Kosa kubwa walilofanya wanasiasa wa upinzani hiyo miaka ya 1992, ni kukubali kuingia katika mfumo wa vyama vingi bila kumuomba mwl Nyerere azirudishe mali za CCM serikalini, na waanze upya vyama vyote.
Kwa kifupi, Tanzania iliingia katika mfumo wa chama kimoja 1967 mpaka miaka 1992, ambapo mfumo wa vyama vingi ulirejeshwa nchini.
Viwanja vingi vya mpira vimejengwa enzi za chama kimoja. Kama inavyojulikana, kauli ya kiongozi katika chama kimoja ni amri. Hivyo, wananchi walikuwa watiifu sana kujitolea kuhusu shughuli mbalimbali za ujenzi wa nchi vikiwemo hivyo viwanja.
Tunaweza kusema kipindi hicho, viwanja vilikuwa ni mali ya serikali kwa sababu, CCM ndio ilikuwa ni serikali, na serikali ilikuwa ni CCM.