The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 10,959
- 13,425
Kuna kitu kinanishangaza. Natamani nijue sababu. Tangu aingie bi mkubwa, mashehe wengi wamejitokeza kuwa machawa na waimba kwaya kama wasanii walio wengi.
Je, tatizo ni njaa au uhaba wa maarifa?
Je, ni kwa vile rais ni mwenzao?
Je, huu siyo udini wa wazi kabisa?
Ina maana mashehe huwa hawapewi mishahara na maruprupu vya kutosha kiasi cha kujiamini na kujitegemea?
Huwa wanajituma au kutumwa?
Hivi, wanajua madhara ya wanachofanya?
Wanatoa somo gani kwa vijana?
Mbona shida za Tanzania hazijui dini au ni kwa vile ni wabinafsi na wasaka ngawira kama viongozi wa kikristo wa kujipachika?
Mie wallahi sielewe. Naomba wanangu mnipe elimu bure.
Shukrani sana.