Ndugu wanajamvi, nimekuwa nikifuatilia jinsi serikali yetu ya Tanzania inavyoanza kutengeneza na kuwaandaa waislam na wapinga dhulma kujiunga na ugaidi.
Kama mwezi mmoja uliopita nimekuwa nikiona msako mkali wa kuzifunga madrasa huko Arusha na Moshi, polisi na serikali kwa ujumla wakiziita madrasa eti ni vituo vya kufundisha ugaidi. Kwani hizi madrasa zimeanza Leo?
Na kwanini zimebadilishwa jina badala ya madrasa zinaitwa vituo kweli hii ni haki?
Je, BAKWATA wapo wapi? Masheikh wa mikoa wapo wapi? Je, wanajua kuwa ugaidi unajengwa kwa kuwa na mfumo kandamizi unao pendelea upande mmoja na hatimae upande mwingine kuona kama unaonewa nakuamua kujitoa muhanga kwa ajili ya wengine?
Leo tarehe 17.04.2015 nimeona taarifa ya habari ITV police pamoja na mkuu wa mkoa DODOMA wamefunga madrasa mbili eti wanaviita vituo haram vya mafunzo ya kigaidi. Je, kweli hii ni sawa? Waislam na wapenda amani hii kweli ni sawa tunavyoonewa na kunyanyaswa ndani ya nchi yetu sote ni sawa?
Na kwanini wanavyokamatwa hawahojiwi kila mtu akawasikia kwenye vyombo vya habari na kinachofanyika ni kamanda wa polisi kuwapa kesi na kuwaita anavyojua yeye kisha kuswekwa kwenye gari ili umma ujue ni wahalifu.Kweli hii ni sawa? Kwanini hawajawahi kuulizwa tukasikia majibu yao mbele ya kadamnasi?
Na kwanini wakristo wana vikundi vya scout makanisani mbona hawajawahi kukamatwa, kweli hii ni sawa? Hawajui kama roho zinauma na lolote linaweza tokea?
Kwanini nchi hii inakuwa na double standard?Mfano mashekh wengi wapo mahabusu na wamenyimwa dhamana na kuteswa eti wanaeneza chuki na kuhatarisha amani. Kweli hii ni haki?
Shekh Ponda alinusurika kuuawa kwa risasi pale Morogoro serikali walikaa kimya.
Leo hii mchungaji Gwajima amemtukana kiongozi mkubwa wa kanisa mbona hajafanyiwa kama alivofanyiwa Ponda? Mbona yeye hajanyimwa dhamana kwa kuhatarisha uvunjifu wa amani kwa kudhalilisha kanisa katoliki?
Kama angekuwa shekh yeyote kamkejeli Muft Simba ingekuwaje kama si kufanywa kama Shekh Ponda?
Hivi mnajua kinachoendelea Kenya kilianza kama hivi? Kwanini nchi yetu inakuwa hivi?
Naomba nisaidiwe ni sheria gani inasema ukitaka kuanzisha madrasa lazima isajiliwe? Eti wameanza kusaka vituo vya watoto Yatima vilivoanzishwa bila kufuata utaratibu kumbe wanasaka madrasa, hii haikubaliki tumewastukia na mabomu mnayaandaa mwenyewe siku yakilipuka mtamtafuta mchawi kumbe mchawi ni serikali ya kidhalimu.
Naomba kuwasilisha.