Kwanini Madereva wana uelewa wa mambo mengi sana?

Kwanini Madereva wana uelewa wa mambo mengi sana?

Nitajaribu kuulizia kuhusu mambo yanayonitatanisha hapa ardhi ya nyumbani. Nadhani nitapata clues za kunisaidia
 
Huwa wanasikiliza mabishano ya raia kwenye madaladala. Mimi mmoja ninayetoa elimu bure ya uraia kwenye dalala.
 
Madereva muda mwingi wanasikiliza redio ndani ya gari... imagine dereva wa DFP anavyokula lami karibia nchi nzima karibia siku nzima anasikiliza redio au habari..muda mwingi wanasikiliza redio.
1. Akiwa anaosha gari anapiga stori na waosha magari, exposure hiyo.

2. Wakati anamsubiri bosi ofisini anasikiliza Sports Headquarters,wakati wewe umekodolea macho Microsoft Excel ofisini au uko semina

3. Madereva wengi hasa hawa professional wananunua magazeti wanasoma,pita hata kwenye foleni madereva wa daladala wanasoma Sana magazeti ya michezo

4. Wakija gereji ndo kabisaa full story na wana...

5. Madereva hawana roho mbaya...ona madereva wa daladala Dar wanavyoachiana dei waka,na kuwapa fair magari ya private...hiyo inawapa marafiki wengi ambao wanawapa taarifa nyingi...

6. Madereva wana interaction kubwa na abiria wengine...hapo ndio wanapiga story na ku exchange new ideas
ukweli na uhakika.
 
Sema madereva ni washerati ile mbaya. Haswa wale wanaokwenda mikoani. Kila mkoa au center kubwa kama chalinze na mikumi kote huo wana totoz.
 
Hawa jamaa ni watu wa ajabu sana halafu si mmoja ni wote, wanajua vitu vingi sana, taarifa mbalimbali za kila nyanja wanazo. Ni watu wapelelezi na wadadisi ndio maana wana fahamu mambo mengi sana yanayoendelea kila kona . wanashangaza sana ni tofauti sana na watu wa taaluma nyingine. Hawa jamaa wapo vizuri kila sekta
1. Mambo ya siasa wanayajua na wanafuatilia, wanajua viongozi tofauti na taaluma nyingine kuna dokta nilimuuliza mkuu wa police na mkuu wa wilaya wa mkoa wako ni nani hakujua lakini dereva anajua majina yote
2. Mambo ya mpira wa nje na ndani nchi wapo vizuri
3. Habari za udaku na wanamuziki wapo vizuri wanamjua hadi tunda. Diamond etc
4. Mambo ya biashara wanajua
5. Sekta ya elimu wanaijua. Na kuzitambua shule bora
6. Nchi wanaifahamu vizuri
7. Mambo madogo madogo ya ujenzi. Ufundi, ubora wa vitu etc
8 mambo ya dini na viongozi wa dini wanawajua
9. Waganga wachawi
10. Ukiwa na shida yeyote madereva wanakuwaga na konection za kukusaidia

Madereva nimewavulia kofia, hawa watu ni nomaa
Na je "Makonda"?
 
Haswa ukutane na madereva wa mawaziri,wale wanawapeleka mpaka kwa waganga,kila kitu wanafahamu,hebu imagine dereva anatembea na msafara wenye escort ya maafisa usalama ataachaje kufaham baadhi ya siri
 
Haswa ukutane na madereva wa mawaziri,wale wanawapeleka mpaka kwa waganga,kila kitu wanafahamu,hebu imagine dereva anatembea na msafara wenye escort ya maafisa usalama ataachaje kufaham baadhi ya siri
maafisa usalama hawatoi siri
 
Sasa mbona wengi mnawadharau?utamsikia mtu anasema yule si dereva tuu..hafu ukija kwenye income dereva kamzidi hadi mwalimu mwenye digrii.ila nawakubali maana wenyewe wamekubaliana hali halisi na wanapambana na hali yao
 
Back
Top Bottom