Kwanini masikini wanabaki hivyo?

Kwanini masikini wanabaki hivyo?

Mkuu shukran san uzi wako umenitoa tongo tongo asubuhi hii ngoja nikatafute tonge kwa juhudi na maarifa yote
 
Sifa ya masikini ni roho mbaya na kujadili kila kilichopo mbele yake. Umasikini mbaya ni umasikini wa fikra.

Lakini namba 12 hapo bado haipo clear, anachopata masikini anatakiwa afanye investment kwenye vitu vitakavyompa faida na kutoka kwenye faida hiyo ndio anaweza akatoa fungu kwa ajili ya shukrani mbele ya Mungu wake. Ila kama akipata 1000 then akasema hiyo 1000 aende akaiwekeze kwa Mungu akaitoe kanisani/msikitini kesho tena ataamka hana kitu akitegemea miujiza ya kupata 1000 nyingine
 
Mtoa mada , ulichosema ni kweli . shida je wanakuelewa? Watakubali? Hasa hasa sie akina - Weusi!
 
4)ukiwaambia wajaribu vitu vipya, watakwambia hamna uzoefu: umewahi kuona wapi hichi kitu kimefanikiwa? Nani amewahi kufaidika nacho?
Aisee hapa nimekuelewa wabongo ukiwaambia let's say idea yeyote ile mpya utasikia italipa, masoko vipi na bla bla nyingi.
 
They must try it again and again
 
Barikiwa Sana
5b668455aa11a6ac9d0bec91f4a15dfa.jpeg
08a9c0e7a56e5ec812ae9d00d07f8140.jpeg
b5fa392ba342d48288ccfcd7e12f093e.jpeg
 
Taking chances is risky but not taking chances at all is riskier.
 
Mimi nadhani kuna vitu vinatakiwa vianzie toka utotoni katika malezi,yaani unamjengea mtoto tabia ya kujiamini self confidence,

Mfano angalia wahindi jinsi wanavyowalea watoto wao,unakuta muhindi anamuandaa mtoto wake kuja kua mtafutaji,kuanzia malezi mpaka elimu,wahindi hupenda kuwachukua watoto wao kwenye biashara zao hasa madukani ili tu wawe na mazowea na kujifunza kuhusu utafutaji,

Ni ngumu sana kumbadilisha mtu ambaye ni matured tayari na hasa ikiwa yeye mwenyewe hayupo tayari kubadilika,

Better late than never.
 
Shukrani Mkuu
 
mkuu umeeleza vyema sana, kwa nyongeza ndogo, mtu hurithi umasikini pia hasa ka si makini, hii inatokana na maisha alokulia baada ya kuzaliwa na anaona kumbe hayo ndo maisha, hasa ka hajakulia sehemu na kupata changamoto toka kwa watu mbalimbali,

Ila tunakilasababu ya kujitahidi kwa nafasi zetu kufika sehemu nzuri kimaisha na kihali
 
Mtu mmoja aliwahi kusema, "ukichukua fedha zote ulimwenguni na ukizagawa sawa sawa kwa kila mmoja, baada ya mda hela zitawarudia wale walio kuwa nazo mara ya kwanza" Kwanini?

......."Maskini ni watumiaji wakati matajiri ni wawekezaji"......

Nioneshe mtu maskini, nitakuonyesha mtu anae pishana na fursa mara kwa mara.

Mtu anaeona changamoto ndani ya kila fursa badala ya kuona fursa ndani ya kila changamoto.

Kuwa KIJANA sio cheo, ni jukumu. Inamaanisha unapaswa kuwajibika kiuchumi Asubuhi, Mchana na Usiku.

Lazima uchukue maamuzi magumu ili upate matokeo makubwa.

Unapaswa kupanga na kuweka mikakati, lazima uthamini faida na fedha kidogo unayoipata. Lazima uwe makini na mwenye nia kama unataka kufanikiwa.

Watu wanaoshangaza kabisa hapa duniani ni WATU MASKINI.

UMASIKINI Ni kupishana na fursa kila wakati.

Angalia sababu hizi
1) ukiwapa bure, watahisi ni mtego.

2) ukiwaambia ni mradi mdogo wawekeze, watakwambia hauwezi ukaleta faida

3) ukiwambia waingie kuwekeza katika ukubwa, watakwambia sina hela

4)ukiwaambia wajaribu vitu vipya, watakwambia hamna uzoefu: umewahi kuona wapi hichi kitu kimefanikiwa? Nani amewahi kufaidika nacho?

5) Ukiwaambia ni biashara ya kawaida ya kila siku, watakwambia ni kazi ngumu sana hiyo

6) ukimwambia ni mpango biashara mpya, atakwambia mimi huwa siongeagi sana na watu alafu ni kwa miaka mingapi sasa huu mpango biashara umekuwepo?

7) ukimwambia afungue duka, atakwambia nitakosa uhuru ntashindwa kufanya mambo mengine.

8) ukimwambia afate mpango wa biashara yake kwa mwaka mmoja, atakwambia ni mda mrefu sana huo, siwezi subiri.

9) ukimuuliza ni nini anaweza kufanya, atakwambia "naweza kufanya chochote"

10) wanapenda kuwauliza marafiki zao, ambao ni kama wao juu ya mtazamo wao. Hata maandiko matakatifu yameeleza kuwa vipofu, kamwe hawaongozi vipofu wenzao.

11) wanafikiri zaidi ya mkufunzi wa chuo kikuu na wanafanya kidogo kuliko kipofu.

12)Akienda kanisani anasema hana kabisa sadaka lakini wakati huo huo anatoka na kununua maandalizi (ANAAMUA KU'INVEST CHOONI KULIKO KWENYE UFALME WA MUNGU)

Changamoto kubwa sana watu maskini walio nayo, ni kukosa kuchukua hatua

Wanafurahia kasehemu kasiko na mahangaiko. Wanakwea katika dimbwi la ulimwengu wao na ufahamu wao ....

NB;
kuna hatari katika kuchukua hatua, lakini ni hatari zaidi kutokuchukua hatua.. je Ni Bora kuchuka hatua badae usipofanikiwa ukajifunza kitu Katika maisha ya utaftaji? au ukaacha kuichukua hatua badae ukaanza kushangaa mafanikio ya wale waliochukua hatua? (utasikia huyu nilisoma nae secondary) "maneno ya wasiopenda kuchuka hatu"

Bora kuchukua hatua.
Hii ni moja ya nyuzi zisizopendwa sana hapa na sitashangaa ikifukiwa na mada za kijinga muda mchache ujao kwa kisingizio cha "nani anayetaka mambo ya kuumiza kichwa"
 
Back
Top Bottom