Kwanini madirisha ya choo hujengwa madogo?

Kwanini madirisha ya choo hujengwa madogo?

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,618
Kila siku najiuliza kwanini nyumba zinapojengwa madirisha ya chooni hujengwa madogo tena yanakuwa juu?

Je sababu ni nini?

Karibuni kwa michango yenu.

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)
 
Last edited by a moderator:
Ili mtu wa nje asikupige chabo japo ni mambo ya kizamani tu na mazoea ya kujenga nyumba za hivyo tangu enzi na enzi.
 
topic zingine za ajabu sn.

Great Thinker (Philosopher) kawaida yake ni kuuliza maswali kama haya; Ni Kawaida Ukakuta Mwingine Kauliza.
1.Kwanini Tunapoingia Ndani Ya Nyumba Tunapitia Mlangoni?
2. Kwanini Tunajisaidia Haja Kubwa Tukiwa Tumechuchumaa?
3. Au Kwanini Choo Isijengwe Eneo Wazi Bila Kuta Ili Kila Mmoja Aonekane Wakat Anawajibika?

Hayo Yote Ni Maswali Ya Great Thinker.
 
Ukubwa wa dirisha hutegemea na ukubwa wa Chumba
Huwezi kuweka Ki dirisha kidogo kwenye chumba kikubwa,
Anyway umewahi kutembelea na nchi za watu? Au swali lako limebase Vyoo vya kibongo tuu?
 
Kila siku najiuliza kwanini nyumba zinapojengwa madirisha ya chooni hujengwa madogo tena yanakuwa juu?

Je sababu ni nini ?

Karibuni kwa michango yenu.

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)

Hoja nzuri ila hapo umeongea kwa ujumla, Nyumba hizo za wapi, hapa nilipo madirisha ya choo ni makubwa tu. Okay turudi kwenye mada, tuanze kwa kuangalia kazi ya madirisha, hebu jaribu kutaja hata kazi mbili za madirisha unazozifahamu ambazo ni za msingi halafu oanisha majibu yako na chumba cha chooni huku ukiwaza matumizi ya eneo, mahali lilipo na kusudi. Nathani kwa kiasi tunaweza pata majibu ya msingi juu ya hiyo hoja. Na pia niongeze hapo ktk swali lako ili kuleta uelewa kwamba madirisha ni madogo na yanakuwa juu. Asante
 
Kazi za madirisha ni pamoja na kuingiza hewa na kuingiza mwanga, hivyo vitu viwili vinahitajika hata chooni mkuu.
 
Hakuna ulazima wa kuweka dirisha dogo ila kwa nchi zingine kuna regulations kama kuweka ventilation na pia choo kiwe wapi.
Lakini kwa madirisha ni uamuzi wako kuweka dirisha kubwa ambalo linapitisha mwanga mkubwa au unaweka glass blocks, ni uamuzi tu kwani madirisha madogo yamepitwa na wakati sasa
 
kazi za madirisha ni pamoja na kuingiza hewa na kuingiza mwanga, hivyo vitu viwili vinahitajika hata chooni mkuu.

Ndio maana huku tuliko tunajisaidia pembezoni mwa bahari, huko ukikumbana na mama mkwe utajijua mwenyewe.
 
kazi za madirisha ni pamoja na kuingiza hewa na kuingiza mwanga, hivyo vitu viwili vinahitajika hata chooni mkuu.

Ni kweli mkuu ila inategemea na aina ya choo hasa vyoo vya shimo inashauriwa kiwe na dirisha dogo ili lisiruhusu mwanga kupita kiurahisi ndani yaani vyoo vya shimo havihitaji mwanga sana hasa mida ya mchana
 
kama ni kupigwa chabo kwanini wasijenge madirisha makubwa lakini wakaweka na mapazia pia

Usisahau pia kuna matumizi ya maji ambayo kama ukiweka madirisha makubwa na mapazia yatalowa Sana na isiwe nzuri kiafya pia
 
kazi za madirisha ni pamoja na kuingiza hewa na kuingiza mwanga, hivyo vitu viwili vinahitajika hata chooni mkuu.

Sijakupinga mkuu ndio maana nimesema hapa nilipo madirisha ni makubwa, nilikuwa najaribu kujenga hoja. Maana hata mwanga una kiasi kinachotakiwa kwa eneo husika, studio nyingi zina giza kwakuwa hazina madirisha.
Nys watu wengi katika kujenga kwetu tunaona kama chooni ni sehemu ambayo haina msingi au pahali pa kawaida sana tunasahau kupahudumia kama palivyo muhimu kiuhalisia. Mazingira pia huchangia ndio maana vidirisha vya juu tofauti na chumbani. Okay labda tujadili kwanini vyoo vingi vinamadirisha madogo hapo ndio tunaweza kuja na suluhisho.
 
Kila siku najiuliza kwanini nyumba zinapojengwa madirisha ya chooni hujengwa madogo tena yanakuwa juu?

Je sababu ni nini ?

Karibuni kwa michango yenu.

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)

Na kwa nini unapoingia chooni Ukichutama ama kukaa kushusha Mambo lazima utizame Mlango
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom