Demokrasia, haki za kiraia, uhuru wa mawazo na uwajibikaji vimekuwa machukizo ya Mtawala wa Awamu hii. Mauaji, vitisho, rushwa, uonevu na kushindwa ndio vimetamalaki Tanzania kwa sasa.
Lakini najipa moyo kwa sababu hayo hapo juu sio mwisho wa habari:-
1) 21 Novemba 2017 Robert G. Mugabe Rais dikteta waZimbabwe aliondoka madarakani bila vita wala kupitia sanduku la kura.
2) 14 Februari 2018 Jacob G. Zuma Rais mtata wa Afrika Kusini aliondoka madarakani bila vita wala kupitia sanduku la kura.
3) 15 Februari 2018 Hailemariam Disalegne Waziri Mkuu wa Ethiopia aliondoka madarakani bila vita wala kupitia sanduku la kura.
Ukiangalia hapo kati ya siku Mugabe na Hailemariam wanaondoka madarakani utaona ni jumla ya siku 87 tu. Yaani wastani wa Kiongozi mmoja kuondoka madarakani kila baada ya siku 29 tu! Tena kwa Zimbabwe na Ethiopia hali ya utawala na udikteta ilikuwa ni mbaya zaidi kuliko Tanzania, kwa kipindi kirefu tu. Kwa hiyo na hapa kwetu tusife moyo Mwenyezi Mungu yuko kazini. Siku, saa na majira yake havikawii giza letu litapita nasi tutaona mapambazuko na nuru njema kutuzukia Watanzania.
Walipita watawala wakubwa, wenye nguvu na wenye kutisha dunia nzima wachilia mbali ndani ya nchi zaod zaidi ya huyu, hivyo huyu naye atapita.