MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Ninapenda kufahamu tu ni lini huyu bwana mkuu wa Dar alifanikiwa kudhibiti biashara na utumiaji dhidi ya Madawa ya kulevya na taifa likamtambua na kumtunuku nishani juu ya kazi yake?
In juzi tu alijaribu zoezi hilo pamoja na kujikuta anaingiza na ajenda zake binafsi kwa mahasimu wake, tatizo lilikua kutofuata taratibu za kisheria juu ya kuwakamata watuhumiwa hali iliyozua maswsli mengi. Naweza kusema kua zoezi hilo liligubikwa na personal interests kwa sababu ya kuwataja baadhi ya watu ambao walifikishwa hata kwa mkemia mkuu na kuthibitishwa kua hawatumii madawa ya kulevya,kuna watu walikamatwa kwa tuhuma za Madawa ya kulevya leo tunasikia wanatuhumiwa kuajiri wahamiaji haramu.Hivyo zoezi halikutua kwa mpambanaji sahihi kamaa ambavyo baadhi ya watu wanajaribu kutuaminisha,lakini kama wananchi tunashukuru kwa kulianzisha hilo hali iliyomfanya Mh Rais kuteua kamishna wa mamlaka ya kupambana na kudhibiti Madawa ya kulevya.
Kumkingia huyu mtu kifua kutokana na kasoro zake za kimaadili ya kiutumishi kwa madai ya kwamba hatuna nia ya dhati na upambanaji juu ya Madawa ya kulevya ni kupotoka kabisa, Tunapotoka sana kwa sababu hivi sasa tunaye mamlaka kamili ya kupambana kadhia hiyo chini ya kamishna aliyepewa nguvu kishera tatizo liko wapi?
Katika mamlaka ya kupambana na kudhibiti Madawa ya kulevya kumejaa wasomi na makachero wataalam waliofunzwa namna ya kupambana nayo sasa huyu mkuu wetu wa mji amesomea wapi? Kwanini tunaingiza siasa kwenye mambo muhimu namna hii?
Itoshe kusema aliyekosea awajibishwe kwa mujibu wa sheria za nchi, kama mtu anatuhumiwa kwa jambo flani achunguzwe iundwe kamati aitwe juu ya tuhuma zinazomkabili na ikithibitika ni kweli achukuliwe hatua kama watanzania wengine, ikidhibitika hana hatia aendelee na ujira wake! Kwani tatizo liko wapi kuliko kuendelea na sintofahamu chini ya wingu nene na zito lililotanda kwenye taifa letu kwa sababu ya mtu moja?