Kwanini masikini wanabaki hivyo?

Kwanini masikini wanabaki hivyo?

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
766
Reaction score
1,536
Mtu mmoja aliwahi kusema, "ukichukua fedha zote ulimwenguni na ukizagawa sawa sawa kwa kila mmoja, baada ya mda hela zitawarudia wale walio kuwa nazo mara ya kwanza" Kwanini?

......."Maskini ni watumiaji wakati matajiri ni wawekezaji"......

Nioneshe mtu maskini, nitakuonyesha mtu anae pishana na fursa mara kwa mara.

Mtu anaeona changamoto ndani ya kila fursa badala ya kuona fursa ndani ya kila changamoto.

Kuwa KIJANA sio cheo, ni jukumu. Inamaanisha unapaswa kuwajibika kiuchumi Asubuhi, Mchana na Usiku.

Lazima uchukue maamuzi magumu ili upate matokeo makubwa.

Unapaswa kupanga na kuweka mikakati, lazima uthamini faida na fedha kidogo unayoipata. Lazima uwe makini na mwenye nia kama unataka kufanikiwa.

Watu wanaoshangaza kabisa hapa duniani ni WATU MASKINI.

UMASIKINI Ni kupishana na fursa kila wakati.

Angalia sababu hizi
1) ukiwapa bure, watahisi ni mtego.

2) ukiwaambia ni mradi mdogo wawekeze, watakwambia hauwezi ukaleta faida

3) ukiwambia waingie kuwekeza katika ukubwa, watakwambia sina hela

4)ukiwaambia wajaribu vitu vipya, watakwambia hamna uzoefu: umewahi kuona wapi hichi kitu kimefanikiwa? Nani amewahi kufaidika nacho?

5) Ukiwaambia ni biashara ya kawaida ya kila siku, watakwambia ni kazi ngumu sana hiyo

6) ukimwambia ni mpango biashara mpya, atakwambia mimi huwa siongeagi sana na watu alafu ni kwa miaka mingapi sasa huu mpango biashara umekuwepo?

7) ukimwambia afungue duka, atakwambia nitakosa uhuru ntashindwa kufanya mambo mengine.

8) ukimwambia afate mpango wa biashara yake kwa mwaka mmoja, atakwambia ni mda mrefu sana huo, siwezi subiri.

9) ukimuuliza ni nini anaweza kufanya, atakwambia "naweza kufanya chochote"

10) wanapenda kuwauliza marafiki zao, ambao ni kama wao juu ya mtazamo wao. Hata maandiko matakatifu yameeleza kuwa vipofu, kamwe hawaongozi vipofu wenzao.

11) wanafikiri zaidi ya mkufunzi wa chuo kikuu na wanafanya kidogo kuliko kipofu.

12)Akienda kanisani anasema hana kabisa sadaka lakini wakati huo huo anatoka na kununua maandalizi (ANAAMUA KU'INVEST CHOONI KULIKO KWENYE UFALME WA MUNGU)

Changamoto kubwa sana watu maskini walio nayo, ni kukosa kuchukua hatua

Wanafurahia kasehemu kasiko na mahangaiko. Wanakwea katika dimbwi la ulimwengu wao na ufahamu wao ....

NB;
kuna hatari katika kuchukua hatua, lakini ni hatari zaidi kutokuchukua hatua.. je Ni Bora kuchuka hatua badae usipofanikiwa ukajifunza kitu Katika maisha ya utaftaji? au ukaacha kuichukua hatua badae ukaanza kushangaa mafanikio ya wale waliochukua hatua? (utasikia huyu nilisoma nae secondary) "maneno ya wasiopenda kuchuka hatu"

Bora kuchukua hatua.
 
Sasa kama wote tutakua matajiri nani atakae msaidia mwenzie?

Mfano hawa wanaofanya kazi za watu wanawasaidia mabosi wao na hao mabosi wanawasaidia watumishi wao kuwapa pesa, kwa hiyo huo ndiyo mzunguko wa maisha duniani na sidhani kama kuna nchi ambayo haina maskini kulingana na pato la nchi hiyo.
 
Ofcourse itakuwa ngumu wote kuwa Bourgeoise
 
Hizi ni nadharia, inaweza kuwa kweli au isiwe kweli.. kwa sababu hizo Pesa hazijawahi gawiwa!
 
Mtu mmoja aliwahi kusema, "ukichukua fedha zote ulimwenguni na ukizagawa sawa sawa kwa kila mmoja, baada ya mda hela zitawarudia wale walio kuwa nazo mara ya kwanza" Kwanini?
......."Maskini ni watumiaji wakati matajiri ni wawekezaji"......
Nioneshe mtu maskini, nitakuonyesha mtu anae pishana na fursa mara kwa mara.
Mtu anaeona changamoto ndani ya kila fursa badala ya kuona fursa ndani ya kila changamoto.
Kuwa KIJANA sio cheo, ni jukumu. Inamaanisha unapaswa kuwajibika kiuchumi Asubuhi, Mchana na Usiku.
Lazima uchukue maamuzi magumu ili upate matokeo makubwa.
Unapaswa kupanga na kuweka mikakati, lazima uthamini faida na fedha kidogo unayoipata. Lazima uwe makini na mwenye nia kama unataka kufanikiwa.
Watu wanaoshangaza kabisa hapa duniani ni WATU MASKINI.
UMASIKINI Ni kupishana na fursa kila wakati.
Angalia sababu hizi
1) ukiwapa bure, watahisi ni mtego.
2) ukiwaambia ni mradi mdogo wawekeze, watakwambia hauwezi ukaleta faida
3) ukiwambia waingie kuwekeza katika ukubwa, watakwambia sina hela
4)ukiwaambia wajaribu vitu vipya, watakwambia hamna uzoefu: umewahi kuona wapi hichi kitu kimefanikiwa? Nani amewahi kufaidika nacho?
5) Ukiwaambia ni biashara ya kawaida ya kila siku, watakwambia ni kazi ngumu sana hiyo
6) ukimwambia ni mpango biashara mpya, atakwambia mimi huwa siongeagi sana na watu alafu ni kwa miaka mingapi sasa huu mpango biashara umekuwepo?
7) ukimwambia afungue duka, atakwambia nitakosa uhuru ntashindwa kufanya mambo mengine.
8) ukimwambia afate mpango wa biashara yake kwa mwaka mmoja, atakwambia ni mda mrefu sana huo, siwezi subiri.
9) ukimuuliza ni nini anaweza kufanya, atakwambia "naweza kufanya chochote"
10) wanapenda kuwauliza marafiki zao, ambao ni kama wao juu ya mtazamo wao. Hata maandiko matakatifu yameeleza kuwa vipofu, kamwe hawaongozi vipofu wenzao.
11) wanafikiri zaidi ya mkufunzi wa chuo kikuu na wanafanya kidogo kuliko kipofu.
12)Akienda kanisani anasema hana kabisa sadaka lakini wakati huo huo anatoka na kununua maandalizi (ANAAMUA KU'INVEST CHOONI KULIKO KWENYE UFALME WA MUNGU)
Changamoto kubwa sana watu maskini walio nayo, ni kukosa kuchukua hatua
Wanafurahia kasehemu kasiko na mahangaiko. Wanakwea katika dimbwi la ulimwengu wao na ufahamu wao ....
NB;
kuna hatari katika kuchukua hatua, lakini ni hatari zaidi kutokuchukua hatua.. je Ni Bora kuchuka hatua badae usipofanikiwa ukajifunza kitu Katika maisha ya utaftaji? au ukaacha kuichukua hatua badae ukaanza kushangaa mafanikio ya wale waliochukua hatua? (utasikia huyu nilisoma nae secondary) "maneno ya

wasiopenda kuchuka hatu"
Bora kuchukua hatua.
Hata itakapofika mwisho wa ulimwengu, masikini watakuwepo na matajiri watakuwepo, naweza kusema ndio mpangilio wa maisha ya viumbe wote ulimwenguni, binadamu,wanyama na hata wadudu. na hata mazingira kuna sehemu kame na sehemu zenye rutuba, Tuangalie maji yanavyotiririka toka sehemu kame kabisa za milimani ambazo ndio zinauhitaji na kuelekea baharini ambako tayari kuna maji tele.
 
Mawazo yako tutayaheshimu
 
Back
Top Bottom