Kwanini Malima kwa Obama?

Kwanini Malima kwa Obama?

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
JUMAPILI, JULAI 07, 2013 05:35 NA EVANS MAGEGE

NAIBU Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima, ameanza kuangaliwa kwa jicho tofauti, kutokana na kuwa kiongozi pekee mwenye wadhifa wa chini wa uwaziri kuonekana akiwa mstari wa mbele wa viongozi wa serikali wakati wa mapokezi ya Rais wa Marekani, Barack Obama, katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Jumatatu iliyopita.

Hatua ya Malima kuonekana katika jopo hilo lililowajumuisha viongozi wachache wa serikali imeacha maswali, huku baadhi ya watu wakianza kuhoji kwa nini awe yeye, tena Naibu Waziri na wasiw, mawaziri wengine wakubwa wanaoshikilia Wizara nyeti au Waziri wake, Christopher Chiza.

Wakati wa mapokezi ya Obama hadi kuondoka kwake nchini Julai 2, mwaka huu, ni Malima pekee ambaye ni Naibu Waziri aliyejumuika na viongozi wengine wachache ambao wengine si wa hadhi yake, kama Rais wa Zanzibar, Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mkuu wa Majeshi, David Mwamunyange.

Tofauti na Malima, Kiongozi kama Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe hana mjadala kwa sababu suala la ujio wa Obama linaratibiwa na wizara yake.

Viongozi wengine waliokuwepo katika mapokezi hayo ni kwa sababu ugeni huo ulihusu maeneo yao ya kazi, kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Ma------.

Wafuatiliaji wa mambo na masuala ya kisiasa, wameelezea kuonekana huko kwa Malima katika mapokezi hayo kumeacha tafsiri pana, wengine wakidhani kwamba huenda Malima ana umuhimu mwingine tofauti usiofanana na hadhi yake ya Unaibu Waziri katika serikali ya Rais Kikwete.

Wanaosema hivyo wanakumbuka jinsi alivyosalimika kubaki nje ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, yaliyofanywa na Rais Jakaya Kikwete, Mei, 2012, kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma, ambazo pia ziliigusa Wizara ya Nishati na Madini, ambayo Malima alikuwa Naibu wake.

Waziri wake, ambaye alikuwa William Ngeleja, alikuwa miongoni mwa mawaziri watano waliotupwa nje ya baraza hilo, wakiwemo pia Manaibu Mawaziri wengine wawili.

Hatua hiyo ilitanguliwa na tishio la wabunge kutaka kumng'oa Waziri Mkuu, Pinda, kwa kura ya kutokuwa na imani naye bungeni, baada ya ripoti iliyotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kuwatia hatiani mawaziri kwa utumiaji mbaya wa fedha za umma.

Hata hivyo katika mabadiliko aliyoyatangaza Rais Kikwete Mei 4, 2012, Malima alipelekwa kwenye Wizara ya Kilimo na Chakula, chini ya Waziri wake, Christopher Chiza.

Wizara nyingine zilizoshutumiwa kwa ubadhirifu, kama Wizara ya Afya, Fedha na ile ya Usafirishaji, waliondolewa mawaziri pamoja na manaibu wao, isipokuwa Wizara ya Fedha, aliondolewa naibu waziri mmoja, huku mwingine akihamishwa wizara.

Sababu za Malima pamoja na wengine kubaki ndani ya Baraza la Mawaziri hazikujulikana, ingawa hilo nalo lilizua maswali kutoka kwa wachambuzi na wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa.

Kuhusu hili la sasa la kuonekana kuwa mstari wa mbele katika mapokezi ya Rais Obama, limetolewa ufafanuzi na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mkumbwa Ali, akisema kuwa si Malima tu, bali hata mawaziri wengine, kama Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki, Waziri wa Viwanda, Abdallah Kigoda, Waziri wa Fedha, William Mgimwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, wote walikuwa katika jopo la viongozi wa serikali kwenye mapokezi hayo, lakini katika maeneo tofauti.

Hata hivyo, pamoja na orodha hiyo, Malima bado anabaki kuwa Naibu Waziri pekee aliyekuwemo kwenye jopo la viongozi wa serikali walioteuliwa kwenye mapokezi.

Kwa mujibu wa Mkumbwa, jopo hilo la mawaziri liligawanywa katika makundi mawili, ambapo wengine walitakiwa kuwahi Ikulu kwa ajili ya kumpokea Obama, ambaye mara baada ya kuwasili nchini alielekea huko.

Gazeti hili lilizungumza na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, ambaye alisema kuwa katika mapokezi hayo hakuwepo, hivyo ilibidi awakilishwe na Naibu wake, ambaye ni Malima.

Waziri Chiza alisema alikwenda Ethiopia kumwakilisha Rais Kikwete katika mkutano wa kimataifa kuhusu masuala ya kilimo na chakula.

Sasa inaogopesha ina Maana Mawaziri wengi wa KIKWETE walifeli SECURITY CHECKS...

Kighoma Malima Senior alikuwa hampendi KIKWETE sababu alipata fununu za MWINYI kuwa anataka awe Rais wa Jamhuri; Ndio Maana akaanzisha na kukikimbia CCM

Lakini KIKWETE ni LOYAL kwa Watu wa KISARAWE...
 
Viongozi wengine waliokuwepo katika mapokezi hayo ni kwa sababu ugeni huo ulihusu maeneo yao ya kazi, kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Ma------.
Aluu, kwanini hili neno limekatwa? Ok, never mind..
 
Malima alipelekwa Wizara ya Kilimo kama kuwadi wa biashara ya ugawaji wa vibali vya uagizaji wa bidhaa za kilimo nchini hasa sukari na mchele. Uagizaji wa sukari ulipaswa kuwa viwanda na biashara lkn sasa upo kwa Malima.

Ukitaka kibali cha sukari na hela ya kuhonga ipo unaelekezwa kwa Riz1. Ukifika kwa huyu hatua inayofuata utasindikizwa kwa memo nzito hadi kwa Katibu Mkuu-Kilimo na kwa Malima. Na mchezo ndo unakuwa umekamilika hivyo.
 
Ritz njoo ufafanue huku,au we ni kufanya propagand tu??!!
 
Inawezekana huyu jamaa lugha inapanda kuliko mawaziri wengine wa jk

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
Ni kiingereza chake tu si kingine,si unajua wanyamwezi wanavyouma ngeli,baadae kuna mrejesho kwa jk,pale alisema nini eti? Basi nd'o jk anvyoungaunga.
 
Hivi ndie aliyeibiwa bunduki ya kivita smg na $ 4,000 hotelini Moro?

kama ndie anainufaisha U.S.A,vinginevyo ilikuwa sababu ya kutoonana na Obama
 
Huyu mtu alishawahi kukutwa na bunduki aina ya smg pamoja na bastola siku alipoibiwa vitu vyenye thamani ya sh.milioni 23.3 pale Nashera hoteli Morogoro.
Mpaka sasa bado sijaambiwa ni kwanini atembee na smg.
 
Kwani huyu dogo amesomea wapi?
University of Hauana (Cuba)
University of London (SOAS)
Univesity of London (SOAS)
Shaban Robert Secondary School
Upanga Primary School

[TD="align: center"]MSc. (Economics)
[/TD]
[TD="align: center"]1984
[/TD]
[TD="align: center"]1989
[/TD]
[TD="align: center"]MASTERS DEGREE
[/TD]

[TD="align: center"]MSc. (Econ)
[/TD]
[TD="align: center"]1994
[/TD]
[TD="align: center"]1995
[/TD]
[TD="align: center"]MASTERS DEGREE
[/TD]

[TD="align: center"]Post Graduate Diploma (Econ)
[/TD]
[TD="align: center"]1993
[/TD]
[TD="align: center"]1994
[/TD]
[TD="align: center"]POSTGRADUATE
[/TD]

[TD="align: center"]O-Level Education
[/TD]
[TD="align: center"]1979
[/TD]
[TD="align: center"]1982
[/TD]
[TD="align: center"]SECONDARY
[/TD]

[TD="align: center"]Primary Education
[/TD]
[TD="align: center"]1972
[/TD]
[TD="align: center"]1978
[/TD]
[TD="align: center"]PRIMARY
[/TD]
 
F.B.I ndio walikua wanaratibu waziri gani awepo! Kama huamini kamuulize Kova
 
Sasa inaogopesha ina Maana Mawaziri wengi wa KIKWETE walifeli SECURITY CHECKS...

Kighoma Malima Senior alikuwa hampendi KIKWETE sababu alipata fununu za MWINYI kuwa anataka awe Rais wa Jamhuri; Ndio Maana akaanzisha na kukikimbia CCM
Lakini KIKWETE ni LOYAL kwa Watu wa KISARAWE...
Mkuu unauhakika na unachosema? Prof Kighoma Malima hakuwa mtu wa chuki pamoja na watu kumsema vibaya. Prof Malima alihama CCM baada ya jina lake kuenguliwa kwa mizengwe kugombea Urais 1995. Mwalimu na Paul Sozigwa ni miongoni mwa watu waliomwekea mizengwe. Huo ni ukweli, jaribu kuulizia kwa undani, utaelezwa
 
Malima alipelekwa Wizara ya Kilimo kama kuwadi wa biashara ya ugawaji wa vibali vya uagizaji wa bidhaa za kilimo nchini hasa sukari na mchele. Uagizaji wa sukari ulipaswa kuwa viwanda na biashara lkn sasa upo kwa Malima.

Ukitaka kibali cha sukari na hela ya kuhonga ipo unaelekezwa kwa Riz1. Ukifika kwa huyu hatua inayofuata utasindikizwa kwa memo nzito hadi kwa Katibu Mkuu-Kilimo na kwa Malima. Na mchezo ndo unakuwa umekamilika hivyo.
hahahaaaa mkuuu nimecheka mpaka bas
 
Ufataani ndio muujuwao.

Kinawauma nini?
 
Jamaa anagonga Sana Kizungu, huenda alienda kama back up kumsaidia JK pale asipomuelewa Obama maana rais wetu kizungu chake kama Nchimbi tu
 
Back
Top Bottom