Kwanini Marekani haikuingia vitani dhidi ya Bashar Al Asad

MZK

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
223
303
Nianze kwa kuwasalimia, nakuwatakia heri ya mwaka mpya Watanzania na Waafrika wote!

Mnamo januari 14,2011 aliyekuwa rais wa Tunisia bwana Zine El Abidine Ben Ali alipinduliwa kutokana na kile kilichojulikana kama maandamano ya wananchi kupinga ukosefu mkubwa wa ajira uliokuwa umepelekea muhitimu wa chuo kikuu kujiua kutokana na kuvunjiwa banda lake na vyombo vya usalama. Maandamano hayo badae yalikuja kujulikana kama Mabadiliko ya kisiasa katika ulimwengu wa kiarabu kwa kimombo the Arab Spring.

Baada ya Tunisia, Misri nayo ikakumbwa na balaa hili ambapo mwezi wa januari tarehe 25,2011 wananchi walijikusanya katika uwanja wa Tahrir na kupinga hari ngumu ya uchumi na uongozi mbovu wa bwana Hosni Mubarak na serikali yake chini ya chama cha NDP. Pamoja na kujaribu kuyadhibiti maandamano haya, chini ya makamanda wakuu wa jeshi wakiongozwa na Tantawi, Sisi n.k, Mubarak akapinduliwa mnamo tarehe 11.02.2011 na nafasi yake ikachukuliwa na Mohammed Morsi wa chama cha Muslim Brotherhoo ambaye naye alipinduliwa na jeshi nat nafasi hiyo kuchukuliwa na waziri wake wa Ulinzi bwana Abdel Fattah El Sisi ambaye mpaka Leo ni rais wa Misri.

Mapinduzi haya ya nchi mbili kwamaana ya Tunisia na Misri yalitoa mwanya kwa nchi za magharibi zikiongozwa na Marekani,Uingereza na Ufaransa; kutumia fursa hiyo kupandikiza kimbunga cha mapinduzi katika mataifat yaliyokuwa yamesalia kama Libya,Jordan,Bahrain,Yemen, na Syria. Huu ukiwa ni mkakati mahususi uliopangwa kwa ustadi mkubwa na wana mikakati wa Woshngton,Brussels,Paris,London n.k

Katika hali ya kushangaza sana, Libya chini ya Kiongozi mahiri kabisa na mkakamavu bwana Muamar Gaddafi mnamo februari 15,2011 nayo ikajikuta kwenye kanyampasila(wakati usioneneka) wa maandamano ya kushtukiza kuanzia Jijini Benghaz. Mwanzon Ghaddafi hakuwa na taarifa za kutosha juu ya kilichokuwa kinaendelea, lkn badae alikuja kuelewa huku akiwa amechelewa.

Maandamano hayo ya upinzani yakiwa na ajenda kuu ya Uhuru wa kujieleza,yalianikiza mpaka katika viunga vya miji ya Misrata,Tripoli na mingi ya magharibi. Ghaddafi aliamuru waandamanaji wote watiwe kabali. Mwanae Al Islam akiwa instructor mkuu,wakuu wa vikosi waliwapiga risasi na kuwaua waandamanji wengi kwa kutumia mpaka ndege na vifaru. Jambo hili lilipata nguvu baada ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kupitisha azimio(UN resolution) namba 1973 mnamo tarehe 19.03/2012 kuwa lazima NATO iingilie kati kusaidia raia wema waliokuwa wanauawa na vikosi maalum vya Ghaddafi.

NATO ikiongozwa na majeshi maalumu kutoka Marekani,Uingereza na Ufaransa ilianzisha mashambulizi makubwa sana dhidi ya vituo maalum vya jeshi la Libya. Italy ilikuwa imekataa hatua hiyo huku Urus ikawa haijaelewa vizuri mikakati ya magharibi.

Shambulizi la makombora 110 ya Tomahawk kutoka katika Meri za jeshi la Marekani na Uingereza yakiwa yamelenga maeneo muhimu ya jeshi la Libya huku ndege za Ufaransa chapa appach zikiwa zinayahujumu maeneo ya kambi za jeshi na kuvishambulia vifaru, ilipelekea mitambo aina SAM ya kudungulia ndege ya Libya kukosa nguvu na 9K33 Osa launchers kushindwa kurusha makombora dhidi ya jeshi la NATO lililokuwa na hamu kubwa ya kumuangamiza Gaddafi na chama chake cha Libyan Arab Jamairiya huku likiungwa mkono na waandamanji waliogeuka waasi wa Libya.

Opereisheni hii ya NATO ilopewa jina la Harmattan ilimmaliza nguvu mtukutu Gaddafi aliyekuwa ameombwa na marais Zuma wa Afrika ya kusini wa wakati huo na yule wa Chad kuwa wangempa hifadhi ya ukimbizi endapo angeikimbia nchi lakini akakataa huku akiwa analiamini jeshi lake lililogeuzwa kibogomo mbele ya jeshi hatari la NATO huku mataifa ya Afrika yakiwa yamejifungia nyuma ya nondo kubwa yakichungulia jinsi Gaddafi alivyokuwa anachachafulia na mbwa wakali wa kimagharibi.

Mpaka anaamua kukimbilia Sirte,Gaddafi alipoteza nguvu zote baada ya kuuawa kwa walinzi wake wa kike na mpaka tarehe 31.102011 mauti yanamfika, alikuwa anajaribu kuikimbia nchi kuelekea Chad lakini satellite ikamuona katika msafara wa pick up na ndege ya kijeshi ya Ufaransa ikaushambulia msafara wake naye akajificha mtaroni hatimaye akauawa akiwa na mkuu wake wa majeshi.

Nchi za Magharibi zilianza kuuona mwanga mpya wa kuzing'oa meno tawala korofi za kiarabu; ndo zikaanzisha mkakati wa kumfinyanga bwana Bashar Al Asad.

Maandamano yaliyoanikiza hasa kuanzia julai 28,2011;;;; yalionekana kabisa yangemtoa madarakani bwana Asad Mshia na kiongozi wa chama cha Arab Socialist Ba'ath. Akiwa katika ngazi ya U-field Marshal na daktari wa ngazi ya juu wa jeshi LA Republican guard, Asad aliye ingia madarakan mwaka 2000. Aliamua kuliamuru jeshi kuingilia maandamano ya jimbo la Idribu lakin akashindwa kwani kila jimbo lilianzisha maandamano makali yakumpinga,kuanzia Holmes,Aleppo,Deir er Zur,mpaka mji mkuu Damascus.

Ikiwa ni nchi iliyokuwa na Kemikali na silaha nyingine za sumu na yenye mkataba wa ulinzi na Urus tokea kwa baba yake bwana Hafez Al Asad 1971. Syria ilijua fika kuwa Mataifa ya magharibi yangeingia haraka sana, jeshi lake likajikuta linapigana vita ngumu sana yenye watu mchanganyiko.

Marekani ya Obama na Ujerumani ya Markel hazikuona umuhimu wa kuingiza jeshi,bali Ufaransa Na Uingereza zilikuwa na masilahi mapana kuuangusha utawala huu. Marekani ikawa inasita lakini kwa kuombwa na Saudi Arabia na Uturuki Marekani na mataifa ya kisuni,yakaanzisha kikundi cha ajabu cha ISIS. Kundi hili lilijipa jukumu la kuanzisha taifa huru la kiislam kumbe ilikuwa mbinu ya kutaka uungwaji mkono wa haraka. Kundi hili likajibadilisha majina kutoka ISIS na kuwa ISIL badae IS. Cha ajabu likapata wafuasi wengi mpaka kuyaua makundi kama Alqaeda, Nusra fronts, na Taliban.

Kundi hili liliasisiwa Iraq na kuanzisha uasi mwaka 2014 likapigana na serikali cha ajabu likateka miji yote ya kaskazin,mpaka Mosul,Tikrit na visima kibao vya mafuta. Marekani ikawa inasitasita, rais Malik akaomba msaada Urus wa ndege,hapo ndo Marekani ikaamua kuingia vitani dhidi ya IS ndani ya Iraq.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wakati huo katika baraza la senate Marekani bwana John MaCcain akasema hivi 'Magaidi wa IS wanao kimbia vita Iraq lazima watakimbilia Syria hivyo nijukumu la Marekani kuwafata popote watakapo kimbilia. Kweli ikasemekana magaidi wa IS wamejikusanya katika mji wa Ali Raqqa, Mara Deir Azourr,Mara Idribu, Mara wako Aleppo, n.k waasi waliokuwa wanampinga Asad wale wa Syrian Democratic Forces(SDF) wakapotea Mara wakaibuka Wakurdi nao wanataka kuunda taifa lao, Mara kundi la alsham likaibuka,Mara nusra fronts. Vita ikamuwia ngumu Asad.

Akiwa ameelemewa na 3/4 ya nchi yake kuwa imechukuliwa, Marekani na nchi za magharibi zilijua fika jamaa anaondoka. Mnamo tarehe 30.09.2015 Urus ikaanzisha mashambulizi makubwa na kushangaza kabisa mpaka dunia iliduwaa baada kujenga kambi ya siri ya Kheimim katika mji wa pwani wa Latakia ndani ya Syria. Obama akiwa haelewi kipi kinaendelea akamuita Putin mjinga anayeota ndoto za mchana. 'Putin ni kama mwanafunzi anayekaa nyuma ya darasa hajui kipi kinaendelea mbele'

Urus ilitumia nguvu nyingine ikiwemo mashambulizi ya S-24,35 na kuyahujumu maeneo ya chini ya ardhi ya magaidi yaliyofichwa silaha kutokea bahari ya Medterannean na Caspian. Ndege za T-90/160 bomber kwamara ya kwanza zikawa zinawahujumu waasi waliokuwa na kila aina ya silaha. Neno gaidi likapata tafsiri tofauti kati ya Urus na Marekani.

Uingereza na Ufaransa zikitumia kila mbinu huku zikijishambulia kwao afu wanasingizia ni magaidi wa IS walioko Syria wakawa wanafanya hujuma kubwa ndani ya Syria. Wakawa hawana tena ujanja. Urus ya Putin na Shoigu na Lavrov ikiwa inajua inajua imejitwisha zigo, ilijikuta katika mbinu kali ya magharibi baada ya kusemenekana kuwa Syria imetumia silaha za sumu. Putin akashupaa na kura kibao za turufu angalau Mara moja moja ikiungwa mkono na China. Wakawa wanataka uchunguzi huru...Marekani na Ulaya wakakataa wakasema Urus ingeharibu ushahidi.

Ndo Putin akaomba yeye na nchi yake wataziondoa silaha zote za sumu kutoka Syria na kuziteketeza hivyo shirika la atomiki likaanza zoezi la kuondoa silaha hizo kutoka Syria. Hapa ndo Obama alizidiwa ujanja na Putin, matokeo yake silaha nyingi zikahamishwa kijanja na kufichwa kusikojulikana hivyo nchi za magharibi zikabaki hazijui zifanye nn wangejua zilipo washapashambuli zamani.

Ndege ya Su-24 ya Urus ikadunguliwa na Uturuki hili kuchochea Urus ipaniki iivamie kijeshi Uturuki na kuharibu mambo kwani Uturuki IMO katika jumuiya ya NATO; Putin hakujibu. Israel akawa inafanya mshambuli holela Putin akawazuia Syria na Iran kutokujibu maana wangetifua moto usiyo mithilika kwan magharibi wangeingia kwa kigezo cha kumlinda Israel.
Mwishowe Urus ikakumbana na Marekani kufanya ujanja na kutaka kuingia vitani dhidi ya syria kisa inatumia silaha za sumu lkn Urus Ikawa inapisha mashambulizi ya Marekani ndani ya Syria mfano ya uwanja wa All shyrat lakini yenyewe haijibu dawa kufyeka IS.

Mwisho wa siku Putin akaizunguka Marekani kwa kuwaletea Trump kibaraka na mtu asiye aminika kabisa katika utawala wa aina yake yani Trump na Putin ni marafiki mno. Katika hali ya kushangaza Trump kaamuru kuondolewa kwa majeshi ya Marekani kutoka Syria jambo linalo ashiria kushindwa kwa Marekani dhidi ya Asad alielindwa na Putin.

Putin katumia ghalama kubwa kulinda mkataba wa ulinzi kwa Syria kwa sababu Qatar inategemewa na Ulaya kupata gesi ya bei nafuu. So, akipigwa Syria inakuwa rais kujenga mabomba kuelekea Ulaya yakitokea Qatar na kupekeka gesi huko. Jambo litakalo iangusha Urus kiuchumi. Mwishowe tunaona ujenzi mkubwa wa Bomba la gesi la Nod stream 2 la Urus kupitia chini ya bahati ya Uturuki kuelekea ujerumani na Ulaya kwa ujumla. Hii ni kuziba mwanya wa biashara ya gesi unaoweza kuingiliwa na marekani au hata Qatar.

Dunia ya sasa inaongozwa kwa akili nyingi. Karibu tujadili;

Na;
Kamugisha.
 
KWA KWELI DUNIA INAONGOZWA KWA AKILI KUBWA SANA BILA KUJALI SUALA LA UTU. SISI TU NDO WATOTO WA MUNGU. VIJANA WETU WANAKUFA KONGO BILA YA KUWA NA MASLAHI MAPANA NA YA KUDUMU.
 
Safi! Hii vita ya Syria ni kama inaelekea kumalizika na mshindi kama vile anafahamika japo unaweza usiwe Ushindi wa moja kwa moja (maridhiano ya kisiasa yakafuata badaae).
 
Ha ha haa uchambuzi mzuri sana.Putin ni kama mwanafunzi aliyekaa nje ya darasa ambae hajui ndani kinafundishwa nini,maneno ya obama.
Putin alikua anasoma mchezo,
hatimae kwa bahati tu kaonesha speriority ya Urusi,
Ha ha haa,inawezekana labda Warusi walitaka kuijaribu ile fomula yao ya Vita kuu ya pili ya dunia,ya kusubiri mpaka izidiwe ndio ije ianze vita ya ukombozi.maana nasikiaga Hitler alikaribia kidogo tu kuipata Moscow,hapo ndipo RED Army wakaanza shughuli ya kuikomboa mji, mmoja baada ya mwingine hatimae Hitler akatimua mbio.Nadhani huenda Putin alitaka US,UK na FR wakisaidiwa na ISIS waichukue miji yote ibaki miwili tu yaani Damascus na Allepo ili watumie ile fomula yao iliyotumika WWII,ha ha haa.Natania tu.
 
Kwani US anaogopa kuchapana na Urusi? mbona US ni World Super Power?wakati russia ni regional super power? hebu nifafanulie kidogo
kiufupi ni kuwa urusi tayari yupo juu kijeshi zaidi ya Us kinachombeba usa now ni propaganda tu

hakuna asiyejua kuwa vita ya syria ni nato vs urusi akisaidiana na iran na upande unaoelekea kushinda unajulikana tayari kwa lugha nyepesi ni kuwa nato wamechapwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nianze kwa kuwasalimia, nakuwatakia heri ya mwaka mpya Watanzania na Waafrika wote!

Mnamo januari 14,2011 aliyekuwa rais wa Tunisia bwana Zine El Abidine Ben Ali alipinduliwa kutokana na kile kilichojulikana kama maandamano ya wananchi kupinga ukosefu mkubwa wa ajira uliokuwa umepelekea muhitimu wa chuo kikuu kujiua kutokana na kuvunjiwa banda lake na vyombo vya usalama. Maandamano hayo badae yalikuja kujulikana kama Mabadiliko ya kisiasa katika ulimwengu wa kiarabu kwa kimombo the Arab Spring.

Baada ya Tunisia, Misri nayo ikakumbwa na balaa hili ambapo mwezi wa januari tarehe 25,2011 wananchi walijikusanya katika uwanja wa Tahrir na kupinga hari ngumu ya uchumi na uongozi mbovu wa bwana Hosni Mubarak na serikali yake chini ya chama cha NDP. Pamoja na kujaribu kuyadhibiti maandamano haya, chini ya makamanda wakuu wa jeshi wakiongozwa na Tantawi, Sisi n.k, Mubarak akapinduliwa mnamo tarehe 11.02.2011 na nafasi yake ikachukuliwa na Mohammed Morsi wa chama cha Muslim Brotherhoo ambaye naye alipinduliwa na jeshi nat nafasi hiyo kuchukuliwa na waziri wake wa Ulinzi bwana Abdel Fattah El Sisi ambaye mpaka Leo ni rais wa Misri.

Mapinduzi haya ya nchi mbili kwamaana ya Tunisia na Misri yalitoa mwanya kwa nchi za magharibi zikiongozwa na Marekani,Uingereza na Ufaransa; kutumia fursa hiyo kupandikiza kimbunga cha mapinduzi katika mataifat yaliyokuwa yamesalia kama Libya,Jordan,Bahrain,Yemen, na Syria. Huu ukiwa ni mkakati mahususi uliopangwa kwa ustadi mkubwa na wana mikakati wa Woshngton,Brussels,Paris,London n.k

Katika hali ya kushangaza sana, Libya chini ya Kiongozi mahiri kabisa na mkakamavu bwana Muamar Gaddafi mnamo februari 15,2011 nayo ikajikuta kwenye kanyampasila(wakati usioneneka) wa maandamano ya kushtukiza kuanzia Jijini Benghaz. Mwanzon Ghaddafi hakuwa na taarifa za kutosha juu ya kilichokuwa kinaendelea, lkn badae alikuja kuelewa huku akiwa amechelewa.

Maandamano hayo ya upinzani yakiwa na ajenda kuu ya Uhuru wa kujieleza,yalianikiza mpaka katika viunga vya miji ya Misrata,Tripoli na mingi ya magharibi. Ghaddafi aliamuru waandamanaji wote watiwe kabali. Mwanae Al Islam akiwa instructor mkuu,wakuu wa vikosi waliwapiga risasi na kuwaua waandamanji wengi kwa kutumia mpaka ndege na vifaru. Jambo hili lilipata nguvu baada ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kupitisha azimio(UN resolution) namba 1973 mnamo tarehe 19.03/2012 kuwa lazima NATO iingilie kati kusaidia raia wema waliokuwa wanauawa na vikosi maalum vya Ghaddafi.

NATO ikiongozwa na majeshi maalumu kutoka Marekani,Uingereza na Ufaransa ilianzisha mashambulizi makubwa sana dhidi ya vituo maalum vya jeshi la Libya. Italy ilikuwa imekataa hatua hiyo huku Urus ikawa haijaelewa vizuri mikakati ya magharibi.

Shambulizi la makombora 110 ya Tomahawk kutoka katika Meri za jeshi la Marekani na Uingereza yakiwa yamelenga maeneo muhimu ya jeshi la Libya huku ndege za Ufaransa chapa appach zikiwa zinayahujumu maeneo ya kambi za jeshi na kuvishambulia vifaru, ilipelekea mitambo aina SAM ya kudungulia ndege ya Libya kukosa nguvu na 9K33 Osa launchers kushindwa kurusha makombora dhidi ya jeshi la NATO lililokuwa na hamu kubwa ya kumuangamiza Gaddafi na chama chake cha Libyan Arab Jamairiya huku likiungwa mkono na waandamanji waliogeuka waasi wa Libya.

Opereisheni hii ya NATO ilopewa jina la Harmattan ilimmaliza nguvu mtukutu Gaddafi aliyekuwa ameombwa na marais Zuma wa Afrika ya kusini wa wakati huo na yule wa Chad kuwa wangempa hifadhi ya ukimbizi endapo angeikimbia nchi lakini akakataa huku akiwa analiamini jeshi lake lililogeuzwa kibogomo mbele ya jeshi hatari la NATO huku mataifa ya Afrika yakiwa yamejifungia nyuma ya nondo kubwa yakichungulia jinsi Gaddafi alivyokuwa anachachafulia na mbwa wakali wa kimagharibi.

Mpaka anaamua kukimbilia Sirte,Gaddafi alipoteza nguvu zote baada ya kuuawa kwa walinzi wake wa kike na mpaka tarehe 31.102011 mauti yanamfika, alikuwa anajaribu kuikimbia nchi kuelekea Chad lakini satellite ikamuona katika msafara wa pick up na ndege ya kijeshi ya Ufaransa ikaushambulia msafara wake naye akajificha mtaroni hatimaye akauawa akiwa na mkuu wake wa majeshi.

Nchi za Magharibi zilianza kuuona mwanga mpya wa kuzing'oa meno tawala korofi za kiarabu; ndo zikaanzisha mkakati wa kumfinyanga bwana Bashar Al Asad.

Maandamano yaliyoanikiza hasa kuanzia julai 28,2011;;;; yalionekana kabisa yangemtoa madarakani bwana Asad Mshia na kiongozi wa chama cha Arab Socialist Ba'ath. Akiwa katika ngazi ya U-field Marshal na daktari wa ngazi ya juu wa jeshi LA Republican guard, Asad aliye ingia madarakan mwaka 2000. Aliamua kuliamuru jeshi kuingilia maandamano ya jimbo la Idribu lakin akashindwa kwani kila jimbo lilianzisha maandamano makali yakumpinga,kuanzia Holmes,Aleppo,Deir er Zur,mpaka mji mkuu Damascus.

Ikiwa ni nchi iliyokuwa na Kemikali na silaha nyingine za sumu na yenye mkataba wa ulinzi na Urus tokea kwa baba yake bwana Hafez Al Asad 1971. Syria ilijua fika kuwa Mataifa ya magharibi yangeingia haraka sana, jeshi lake likajikuta linapigana vita ngumu sana yenye watu mchanganyiko.

Marekani ya Obama na Ujerumani ya Markel hazikuona umuhimu wa kuingiza jeshi,bali Ufaransa Na Uingereza zilikuwa na masilahi mapana kuuangusha utawala huu. Marekani ikawa inasita lakini kwa kuombwa na Saudi Arabia na Uturuki Marekani na mataifa ya kisuni,yakaanzisha kikundi cha ajabu cha ISIS. Kundi hili lilijipa jukumu la kuanzisha taifa huru la kiislam kumbe ilikuwa mbinu ya kutaka uungwaji mkono wa haraka. Kundi hili likajibadilisha majina kutoka ISIS na kuwa ISIL badae IS. Cha ajabu likapata wafuasi wengi mpaka kuyaua makundi kama Alqaeda, Nusra fronts, na Taliban.

Kundi hili liliasisiwa Iraq na kuanzisha uasi mwaka 2014 likapigana na serikali cha ajabu likateka miji yote ya kaskazin,mpaka Mosul,Tikrit na visima kibao vya mafuta. Marekani ikawa inasitasita, rais Malik akaomba msaada Urus wa ndege,hapo ndo Marekani ikaamua kuingia vitani dhidi ya IS ndani ya Iraq.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wakati huo katika baraza la senate Marekani bwana John MaCcain akasema hivi 'Magaidi wa IS wanao kimbia vita Iraq lazima watakimbilia Syria hivyo nijukumu la Marekani kuwafata popote watakapo kimbilia. Kweli ikasemekana magaidi wa IS wamejikusanya katika mji wa Ali Raqqa, Mara Deir Azourr,Mara Idribu, Mara wako Aleppo, n.k waasi waliokuwa wanampinga Asad wale wa Syrian Democratic Forces(SDF) wakapotea Mara wakaibuka Wakurdi nao wanataka kuunda taifa lao, Mara kundi la alsham likaibuka,Mara nusra fronts. Vita ikamuwia ngumu Asad.

Akiwa ameelemewa na 3/4 ya nchi yake kuwa imechukuliwa, Marekani na nchi za magharibi zilijua fika jamaa anaondoka. Mnamo tarehe 30.09.2015 Urus ikaanzisha mashambulizi makubwa na kushangaza kabisa mpaka dunia iliduwaa baada kujenga kambi ya siri ya Kheimim katika mji wa pwani wa Latakia ndani ya Syria. Obama akiwa haelewi kipi kinaendelea akamuita Putin mjinga anayeota ndoto za mchana. 'Putin ni kama mwanafunzi anayekaa nyuma ya darasa hajui kipi kinaendelea mbele'

Urus ilitumia nguvu nyingine ikiwemo mashambulizi ya S-24,35 na kuyahujumu maeneo ya chini ya ardhi ya magaidi yaliyofichwa silaha kutokea bahari ya Medterannean na Caspian. Ndege za T-90/160 bomber kwamara ya kwanza zikawa zinawahujumu waasi waliokuwa na kila aina ya silaha. Neno gaidi likapata tafsiri tofauti kati ya Urus na Marekani.

Uingereza na Ufaransa zikitumia kila mbinu huku zikijishambulia kwao afu wanasingizia ni magaidi wa IS walioko Syria wakawa wanafanya hujuma kubwa ndani ya Syria. Wakawa hawana tena ujanja. Urus ya Putin na Shoigu na Lavrov ikiwa inajua inajua imejitwisha zigo, ilijikuta katika mbinu kali ya magharibi baada ya kusemenekana kuwa Syria imetumia silaha za sumu. Putin akashupaa na kura kibao za turufu angalau Mara moja moja ikiungwa mkono na China. Wakawa wanataka uchunguzi huru...Marekani na Ulaya wakakataa wakasema Urus ingeharibu ushahidi.

Ndo Putin akaomba yeye na nchi yake wataziondoa silaha zote za sumu kutoka Syria na kuziteketeza hivyo shirika la atomiki likaanza zoezi la kuondoa silaha hizo kutoka Syria. Hapa ndo Obama alizidiwa ujanja na Putin, matokeo yake silaha nyingi zikahamishwa kijanja na kufichwa kusikojulikana hivyo nchi za magharibi zikabaki hazijui zifanye nn wangejua zilipo washapashambuli zamani.

Ndege ya Su-24 ya Urus ikadunguliwa na Uturuki hili kuchochea Urus ipaniki iivamie kijeshi Uturuki na kuharibu mambo kwani Uturuki IMO katika jumuiya ya NATO; Putin hakujibu. Israel akawa inafanya mshambuli holela Putin akawazuia Syria na Iran kutokujibu maana wangetifua moto usiyo mithilika kwan magharibi wangeingia kwa kigezo cha kumlinda Israel.
Mwishowe Urus ikakumbana na Marekani kufanya ujanja na kutaka kuingia vitani dhidi ya syria kisa inatumia silaha za sumu lkn Urus Ikawa inapisha mashambulizi ya Marekani ndani ya Syria mfano ya uwanja wa All shyrat lakini yenyewe haijibu dawa kufyeka IS.

Mwisho wa siku Putin akaizunguka Marekani kwa kuwaletea Trump kibaraka na mtu asiye aminika kabisa katika utawala wa aina yake yani Trump na Putin ni marafiki mno. Katika hali ya kushangaza Trump kaamuru kuondolewa kwa majeshi ya Marekani kutoka Syria jambo linalo ashiria kushindwa kwa Marekani dhidi ya Asad alielindwa na Putin.

Putin katumia ghalama kubwa kulinda mkataba wa ulinzi kwa Syria kwa sababu Qatar inategemewa na Ulaya kupata gesi ya bei nafuu. So, akipigwa Syria inakuwa rais kujenga mabomba kuelekea Ulaya yakitokea Qatar na kupekeka gesi huko. Jambo litakalo iangusha Urus kiuchumi. Mwishowe tunaona ujenzi mkubwa wa Bomba la gesi la Nod stream 2 la Urus kupitia chini ya bahati ya Uturuki kuelekea ujerumani na Ulaya kwa ujumla. Hii ni kuziba mwanya wa biashara ya gesi unaoweza kuingiliwa na marekani au hata Qatar.

Dunia ya sasa inaongozwa kwa akili nyingi. Karibu tujadili;

Na;
Kamugisha.
Wewe ni Jembe Balaaa,I salute you
 
kiufupi ni kuwa urusi tayari yupo juu kijeshi zaidi ya Us kinachombeba usa now ni propaganda tu

hakuna asiyejua kuwa vita ya syria ni nato vs urusi akisaidiana na iran na upande unaoelekea kushinda unajulikana tayari kwa lugha nyepesi ni kuwa nato wamechapwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ha ha haa,nato hawajachapwa.hata hivyo mie naona kama ma marekani hayamuogopi mrusi ila pengine yanaangalia kuna faida gani kupigana na urusi kwa sasa,kisa ni kuwatetea waasi wa syria,ndio yapoteze rasilimali na rasilimaliwatu wao.?
 
vita hiyo ni usa alikuwa anataka kuangusha uchumi wa urusi lkn assad akaweka kauzibe

syria na urusi wanamkataba wa ulinzi lkn mpaka sasa urusi ndie anaetumia pesa yake kuendesha hyo vita maana anajua mchongo wote kuwa target ni yeye

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unataka kujua kuwa warusi ni noma basi angalia ile vita ya kugombea jimbo la Aleppo ndo utajua warusi ni noma.waasi walikuwa wanajificha kwenye maghorofa,warusi wakija walikuwa wanangusha ghorofa zima mpaka sisimizi anafia humo humo ndani ya jengo

Ila vita muda mwingine uwa ni vichekesho sana,kwanzo waasi walikuwa wanashambulia tu mwanzo mwisho huku Assad kazi yake ilikuwa ni kuzuia mashambulizi.lakini baadae mambo yakabadilika Assad akawa anashambulia huku waasi wakawa wanazuia mashambulizi,sasa ivi Waasi wamebanana kwenye mkoa wa Idlib.inamaana Assad akiamua kuchukua Idlib basi itakuwa ndo mwisho wa waasi wa syria

Idlib ni pazito that why wanapavutia kasi na lazima wapachukue kwa usalama zaid

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wajuzi wa mambo ya migogoro leteni uchambuzi uzi umekuwa mtamu kishenzi..!!!
 
Back
Top Bottom