Kwanini ligi ya Nigeria siyo bora?

Kwanini ligi ya Nigeria siyo bora?

Kwa bara la Africa na baadhi ya nchi huko mbele nafikiri WaNigeria ndio taifa lenye wananchi wake waliofanikiwa zaidi kwenye maisha.

Wananchi wa Nigeria mmoja mmoja wana uchumi mzuri sana.

Kwa hiyo WaNigeria wengi muda mwingi wamefocus kwenye kusaka utajiri iwe kwa njia yoyote ile lazima afanikiwe sana. Hata ikibidi atepeli. Na utapeli wa Nigeria ni wa darasani kabisa ni wa kiwango cha juu.

WaNigeria ndio watu wanaoongoza waliotawanyika ulaya na Marekani kote kusaka maisha. Na naweza kusema WaNigeria ndio watu wanaokula bata sana,ksbb uchumi wanao. Taifa lao limewatengenezea mazingira ya kufanikiwa.

Sisi wa juu hawapendi ufunguliwe kuanzia kwenye elimu mpaka kibiashara.

Na bahati nzuri sana kwa Mtanzania tungefunguliwa kuanzia kwenye Elimu iliyo bora. Elimu yetu ni duni sana.

Fikiria mpaka miaka hii watoto mpaka sasa wanafundishwa panzi ana miguu mingapi? Watoto wetu bado wanafundishwa kukariri kumjua kuanzia mtendaji wa kijiji mpaka mawaziri wote hadi waziri mkuu (wakati hawa haina haja ya kuwakariri atawakuta mtandaoni akiwahitaji,na bahati mbaya siku 2 tu wamebadirishwa,kuna haja gani ya kuwakariri?). Wakati huo huo watoto wa KiNigeria na Kenya wanafundishwa uzijue sheria ukiwa nchi nyingine tambua mipaka yako tambua uhuru wako. (Watanzania ni waoga sana wakiwa nje ya nchi,hata kama yuko full document) Elimu.

Mfano tukawekewa mazingira mazuri ya kodi nafuu za bidhaa kutoka nje zitakazoingizwa na Watanzania. Watanzania ni wachakalikaji sana. Watafutaji mno. Na bahati nzuri tuna bandari pia,tungekuwa na siasa Safi Watanzania wengekuwa #one kwenye maendeleo bara la Africa.

Tatizo letu ni CCM tu basi.
Kwa hiyo ccm wanafurahi sana kuona tunamaliza muda mwingi kwa kushabikia mpira sana kuliko kujitafuta suruhisho la maisha yetu. Ksbb ukiingia huko lazima uiguse serikali,lazima ihusike kwa asilimia kubwa kwenye kutengeneza huo unafuu.
Elimu yetu ya msingi hapa Tanzania haina tofauti sana na kwingine huko duniani.

Hayo mapanzi yanasomwa kote duniani mkuu.

Usijarajie syllabus itabadilishwa ufundishwe namna ya kufanya kazi takukuru au benki kuu hapana.

Lengo la formal education ukiachana na ajira ni kukuwezesha kufikiri vyema.

Yale mahesabu na na madude mengine yalilenga kuusaidia ubongo wako kutanuka.

Sasa kama wewe ulikuwa kasuku hutaona faida ya elimu na utazeeka ukilaumu serikali.
 
Umeuliza swali zuri sana.

Kwanza turudi nyuma kidogo, miaka ya nyuma ilikuwa kwamba timu yoyote ya Tanzania ikiwa imepangwa na timu yoyote ya Nigeria hapo ndipo ilikuwa inakuwa ni mwisho wetu.

Nakumbuka mwaka 1975 kwenye raundi ya pili tu ya klabu bingwa Afrika Yanga ilitolewa na Enugu Rangers ya Nigeria ambayo ilienda hadi fainali ya mwaka huo na kutolewa na Hafia FC ya Guinea ambayo ilitwaa taji la mwaka huo.

Baadaye nafikiri mwaka 1976 kwenye kombe la washindi Afrika, Simba ikatolewa na Ibadan Shooting Stars ya Nigeria kwenye raundi ya pili.

Baadaye mwaka 1977 kwenye raundi ya pili ya klabu bingwa Afrika Simba tena ikatolewa na Racca Rovers ya Nigeria ambapo kwenye mechi ya marudiano jijini Dar beki wa Simba Hussein Tindwa alifariki uwanjani (Uwanja wa Uhuru).

Baadaye tena nafikiri mwaka 1982 kwenye kombe la washindi Afrika timu ya Pan African akatolewa kwenye raundi ya pili na klabu ya ICC Shooting Stars ya Nigeria.

Hizo ndizo rekodi ambazo bado nazikumbuka hadi leo hii, huko nyuma timu za Tanzania zilikuwa haziwezi kabisa kutamba mbele ya vilabu vya Nigeria wakati huo ambapo wachezaji katika vilabu vya Nigeria walikuwa hawajaanza kutimkia Ulaya.

Lakini toka walipoanza kutimkia Ulaya na vilabu vya Nigeria kukosa wawekezaji basi hapo ndipo vilabu vya Nigeria vilipo poromoka kabisa kisoka.
 
Nchi zote za afrika magharibi ligi zao za ndani tia maji tia maji. Maskauti wa ulaya wameweka kambi uko. Mchezaji akiibuka tu wanamnasa fasta. Wanatuachia magarasa. Hawa wakina Yao tunaowaimba hapa kwetu, uko kwenye nchi zao vinaweza kupangwa vikosi vya timu ya taifa hata vinne na wasipate namba
 
Back
Top Bottom