Kwanini Lowassa anakwepa kuzungumzia ufisadi?

Septemba 15, 2007; siku ile mwanga mpya ulipoizukia nchi hii pale Mwembe Yanga - Temeke, Dar es Salaam kwa kutangazwa ile orodha maarufu kama ORODHA YA AIBU ambapo neno kuu lilikuwa UFISADI haraka haraka kesho yake CCM kupitia kwa mtendaji wake mkuu Lt. Yusufu Makamba wakatangaza kwamba neno UFISADI haliko kwenye kamusi yao!

So, nitashangaa sana kama CCM wataongelea neno lisilokuwepo kwenye orodha yao ya maneno yaani Kamusi unless hiyo dictionary iliyotajwa na Makamba wakati huo imefanyiwa marekebisho makubwa. Nadhani Lowassa hapendi kuwa mnafiki kama hao CCM wengine wanojifanya kuongelea ufisadi kumbe ni usanii mtupu.
 
Lowassa na ufisadi ni sawa na samaki na maji,havitengamani...
 
Lazima uweze kufanya maamuzi magumu.... wakati hazungumzii mamilioni ya uswizi kama ni kweli au laa! Na EPA ni kweli au laa!
Tusizingane, yaani huyu jama akipewa kura na watanzania, Basi nitadhibitisha ujinga wa WANANCHI WA NYERERE; ambao wao tuu ndio waliobaki nyuma na kuachwa mbali na raia wa Kenyata, Nkuruma, Mandela, etc????
 
hv huyu bwana anatumia pesa nyingi sana kutaka kuingia ikulu kwani anataka kufanya nn ikulu? Atazirudishaje hizo pesa? Simpend huyu baba kwa wizi ambao wameufanya na mwenzake..na kama watanzania watarudi nakumpa kura jamaa awe raisi nitawashanga sana na nitaamini ccm aitatoka madarakani labda baada ya miaka kumi na tano
 
Nitashangaa Watz wakimuingiza huyu fisadi pacha wa JK madarakani mwaka 2015. Yaani itakuwa miaka 20 Watz tunaongozwa na known corrupt leaders. What a waste!
 
Stop kidding bro.. Lowassa won't bite the very finger his mother feeds him with..!! anafanya vyema kutokuonyesha kuwa anakerwa na ufisadi kwani he is a player in it.. he is showing us his true colours..
 
lowasa, ni mwizi,fisadi na jangiri alie tusababishie tuwe na maisha magumu kama wakimbizi ndani ya nchi yetu tajiri
 




Huyu ndiyo LAIGWANAN a.k.a the next Presidaaaahhh!!

Yaani haka kajamaa katika kitu kinachoitwa Urais hakana aibu kabisa,Sidhani kama Waislamu walio wengi wanavutiwa na haya maigizo.Huenda JK amemuahidi kumuachia kijiti,JK anajulikana kwa kuwatosa wenzie dakika mwisho.Ila mwisho wa siku ni wapiga kura ndio tutakaomchagua Rais tutamkae.Atapata mshangao wa mwaka.
 
Siku atakapoongelea ufisadi -- hasa ufisadi wa ngazi za juu (siyo rushwa za matrafiki na manesi) nitampa kura yangu bila kufikiri mara mbili -- iwapo atagombea urais.


Kama atawataja wala rushwa wakubwa kama alivyofanya dr Slaa hapo kidoogo nitamwamini
 
GM kila mtu yu-akerwa na ufisadi, na kukereka na ufisadi sio kivile kwamba mtu apande jukwaani aropoke audanganye umma halafu akishuka jukwaani apelekwe baa ya jirani kwa mbuzi choma. Ilivyo ni kuwa ndani ya chama ndiko mkakati wa kupiga vita ufisadi unasukwa na kuanza utekelezaji kimya kimya na sio kama ninyi CDM ambao kwenu kila issue maandamano...
 
Msarendo; Ni sawa na kusema eti kupe mkubwa aseme nakerwa na wanaonyonya damu ya ng'ombe, is it logical?
 
Last edited by a moderator:
Kama kura zitapigwa jamiiforums lowassa atashindwa and not otherwise
 
Waziri mkuu wa zamani aliejizulu kwa kashfa ya Rushwa na mbunge wa Monduli mh Edward Ngoyai Lowassa,ni mmoja wa viongozi waandamizi na wenye ushawishi mkubwa ndani ya Chama chama Mapinduzi.

Mh Lowassa amekuwa akitajwa sana kuwa ni miongoni mwa wana CCM ambao wanatarajiwa kujitosa ktk uchaguzi mkuu wa rais 2015. Mh Lowassa amekuwa akizunguka nchi nzima ktk makanisa,misikiti na taasisi mbalimbali za kijamii akitoa michango mikubwa ya pesa pale anapokua amehudhuria km Mgeni rasmi.

Mh Lowassa pia amekuwa akitoa kauli nzito nzito pale anapohutubia,mfano kauli aliyowahi kuitoa kuwa Ajira kwa vijana ni Bomu linalosubiriwa kulipuka muda wowote endapo serikali haitatafuta njia mbadala ya kukabiliana nayo.

Mh Lowassa aliwahi pia kuikosoa serikali ya Jakaya Kikwete kwa kutokua na uwezo wa kuchukua Maamuzi magumu kwa maswala mbalimbali ya kijamii.

Ni hapo jana tu akizungumza ndani ya Bunge kwa mara ya tatu tangia alipojiuzulu mh Lowassa aliikosoa serikali ya Ccn kwa kile alichodai kuwa viongozi wake hawana vipaumbele maalum ktk mambo mbalimbali kwa kuyainisha vipaumbele vichache na badala yake wamekuwa wakifanya mambo Kiswahili kwa kuzungumza mambo mengi na yasiyotekelezeka.

Mh Lowassa amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali iliyoko madarakani,lakini ktk kukosoa kwake pamoja na kuwa anajua kwamba RUSHWA ndio ugonjwa mkubwa unaoitafuna nchi,,binafsi sikuwahi kumsikia mh Lowassa akizungumzia UFISADI NA RUSHWA ambao umeshamiri sana ktk sekta mbalimbali za serikali huku ikifanya watu wa chini hususan vijana anaowapigia (yeye Lowassa) debe kukosa haki zao na maisha yao yakizidi kukosa mwelekeo.

Mh Lowassa amekuwa shujaa anaetaka viongozi kuchukua maamuzi magumu bila kuogopa ktk maswala mbalimbali ya nchi,lakini ni kwanini Mh Lowassa amekuwa hazungumzii swala la Rushwa na Ufisadi ulioshamiri ktk serikali na taasisi zake huku akijua kuwa Rushwa ndio adui mkubwa wa maendeleo na maamuzi magumu anayatoka viongozi kuchukua?
Kiongozi anaechukua Rushwa atawezaje kuchukua maamuzi magumu?
 
mkuu umelala unamuwaza lowassa,kila utakacho gusa nchi hii ni lowassa,lowassa!hata mkeo atakuwa anamuwaza lowassa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…