiwa taarifa ya Mambosasa ni kweli, basi nashauri NBC watoe statement ya kuomba radhi kwa mtumishi wao kuhusishwa na kashfa hii kubwa, otherwise this will turnish the reputation of the bank. Watu watajifeel insecured kuweka pesa zao NBC na kuamua kuzitoa kupeleka bank nyingine. Nani yuko tayari kuona siri zake za miamala ya fedha zikivujishwa? Nani yuko tayari kuvamiwa na majambazi akienda kutoa kiasi kikubwa cha pesa? NBC should make clear statement to apologize and clatify the matter. Vinginevyo wajiandae kupoteza wateja.
Mwisho, kwa kuwa polisi wamekiri "kutrack" mawasiliano ya huyo banker na kujua alikua anawasiliana na hao majambazi, ni kwanini "wasitrack" pia mawasiliano ya Bashite maana imedaiwa kwamba alikua anawasiliana na watu waliomshambulia Lissu? Hawaoni kuwa hii itasaidia upelelezi na kuwajua wahalifu waliomshambulia Lissu kwa haraka kama ilivyosaidia kuwajua wahalifu waliomshambulia Meja Karyogo?