Kwanini kuwepo na visimbuzi vya antena na dish huku lengo lake ni lile lile?

deo paul555

JF-Expert Member
Oct 22, 2018
1,411
1,500
Habari wadau, naomba kujuzwa kwanini kumekuwepo na mfumo wa aina mbili kupata matangazo ya runinga yaani dish na antenna lengo lake ni nini ikiwa matangazo ni yale yale?

Na gharama zikoje kuendesha hiyo mifumo kwenye kampuni husika?
 
ymollel

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,811
2,000
Habari wadau, naomba kujuzwa kwanini kumekuwepo na mfumo wa aina mbili kupata matangazo ya runinga yaani dish na antenna lengo lake ni nini ikiwa matangazo ni yale yale?

Na gharama zikoje kuendesha hiyo mifumo kwenye kampuni husika?

Kwanza kuna ku Target wateja wa aina zote, wenye uwezo na wasio na uwezo wa kupata mfumo fulani. Kumbuka gharama zinatofautiana kati ya dishi na antenna. Pia ubora wa huduma (picha/sauti) pia zinaweza kutofautiana kati ya mtumiaji wa dishi na mtumiaji wa antenna, kwa kampuni zingine hata vifurushi vinatofautiana kati ya Dishi na antenna.

Kuhusu gharama za uendeshaji wa kampuni husika, kurusha matangazo kupitia satellite (Kwaajili ya wenye Dishi) na kurusha matangazo kwa Minara (Kwaajili ya wenye antenna) pia zinatofautiana. Lakini inabidi tu wawe na Minara na Satellite kwaajili ya kuwafikia wateja zaidi na kuwapa wateja huduma wanayohitaji kulingana na gharama za huduma na pia kulingana upatikanaji wa huduma kulingana na umbali.

Nimepata tetesi kwamba Dstv wanakuja na dikoda za antenna pia.
 
Ohhh ahsante,niliwahi sikia tetesi kua satellite ni gharama kubwa kuliko minara ya antena,ngoja tusubiri hao ulisema wanaleta
 
Heisenberg

JF-Expert Member
Apr 26, 2017
1,166
2,000
Kuna issue kadhaa hapa

1. Sattelite ina wide range ya beam. Mfano, sattelite moja inaweza mwaga beam Nusu ya bara la afrika. mfano azam TV kwa sattelite wanayotumia hata ukiwa Malawi, uganda, sudani Zambia kote huko utaipata lakini kwa Minara ya ardhini (Telestrial) inaweza rusha matangazo kwenye Kipenyo cha (radius) Km 50

2. Ubora wa picha. Sattelite ina ubora wa picha kutokana kuwa na bandwith kubwa kuliko masafa ya minara ya ardhini. kwa sattelite unaweza pokea Video ya Full HD hata 4k wakati kwa minara ni kazi sana picha lazima itasumbua au kukwama kwama
 
Ahsante, je ni kweli wenye visimbuzi wanalipa gharama kubwa kwajili ya malipo ya satellite? Na tv moja moja km ITV Yale masafa yake hulipa gharama gani kwenye wamiliki wa satellite? Manake kwenye madish ya FTA tunawapa ikoje hii?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom