Kwanini mahusiano mapya unapata raha sana lakini mkizoeana unaona kero?

Applicant

JF-Expert Member
Feb 12, 2020
1,962
1,746
Yaani hii imekaaje?

Unakuta mtu unapania kabisa kua nikimpata huyu naoa kabisa, lakini baada ya kumpata na kupata unachotaka unaona kama yaani hana jipya, na unakua huna hamu naye kabisa, yani hata akikuita unatamani hata kupasuka kwa hasira, hii imekaaje?
 
Ni kawaida kuashkia sana kitu usichokua nacho ila ukikipata kinakinai mfano ukiwa huna hata elfu kumi unaiona laki ni hela lakini ukishashika laki mara mbili tatu unawaza mamilioni,ukipanga chumba kimoja unawaona waliopanga nyumba nzima wameyapatia ila ukifikia uwezo wa kupanga nyumba unawaza kujenga yako.

Sasa kwenye mapenzi mfumo ni uleule tena kwenyewe ni mbaya zaidi sababu wapenzi wapya huficha makucha yaani zile tabia flani,akikuona anatembea kama anakanyaga mayai,siku akija kwako anakuja na ile chupi nyeupe mpaka katikati yaani hathubutu hata kujamba mbele yako,chakula anakula kistaarabu tena kidogo tuu ameshiba.

Punde si punde badala ya kukuita Sweet ni kukusonya msonyo wa jini kikongwe,anakula tonge kubwa kama kitenesi na anaweza kunywa mchuzi katikati ya ugali,akikokota sufuria la kiporo cha wali kama alitoboe wakati mwanzo alikua hamalizi chipsi,na kwa kuwa unakuwa nae muda mrefu sms na simu za michepuko na yule X wake aliyekuambia wameachana unazifuma mara moja moja hapo ndio utajua kazi zingine za moyo mbali na ile ya kusukuma damu.
 
Mapenzi hua hayadum .....baada ya mapenzi kuisha kinachobaki Ni Bond
Kama Ni ka Dem unakidinya mwisho wa siku kinachokuja kubaki baada ya amsha amsha ya mapenzi Ni Bond ya mdinyano...! Ndo maana mnaeza achana lakin bado mkaendelea kupasha kiporo milele daima( Bond)
Kama Ni mke wako mbwembwe za honeymoon nk zitaisha mkizaa watoto hyo tyari Ni Bond iliyotokana na mjegejo ambayo itadum milele hata muachane ndo maana wanasemaga Mtalaka hatongozwi Ni kujibebea tu
 
Ni kawaida kuashkia sana kitu usichokua nacho ila ukikipata kinakinai mfano ukiwa huna hata elfu kumi unaiona laki ni hela lakini ukishashika laki mara mbili tatu unawaza mamilioni,ukipanga chumba kimoja unawaona waliopanga nyumba nzima wameyapatia ila ukifikia uwezo wa kupanga nyumba unawaza kujenga yako.
Sasa kwenye mapenzi mfumo ni uleule tena kwenyewe ni mbaya zaidi sababu wapenzi wapya huficha makucha yaani zile tabia flani,akikuona anatembea kama anakanyaga mayai,siku akija kwako anakuja na ile chupi nyeupe mpaka katikati yaani hathubutu hata kujamba mbele yako,chakula anakula kistaarabu tena kidogo tuu ameshiba.
Punde si punde badala ya kukuita Sweet ni kukusonya msonyo wa jini kikongwe,anakula tonge kubwa kama kitenesi na anaweza kunywa mchuzi katikati ya ugali,akikokota sufuria la kiporo cha wali kama alitoboe wakati mwanzo alikua hamalizi chipsi,na kwa kuwa unakuwa nae muda mrefu sms na simu za michepuko na yule X wake aliyekuambia wameachana unazifuma mara moja moja hapo ndio utajua kazi zingine za moyo mbali na ile ya kusukuma damu.
Aisee! watu mna fani za uchambuzi!
 
Yani hii imekaaje??

Unakuta mtu unapania kabisa kua nikimpata huyu naoa kabisa, lakini baada ya kumpata na kupata unachotaka unaona kama yani hana jipya, na unakua huna hamu nae kabisa, yani hata akikuita unatamani hata kupasuka kwa hasira, hii imekaaje??
Ulitamani. Hukupenda
 
Binadamu tumeumbwa kukinai kitu...

Kupitia hilo inashauriwa kupeana kabreak kafupi au kalikizo kafupi ktk mapenzi kwa kila baada ya muda fulani...

Pia tunashauriwa kuwa wabunifu ktk mapenzi coz mapenz ni sanaa kubwa sana,yaani mkifanyiana mautundu kuna muda ule wa kupeana kalikizo mtakuwa mnamisiana kwa hisia kali.

Mfno...mpishi mzuri anaweza akakupikia pishi tofautitofauti kwa mchele mmoja nawala usikinae mwezi mzima.

Na ndo Mana baadhi ya dini na kabila wameruhusu mwanaume kuoa mwanamke zaid ya mmoja kuna faida kubwa sana apo...moja hyo ya kutochokana na kumisiana.
 
Kuna kitu inaitwa ubinafsi

Unajiona utampenda ipasavyo
Ila hupendi matatizo yatayojitokeza baadae km sehemu ya maisha yenu.

Unakuta mtu ata mute mpaka asikie umerecovery ndo

Utaona text

"Mambo VP"
 
Back
Top Bottom