Kwanini Maalim Seif Shariff Hamad hatibiwi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Katika kampeni zake uchaguzi wa 2010 Maalim SEIF alikuwa akisema Kuwa Hospitali ya Mnazi MMOJA zanzibar iko katika hali mbaya kwa sababu viongozi wa nchi ya Zanzibar hawatibiwi pale wanatibiwa nje ya nchi.Akasema kuwa yeye akichaguliwa kamwe na asilani haji kukubali kwenda kutibiwa nje ya nchi yeyote.Atatibiwa Mnazi mmoja wanakotibiwa wazanzibari wengi wa kawaida.

Mungu si Athumani wananchi wakampa kura akateuliwa kuwa makamu wa kwanza wa Raisi wa Zanzibar.Alipopata umakamu wa Raisi tu huyo akatimuka india kwenda kufanyiwa Medical CHECKUP.Aliporudi akaulizwa na waandishi wa habari haya kulikoni mwenzetu mbona ulisema hutakubali kwenda hospitali nje? Akajibu kuwa yeye kakuta taratibu hiyo ipo ya viongozi wakuu kutibiwa nje.Anaenda kule kwa mujibu wa huo utaratibu ambao kaukuta.Lile la kusema sitakubali kalitupa kwenye kilindi cha bahari kule pemba.

Toka wakati huo ni yeye na matibabu nje ya nchi.Hospitali ya Mnazi mmoja kuboreshwa ni ndoto ya mwendawazimu.

Swali lile lile linaendelea ni lini Maalim SEIF atatibiwa Hospitali ya Mnazi mmoja zanzibar.Ni swali ambalo labda waandishi wa habari wamuulize Seif Sharrif Hammad.
 
Mtoa post buana umesahau mkwere alipowahadaa wasukuma kuwa kila mtu atakula mayai mawili kila siku na chai ya maziwa,kwa kipindi chote cha urais wake,
Kilichowapata wanajua wenyewe
 
Back
Top Bottom