Kwanini kura za Mtulia zimepungua kwa zaidi ya 60%?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,558
Kwa mujibu wa magazeti ya leo ni kwamba pamoja na Mtulia kushinda kwa kishindo kwa kupata kura 30,000 plus, lakini kura hizo ni pungufu kwa zaidi ya kura 40,000 plus ukilinganisha na kura alizopata mwaka 2015. Hii inamaanisha nini kwenye demokrasia?

Chanzo: Magazetini!
 
Kwa mujibu wa magazeti ya leo ni kwamba pamoja na Mtulia kushinda kwa kishindo kwa kupata kura 30,000 plus, lakini kura hizo ni pungufu kwa zaidi ya kura 40,000 plus ukilinganisha na kura alizopata mwaka 2015. Hii inamaanisha nini kwenye demokrasia?....source Magazetini!
Dsm nw ccm hawana chao .. na ndio kwanz kazi inaanz..sas kuna watu wabshi sana hasa wakiwa na uelewa juu ya jambo fulan..... Wavivu wa kufikiri na wale wanaojfnya wabakpenda chama(ccm) na wale wote wenye tamaa ya madaraka na fedha ndio pekee watakaobaki kuipenda ccm .... Hmna kpya anachofny Magugu knachowez kuisaidia ccm zaid anazd kuipoteza tu
 
Hata kama wangepiga kura 10 tu na mtulia kapata kura 6 angetangazwa mshindi
 
Tafuta kwanza tofauti ya kura 18,000 zilizopo kàti ya chagadema na chichiemu ndo uje utafute tofauti ya kura za 2015 na za sasa.
 
Kwasabab hakubariki na wenye akili timamu tena, na hapo ni baada ya kuiba ila angewez pata ata 5000 tu za mambumbumbu
We unaona kura 5000 ni ndogo?......pale bungeni wapo wabunge waliochaguliwa kwa kura 2000 tu!
 
Tuliwaambia mapema, baada ya Uchaguzi mtakuwa mnakuja na thread za kujifariji mkabisha !
 
Kwa mujibu wa magazeti ya leo ni kwamba pamoja na Mtulia kushinda kwa kishindo kwa kupata kura 30,000 plus, lakini kura hizo ni pungufu kwa zaidi ya kura 40,000 plus ukilinganisha na kura alizopata mwaka 2015. Hii inamaanisha nini kwenye demokrasia?....source Magazetini!
Hivi kweli unaamini haya matokeo yanayopangwa Lumumba ...............!!?
 
Hata kama wangepiga kura 10 tu na mtulia kapata kura 6 angetangazwa mshindi
Binafsi sizungumzii mshindi hilo linajulikana hata Marekani kuna wakati Rais anachaguliwa na watu chini ya 10. Concern yangu ni tafsiri ya kidemokrasia na hapa Prof Kitila angeweza kunipa majibu mazuri zaidi!
 
Sababu wapiga kura hawakujitokeza kwa wingi kupiga kura wakiohofia Kinondoni "Kugeuzwa majivu..." Kwa mujibu wa mfunga kampeni za Chadema, mheshimiwa sana Mbowe
 
Hilo gazeti nafikiri wangeandika hivi UKAWA mgombea ubunge wao 2015 alipata kura elfu 70 safari hii mgombea wao wa UKAWA Salum Mwalimu kapata kura elfu 12 ambazo ni pungufu ya kura elfu 58 ukilinganisha na za 2015 inamaanisha nini kwa UKAWA?
 
Demokrasia, haki za kiraia, uhuru wa mawazo na uwajibikaji vimekuwa machukizo ya Mtawala wa Awamu hii. Mauaji, vitisho, rushwa, uonevu na kushindwa ndio vimetamalaki Tanzania kwa sasa.

Lakini najipa moyo kwa sababu hayo hapo juu sio mwisho wa habari:-

1) 21 Novemba 2017 Robert G. Mugabe Rais dikteta waZimbabwe aliondoka madarakani bila vita wala kupitia sanduku la kura.

2) 14 Februari 2018 Jacob G. Zuma Rais mtata wa Afrika Kusini aliondoka madarakani bila vita wala kupitia sanduku la kura.

3) 15 Februari 2018 Hailemariam Disalegne Waziri Mkuu wa Ethiopia aliondoka madarakani bila vita wala kupitia sanduku la kura.

Ukiangalia hapo kati ya siku Mugabe na Hailemariam wanaondoka madarakani utaona ni jumla ya siku 87 tu. Yaani wastani wa Kiongozi mmoja kuondoka madarakani kila baada ya siku 29 tu! Tena kwa Zimbabwe na Ethiopia hali ya utawala na udikteta ilikuwa ni mbaya zaidi kuliko Tanzania, kwa kipindi kirefu tu. Kwa hiyo na hapa kwetu tusife moyo Mwenyezi Mungu yuko kazini. Siku, saa na majira yake havikawii giza letu litapita nasi tutaona mapambazuko na nuru njema kutuzukia Watanzania.

Walipita watawala wakubwa, wenye nguvu na wenye kutisha dunia nzima wachilia mbali ndani ya nchi zaod zaidi ya huyu, hivyo huyu naye atapita.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom