Kwanini mali zilizokuwa zimejengwa au kufanywa na wananchi na Serikali zinageuzwa kuwa za CCM?

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,709
Leo nimepata story mfano viwanja vya mpira vingi vilenjengwa na wananchi na Serikali ila mwisho wa siku vinasemwa mali ya CCM.

Miradi mingi ya wananchi mwisho wa siku kuwa mali ya CCM.

Nini tatizo na kwa lipi kutoka kuwa mali ya wananchi mpaka kuwa mali CCM
 
Ndugu kujishughulisha na mambo ya ccm lazima uwe na ugonjwa wa akili.
Hivyo kaa mbali kwa afya ya akili yako


Uzi umefungwa
 
Mkuu umeleta wazo zuri sana wenye uelewa na haya mambo waje watufafanulie imekuaje viwanja vingi kuwa mali ya chama na siyo mali ya umma

Viwanja vingi vilijengwa miaka ya nyuma hivi CCM iliwezaje kujenga viwanja hivyo vyanzo vya mapato vya kuweza kujenga hivyo viwanja vilikua ni vip
 
Kosa kubwa walilofanya wanasiasa wa upinzani hiyo miaka ya 1992, ni kukubali kuingia katika mfumo wa vyama vingi bila kumuomba mwl Nyerere azirudishe mali za CCM serikalini, na waanze upya vyama vyote.

Kwa kifupi, Tanzania iliingia katika mfumo wa chama kimoja 1967 mpaka miaka 1992, ambapo mfumo wa vyama vingi ulirejeshwa nchini.

Viwanja vingi vya mpira vimejengwa enzi za chama kimoja. Kama inavyojulikana, kauli ya kiongozi katika chama kimoja ni amri. Hivyo, wananchi walikuwa watiifu sana kujitolea kuhusu shughuli mbalimbali za ujenzi wa nchi vikiwemo hivyo viwanja.

Tunaweza kusema kipindi hicho, viwanja vilikuwa ni mali ya serikali kwa sababu, CCM ndio ilikuwa ni serikali, na serikali ilikuwa ni CCM.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom