Kwanza kuna ku Target wateja wa aina zote, wenye uwezo na wasio na uwezo wa kupata mfumo fulani. Kumbuka gharama zinatofautiana kati ya dishi na antenna. Pia ubora wa huduma (picha/sauti) pia zinaweza kutofautiana kati ya mtumiaji wa dishi na mtumiaji wa antenna, kwa kampuni zingine hata vifurushi vinatofautiana kati ya Dishi na antenna.
Kuhusu gharama za uendeshaji wa kampuni husika, kurusha matangazo kupitia satellite (Kwaajili ya wenye Dishi) na kurusha matangazo kwa Minara (Kwaajili ya wenye antenna) pia zinatofautiana. Lakini inabidi tu wawe na Minara na Satellite kwaajili ya kuwafikia wateja zaidi na kuwapa wateja huduma wanayohitaji kulingana na gharama za huduma na pia kulingana upatikanaji wa huduma kulingana na umbali.
Nimepata tetesi kwamba Dstv wanakuja na dikoda za antenna pia.