SOCIOLOGISTTZ
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 2,615
- 929
Mama wakwe wengi kutoka makabila mengi kama siyo yote hapa Tanzania wana tabia ya kuangalia watoto wachanga wanapozaliwa viungo vyake vya mwili kama kucha, vidole, miguu, mikono nk, Lakini huwa wanaangalia zaidi kucha na vidole vya miguu na mikono kuliko viungo vingine. Mama wakwe hawa ni wamama wa mume wa mtu. Nilijaribu kuwauliza baadhi yao lkn hawakunipa majibu ila wanasifia tu mtoto ni mzuri, mwenye kujua siri hii tafadhali atujuze ili tuelimike wote, Asante