Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 888
- 4,136
Mauaji yamezidi kuongezeka nchini. Matukio ya vifo vya utata vinavyofanywa na wanajamii pamoja na dola vimekuwa vingi. Mapuuza yamezidi kuwa mengi na Mamlaka za uchunguzi zimezidi kutoa ufafanuzi wenye utata kwenye matukio yanayofanywa na dola au wananchi.
Hakuna waziri anayekemea hali hii. Hakuna kiongozi wa dini aliyesimama adharani akasema polisi mmekosea na kuomba au kushauri uchunguzi ufanyike. Hakuna mwanaharakati aliyejitokeza kuonyesha kukerwa na hali hiyo.
Kinachotokea sasa, bila taarifa kuandikwa kwenye mitandao hakuna hatua inayochukuliwa. Na zikiandikwa zisipopata comments nyingi serikali nayo inapuuza.
Nichukue mfano wa kesi ya mwanamke aliyechomwa visu ishirini na tano huko Moshi ambaye amezikwa leo. Jaribu kusikiliza waombolezaji wanavyolalamikia jeshi la polisi then soma taarifa ya msemaji wa jeshi husika. Kuna utata mkubwa na uzembe ila hakuna anayekubali huo uzembe.
Ukimya wa vyombo vya dola sambamba na mawaziri wenye dhamana hauna afya kwa nchi. Mimi siyo mtabiri ila naona wazi upo uwezekano mkubwa ukimya wa mwenye nchi ukaja na tumbua ya kisiasa kutuliza upepo. Tujirekebishe.
Kadri mapuuza yanavyozidi kuathiri jamii kubwa ndivyo chuki inavyoongezeka. Kesho hii inakwenda kuwa agenda kwenye mitaa kwamba serikali imewapuuza wananchi. Uthibitisho utakuwa haya haya tunayoyapuuza leo na chama kitaathirika na chuki hii.
Watu wenye dhamana chukueni hatua.....haipendezi kusikia watu wanatamka adharani kwamba hakuna serikali