Kwanini mara nyingi pesa hutumika kutoa pole kwa mfiwa au wafiwa?

6321

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
649
1,116
Habari za asubuhi!

Nimeona mara nyingi mtu akipatwa na msiba basi ndugu, jamaa na marafiki hujichangisha pesa(rambirambi) kwa ajili ya mkono wa pole kwa mfiwa.

Je, kuna ulazima wowote wa kutumia pesa kama mkono wa pole?
 
Pesa ni kitu rahisi kubadilisha na kupata kile ambacho mhitaji anahitaji.Huwezi kubaini mara moja mfiwa anahitaji Nini kwa wakati ule hivyo ukitoa pesa itamsaidia yeye au wahusika kununua mahitaji yanayohitajika.Kwetu vijijini kukitokea msiba mtu atabeba alichonacho.Unga,maharage, pombe,kuku ,mboga za majani chochote ambacho anajua kitahitajika pale msibani ili mfiwa asihangaike kufikiria atawapa Nini watu wanaokuja kuomboleza pamoja naye.
 
Habari za asubuhi!

Nimeona mara nyingi mtu akipatwa na msiba basi ndugu, jamaa na marafiki hujichangisha pesa(rambirambi) kwa ajili ya mkono wa pole kwa mfiwa.

Je, kuna ulazima wowote wa kutumia pesa kama mkono wa pole?
Pale msibani hujaona watu wakila na wakinywa? Ulitaka wale pesa ya Nani?
Gharama za mazishi je?
Wewe Ni mkenya?
 
Ukienda Mwakaleli kwa kina Bujibuji kule ni vitu zaidi, sado ya mahindi, kuni, maharage, ndizi, mafuta ya kupikia, chumvi, sukari n.k.
Wafiwa wanakaa ndani nje mambo yanaendelea.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Mkuu ukifiwa unijiulishe nikuletee kitabu cha rich Dad poor dad Kama rambi rambi yangu
 
Habari za asubuhi!

Nimeona mara nyingi mtu akipatwa na msiba basi ndugu, jamaa na marafiki hujichangisha pesa(rambirambi) kwa ajili ya mkono wa pole kwa mfiwa.

Je, kuna ulazima wowote wa kutumia pesa kama mkono wa pole?
Because it is the main medium of exchange and measure of value.
 
Back
Top Bottom