Kwanini madirisha ya choo hujengwa madogo?

Kwanini madirisha ya choo hujengwa madogo?

Hehehe nimeshtuka nilivyoona title sababu nilikuwa nawaza hilo hilo. Nikajiuliza nimepost saa ngapi tena hii.
Sababu kuu ni Ufaragha.
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Nauliza kitu nisaidie wadau nina rafiki yangu ana mchumba wake yaani kamsomesha chuo ndio anamaliza mwaka huu mwezi wa saba.Jamaa alipeleka barua juzi lakini mama yake demu katoa nje hataki coz wakristo wote ila madhehebu tofauti na dingi yake demu haongei mama ndio last say. Halafu kinachoumiza zaidi wazazi wake wanajua jamaa kamsomesha mtoto wao. Chakushangaza walengwa wenyewe wanapendana.
 
...

....kadirisha kadogo ili kutunza harufu ya kinyesi ova!!!!
 
Wale wasio na aibu wataingilia dirishani
 
Ni kweli mkuu ila inategemea na aina ya choo hasa vyoo vya shimo inashauriwa kiwe na dirisha dogo ili lisiruhusu mwanga kupita kiurahisi ndani yaani vyoo vya shimo havihitaji mwanga sana hasa mida ya mchana
Kwanini vyoo vya shimo havihitaji mwanga sana mkuu? Kumbuka hata vyoo ambavyo si vya shimo pia huwa na madirisha madogo
 
lakini hata chumbani watu hufanyia mapenzi na wanaweka madirisha makubwa, chumbani hakuhitaji privacy?

We nawe na uprofesa wako.....

Issue ni kuwa unahitaji privacy kwa wakati huo na kufunga na kufungua....jiulize chooni kila mara watu wanaenda watapata hiyo adhabu ya pandisha shusha mapazia??

Hata hivyo hoja kuu ni ile hali ya matumizi ya umajimaji unaoweza kuathiri pazia unalotaka kuweka na kufanya mazingira ya usafi na kiafya Kuwa magumu
 
Sijakupinga mkuu ndio maana nimesema hapa nilipo madirisha ni makubwa, nilikuwa najaribu kujenga hoja. Maana hata mwanga una kiasi kinachotakiwa kwa eneo husika, studio nyingi zina giza kwakuwa hazina madirisha.
Nys watu wengi katika kujenga kwetu tunaona kama chooni ni sehemu ambayo haina msingi au pahali pa kawaida sana tunasahau kupahudumia kama palivyo muhimu kiuhalisia. Mazingira pia huchangia ndio maana vidirisha vya juu tofauti na chumbani. Okay labda tujadili kwanini vyoo vingi vinamadirisha madogo hapo ndio tunaweza kuja na suluhisho.
Mbuty studioi kunakuwa hakuna madirisha na hata kama yapo huwa yanazibwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa makelele ya nje hayaingii ndani lakini nashindwa kuelewa kwanini chooni kuwe na madirisha madogo
 
Last edited by a moderator:
Mimi nilishauriwa na fundi na nikalazimika kufuata ushauri wake bila kuwa na sababu....! Labda nimrudie fundi wangu nikamuulize ni kwa nini...
 
kwanini vyoo vya shimo havihitaji mwanga sana mkuu? kumbuka hata vyoo ambavyo si vya shimo pia huwa na madirisha madogo

Sababu ni moja, mara nyingi vyoo vya shimo hasa maeneo ambayo yana nzi wengi hushauriwa zaidi kufanya hivyo lakini choo hicho lazima kiwe na bomba la kutolea hewa chafu na ambalo linaruhusu mwanga kupita, hivyo basi wale nzi wanaokuwa ndani ya shimo wakifanya yao ambayo ni muhimu pia wanakuwa hawaji nje kutoka shimoni na matokeo yake wanakuwa attracted na ule mwanga unaopita kwenye bomba la kutolea hewa safi ambalo mwishoni kule juu linakuwa lina wavu umeziba hivyo wanakuwa wanapanda juu kule kwenye bomba kufuata mwanga, kama kikiwa na mwanga wa kutosha ndani utaona nzi wengi wanazengea mpaka juu.

Hivyo vyoo vingine unavyosema wewe ni mazoea tu ndio yanafanya hivyo lakini bado unaweza ukaweka dirisha si kubwa wala si dogo sana (linaweza likawa sentimita 60 kwa 60 yaani mara mbili ambayo tumeyazoea kikubwa nyumba iwe imejengwa kwa urefu unaostahili.)
 
We nawe na uprofesa wako.....

Issue ni kuwa unahitaji privacy kwa wakati huo na kufunga na kufungua....jiulize chooni kila mara watu wanaenda watapata hiyo adhabu ya pandisha shusha mapazia??

Hata hivyo hoja kuu ni ile hali ya matumizi ya umajimaji unaoweza kuathiri pazia unalotaka kuweka na kufanya mazingira ya usafi na kiafya Kuwa magumu

Punguza jazba, relax kisha changia. Si lazima pazia liwe kubwa kiasi cha kugusa chini hivyo kumsumbua mtumiaji kupandisha na kushusha. Pazia linakuwa la kawaida tu mkuu. Karibu
 
Kila siku najiuliza kwanini nyumba zinapojengwa madirisha ya chooni hujengwa madogo tena yanakuwa juu?

Je sababu ni nini ?

Karibuni kwa michango yenu.

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)

Mambo ya kizamani hayo, bro wangu kajenga nyumba yake dirisha la choo ni kama la chumba cha kawaida ila kaweka kioo kile cha opaque.
 
Last edited by a moderator:
Nauliza kitu nisaidie wadau ninarafiki yangu anamchumba wake yaani kamsomesha chuo ndo anamaliza mwaka huu mwezi wa saba.Jamaa alipeleka barua juzi lakini mama yake demu katoa nje hataki coz wakristo wote ila madhehebu tofauti na dingi yake demu haongei mama ndo last say. Halafu kinachoumiza zaidi wazazi wake wanajua jamaa kamsomesha mtoto wao. Chakushangaza walengwa wenyewe wanapendana.

Kwa vile wanapendana Waambie watoroke na wakafunge ndoa mbali ta kiserikali
Kisha warudi kusalimia nyumbani baada ya kupata mtoto
Hapo kesi itakuwa imeisha.
 
Punguza jazba, relax kisha changia. Si lazima pazia liwe kubwa kiasi cha kugusa chini hivyo kumsumbua mtumiaji kupandisha na kushusha. Pazia linakuwa la kawaida tu mkuu. Karibu

Bro Kati ya vitu sijajaliwa na aliyeniumba ni jazba.....haifanani hata kidogo na sarcasm
 
Back
Top Bottom