mkorosho
JF-Expert Member
- Dec 9, 2016
- 554
- 608
Deuteronomy cap 28Kitabu gani cha biblia kinasema hivo mkuu!!
Deuteronomy cap 28Kitabu gani cha biblia kinasema hivo mkuu!!
Umejibu Upande Mmoja, na Kukosa Ustaarabu kwetu nako Unakuonaje? Kunyanyasana, Kuoneana Kukandamizana, Kukosa Ujuzi wa Mambo mengi tu zaidi ya Kuwaiga hao hao Ngozi Nyeupe, na Mambo Chungu Mzima!
Samahani, nami nikuulize. Uliona rangi zao za ngozi? Au ndani ya Biblia imeandikwa kuwa, rangi ya ngozi ya Adamu ilikuwa sawa na rangi ya ngozi ya Hawa?naomba nikusahihishe kidogo Mungu alimuumba watu wawili tu na wote walikuwa wanafanana swali ni je hizi tofauti zetu zimetokea wapi?
colonial mentality.Salaam Wandugu!
Ni Jambo ambalo najiuliza kila Uchao, kama kweli Uumbaji wa Mungu Ulikuwa ni wa Haki, Kwanini Kuliwekwa Matabaka ya Ngozi muonekano, yaani Nyeupe na Nyeusi? Mbaya Zaidi, Ngozi Nyeusi ni kama ina Laana Fulani hivi, Matatizo yote kwa Asimilia Kubwa yanatokea kwa Ngozi Nyeusi! Angalia Kutesana, Kudharauriana, Kukandamizana kwa Wenye Madaraka dhidi ya wasio na Madaraka (Siasa Mpaka Ofisini) pamoja kwa wenye Mali na Masikini!
Nimeandika hivi naona kama Kuna Tatizo Mahala, maana Duniani Kote ambapo Waafrika Ndiyo Weusi peke yao. Hapa haijalishi Labda Mataifa mengine Duniani mfano, Wachina, Waarabu nk, sawa muonekano wapo Tofauti Ila wanaunganishawa na Rangi yao, yaani Nyeupe!
Je, Waafrika tulilaaniwa na Ndiyo maana tunafanana na Giza (Nyeusi), na Nani Katulaani? Na Je, kuna Sababu yeyote ya Kisayansi ndiyo tukaumbwa kwa Rangi hii yaani ya giza?
Karibuni kwa Kuelimishana wana Intelligence.
Sijabagua, nimesema Ngozi Nyeusi, vinginevyo huyo Bwana Mdogo (Yaani Baba) alikuw/ama ni Mchina na Vinginevyo!Mimi Baba yangu hajalaaniwa kwa maana siamini hivyo, nimekuuliza wewe unayesema kwamba watu weusi tumelaaniwa, sasa kama unaamini hivyo ina maana unaamini pia kwamba Baba yako mzazi ambaye ni mweusi amelaaniwa?
Na Kikubwa Jibu Hoja na Si Baba yako baba yako hapa, huo ni Utoto! Tunahitaji hoja zenye Mashiko!Mimi Baba yangu hajalaaniwa kwa maana siamini hivyo, nimekuuliza wewe unayesema kwamba watu weusi tumelaaniwa, sasa kama unaamini hivyo ina maana unaamini pia kwamba Baba yako mzazi ambaye ni mweusi amelaaniwa?
Ahsante kwa Mchango wako! Kwenye ya Pili hapo Ishu kweli, inamaana Kuzaliwa Afrika ndiyo Unakuwa Mtu wa Hovyo hovyo si Ndivyo?Ndg Ndikwega kuhusu rangi whether is black or white Kuna nadharia kazaa mfano biblical writing and evolutionally outlook (am standing to be corrected) ww una base zaidi kwenye bible kwa ktu moja inaitwa HAMITIC MYTH
Hapa wazungu na wote wenye ngoz nyeupe wanajiaminisha kwamba ss weus n zao la ham mtt wa Nuhu aliyemcheka baba ake akiwa uchi
Hvo bwana/bi Ndikwega Nuhu alitoa laaana kwa Ham kwa kusema hv .......... Utakuwa mtumwa wa wezio na mbali utaenda kuishi na uzao wako utalaaaniwa pia.... Inasemekana uzao wa ham uliaz kuwa na ngoz nyeus ......... Hiyooo n hamitic myth
Lkn upande wa kisayans tuna amin is just environmental factor wa jf coz hata mwafrika wa ulaya s sawaa na wa huku dabaga hii kwa cc tuliobahatika kwenda had elim za mbele is just adaptation of organism to ze environment from survival for fittest theory wajamen hapa nmejaribu kwa kifup ( i stand to b corrected)
wacha kufikiri kwa kutumia makali.o .kichwa kisichofikiri ni mzigo kwa mwili.Who is Unconquered in Africa? Stop this stupid Idea(s)
hahah miti haikuumbwa binadamu aliumbwa tena kwa mfano wa Mungu sijui unaelewaje hapo miti Mungu alinena iwe miti ya kila aina nayo ikawa hivo lakini Mungu alimuumba binadamu anayefanana ndo maana ya kwa mfano wetu kama alivosema kwenye kitabu cha biblia turudi kwenye swali hizi tofauti zimetoka wapi?Samahani, nami nikuulize. Uliona rangi zao za ngozi? Au ndani ya Biblia imeandikwa kuwa, rangi ya ngozi ya Adamu ilikuwa sawa na rangi ya ngozi ya Hawa?
Mistari konde, kuna wakati uki ifikilia sana hii dunia hupati majibu kamili.. Mtu mweusi "kama tunavyoitwa" katawanyika kila kona ya dunia hii. Wayahudi na Wapalestina weusi mpaka leo wanadai Israel ni Afrika ya Kaskazini. Wakihoji kama ipo Mashariki ya Kati, mbona hakuna Magharibi ya Kati?15 Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
16 Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.
17 Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia.
18 Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.
19 Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo,
20 Bwana atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.
21 Bwana atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki.
22 Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.
23 Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma.
24 Bwana atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie.
25 Bwana atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huko na huko katika falme zote za duniani.
26 Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza.
27 Bwana atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.
28 Bwana atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;
29 utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.
30 Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda yake.
31 Ng'ombe wako atachinjwa mbele ya macho yako, usile nyama yake; utanyang'anywa punda wako mbele ya uso wako kwa jeuri, usirudishiwe; kondoo zako watapewa adui zako, usipate mtu wa kukuokoa.
32 Wanao na binti zako litapewa taifa lingine, na macho yako yataangalia, na kuzimia kwa kuwatamani mchana kutwa; wala hapatakuwa na kitu katika uwezo wa mkono wako.
33 Matunda ya nchi yako, na taabu yako yote, vitaliwa na taifa usilolijua; utaonewa tu, na kupondwa chini daima;
34 hata uwe mwenye wazimu kwa yaonwayo na macho yako, utakayoyaona.
35 Bwana atakupiga magoti na miguu kwa jipu lililo zito, usilopata kupozwa, tokea wayo wa mguu mpaka utosi wa kichwa.
36 Bwana atakupeleka wewe, na mfalme wako utakayemweka juu yako, kwa taifa usilolijua wewe wala baba zako; nawe huko utatumikia miungu mingine ya miti na mawe.
37 Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza Bwana.
38 Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila.
39 Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala hutakunywa katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu.
40 Utakuwa na mizeituni katika mipaka yako yote usijipake mafuta yake; kwa kuwa mzeituni wako utapukutika.
41 Utazaa wana na binti, lakini hawatakuwa wako wewe; kwa sababu watakwenda utumwani.
42 Miti yako yote, na mazao ya nchi yako, nzige watakuwa nayo.
43 Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako; nawe utazidi kushuka chini.
44 Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni kichwa, wewe utakuwa mkia.
45 Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza;
46 nazo zitakuwa juu yako kwa ishara na ajabu, na juu ya uzao wako milele;
47 kwa kuwa hukumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote;
48 kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta Bwana juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza.
49 Bwana atakuletea taifa juu yako kutoka mbali, kutoka ncha ya dunia, kama arukavyo tai; taifa usiloufahamu ulimi wake;
50 taifa lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei kijana;
51 naye atakula uzao wa ng'ombe wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako mpaka utakapokwisha kuangamizwa; wala hatakuachia nafaka, wala divai, wala mafuta, wala maongeo ya ng'ombe wako, wala wana-kondoo wako, hata atakapokwisha kukuangamiza
Hakumlaani Ham alimlaani mtoto wa Ham aka KAANANI. Usilishe watu matango poriKitabu cha mwanzo 10:1 na kuendelea baada ya gharika Nuhu alikuwa na watoto watatu Shem, Yafet na Hamu siku moja Nuhu alikunywa mvinyo akalewa huku akiwa uchi mwanae Hamu alimwona akamcheka lakini ndugu zake wakachukua mavazi wakaenda kinyumenyume wakamfunika alipoamka asubuhi akaambiwa hizo habari alikasirika akamwita Hamu na kumlaani kwamba atakuwa mtumwa wa nduguze basi Hamu akamzaa Misri akaishi Misri, akamzaa putin akaishi somalia, akamzaa Havila akaishi libya pia akamzaa Kush akaishi Ethiopia na pia akamzaa Seba akaishi Ethiopia hao walilaaniwa kutokana na kitendo cha baba yao ila kwa sasa hatupo chini ya hiyo laana Bwana Yesu Kristo alitukomboa pale msalabani kilichobaki ni waafrica kujitambua.